Hatimaye vivo Y11 yavunja rekodi ya simu zangu

Nipe tofauti kubwa ya tecno na samsung mkuu...

ni kama tofauti zilizoko kwenye vits na benz ndugu.
ni ngumu kuzielezea maana ni mpaka ushike vyote kwa wakati ndio utajua.

hapa hata nikikweleza kioo kizuri hujui hata kinafananaje.
 
Katika maisha yangu simu ya kwanza kununua ni Siemens kidole mwaka 2007 mkononi. Sikuwa na matumizi sana wala maana yeyote kwangu.

Miaka kabla ya android kuwa maarufu na kuenea TZ ulikuwa unanunua simu kwa kuulizia vitu mfano ina radio? Au ina bluetooth, memory card n.k.

2010 nikanunua nokia

View attachment 1724133


6030,kwangu ilikua simu ya maana sana sababu ilikua na radio,GPRS,kioo cha rangi,MMS na kanafasi kadogo tu. Sikumaliza nayo mwaka kwani kila simu niliyoona niitamani. Ikawa michezo yangu kubadilisha simu haijalishi nimekaa nayo muda gani.

Simu zote zilikua zimetumika(used) sababu simu dukani zilikua bei kubwa sana,mf nokia 6030 mpya ilikua 220,000,lakini used 60,000.

NOKIA YATAMBA
Kufika 2012,nilishatumia manokia mengi sana,nikaingia dukani
View attachment 1724134
kuchukua simu mpya nokia X2-02 hii ilikua inakuja na kitu kinaitwa play via radio yani unacheza nyimbo kwenye simu kwenda radioni bila waya. Niliipenda lakini bado haikutosha sababu WhatsApp ilikua tayari gumzo(kutumiana picha na video) nikauza kwa hasara,nikachukua nokia E 63.

Hii ilikuwa na uwezo sana,OS yake ilikua symbian ina 3G kamera kali sana ila sikudumu nayo sababu keyboard ya QWERTY sikuizoea nikauza nikachukua nokia E52. Hii nilipenda sana ilikua slim
View attachment 1724136


symbianOS 3G nikakaa nayo miezi 6 Tecno wakavamia soko gafla kwa kushtukiza. E72 ikapoteza mvuto.

ULIMWENGU WA TOUCH WAJA
Nashika touch yangu ya kwanza ikiwa android smartphones Tecno P3 yenye sifa
Ram MB504 ndani 2GB 📷 MP 5 bei rahisi kuliko nokia zote nilizotumia yaani 150k tu mpya. Baada ya kujaa vitu ikageuka kuwa kero tena.

Basi mwendo ukawa ni bandika bandua 2016 nilinunua Tecno J5 nilikaa nayo miezi 10 tu,muda mrefu kuliko simu zote,nikauza nikajipinda nikachukua Huawei Y6 ilidumu miezi 11 sababu niliipenda sana hata kuuzwa kwanke nililazimishwa sana.

2017 Nikachukua Infinix hot 5 kavu miez 11 ikaibiwa,hii ndio simu yangu ya kwanza kuibiwa na ikawa gundu,2019 ulefone note 7P miezi mi4 ikaibiwa ila nikaitrack nikaipata mana sikuweka lock.

Kutokana na umuhimu wa simu kwangu nilitaka kwenda kuchukua infinix lakini nikakuta vivo ndio zimeingia soko la Tanzania. Nikakagua nikaipenda nikachukua vivo Y11 yenye sifa hizi
  • Storage 32GB
  • Ram GB 3
  • 📷 16 MP
  • Android 9.
  • 🔋 lake 5000mAh
OS yao i anaitwa funtouch yenye interface kama iphone flani yani tofauti na simu za android nyingine.

View attachment 1724137

320k nikalipa,hii pesa siijuitii,hii simu haijawahi kuniangusha ila mimi ndio nimeiangusha mara nyingi tu,mara ya mwisho ilianguka urefu wa 9ft haikuvunjika ila motherboard ikaanza kupinda,kioo chake kilivyokuwa kigumu kikapinda na hiyo mazabodi yake. Ilivyozidi kikajifumua upande lakini kikiwa kizima vilevile.

Kwa sasa imepita miezi 12 na siku zaidi ya 15,simu ina krek kidogo lakini haisumbui hata kidogo,hapa nasubiri android 10 muda wowote tutawekewa,sijawah kukaa na simu nyingine muda mrefu hivi.

Wewe mdau simu yako kukaa nayo muda mrefu ni ipi? Uliyoipenda sio kwa sababu ulikosa pesa ya kununua nyingine.
Uliwezaje ku track hio simu na kuipata
 

Tumia hiyo☝️ app
Asante mkuu

Nime download na ku sign in.

Location inanionesha, in my hand.
Screenshot_20210421-142637.png


Je, ikiwa mbali na mimi napaswa kwenda kwenye computer au kufanyaje?

Na naionaje namba ya simu ya mtumiaji?
 
Asante mkuu

Nime download na ku sign in.

Location inanionesha, in my hand.
View attachment 1759258

Je, ikiwa mbali na mimi napaswa kwenda kwenye computer au kufanyaje?

Na naionaje namba ya simu ya mtumiaji?
Kwenye computer au hata simu nyingine afu kwenye app unaingia kama guest unaweka email na password yako kisha utaona kifaa kilipo,mtandao kinaotumia kama kwenye photos ulikua umeweka auto backup badi hata picha utakuwa unaziona mwiz wako akijipiga
 
Back
Top Bottom