Hatimaye vivo Y11 yavunja rekodi ya simu zangu

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,328
2,283
Katika maisha yangu simu ya kwanza kununua ni Siemens kidole mwaka 2007 mkononi. Sikuwa na matumizi sana wala maana yeyote kwangu.

Miaka kabla ya android kuwa maarufu na kuenea TZ ulikuwa unanunua simu kwa kuulizia vitu mfano ina radio? Au ina bluetooth, memory card n.k.

2010 nikanunua nokia

images.jpeg-2.jpg



6030,kwangu ilikua simu ya maana sana sababu ilikua na radio,GPRS,kioo cha rangi,MMS na kanafasi kadogo tu. Sikumaliza nayo mwaka kwani kila simu niliyoona niitamani. Ikawa michezo yangu kubadilisha simu haijalishi nimekaa nayo muda gani.

Simu zote zilikua zimetumika(used) sababu simu dukani zilikua bei kubwa sana,mf nokia 6030 mpya ilikua 220,000,lakini used 60,000.

NOKIA YATAMBA
Kufika 2012,nilishatumia manokia mengi sana,nikaingia dukani
images.jpeg.jpg

kuchukua simu mpya nokia X2-02 hii ilikua inakuja na kitu kinaitwa play via radio yani unacheza nyimbo kwenye simu kwenda radioni bila waya. Niliipenda lakini bado haikutosha sababu WhatsApp ilikua tayari gumzo(kutumiana picha na video) nikauza kwa hasara,nikachukua nokia E 63.

Hii ilikuwa na uwezo sana,OS yake ilikua symbian ina 3G kamera kali sana ila sikudumu nayo sababu keyboard ya QWERTY sikuizoea nikauza nikachukua nokia E52. Hii nilipenda sana ilikua slim
images.jpeg-3.jpg



symbianOS 3G nikakaa nayo miezi 6 Tecno wakavamia soko gafla kwa kushtukiza. E72 ikapoteza mvuto.

ULIMWENGU WA TOUCH WAJA
Nashika touch yangu ya kwanza ikiwa android smartphones Tecno P3 yenye sifa
Ram MB504 ndani 2GB 📷 MP 5 bei rahisi kuliko nokia zote nilizotumia yaani 150k tu mpya. Baada ya kujaa vitu ikageuka kuwa kero tena.

Basi mwendo ukawa ni bandika bandua 2016 nilinunua Tecno J5 nilikaa nayo miezi 10 tu,muda mrefu kuliko simu zote,nikauza nikajipinda nikachukua Huawei Y6 ilidumu miezi 11 sababu niliipenda sana hata kuuzwa kwanke nililazimishwa sana.

2017 Nikachukua Infinix hot 5 kavu miez 11 ikaibiwa,hii ndio simu yangu ya kwanza kuibiwa na ikawa gundu,2019 ulefone note 7P miezi mi4 ikaibiwa ila nikaitrack nikaipata mana sikuweka lock.

Kutokana na umuhimu wa simu kwangu nilitaka kwenda kuchukua infinix lakini nikakuta vivo ndio zimeingia soko la Tanzania. Nikakagua nikaipenda nikachukua vivo Y11 yenye sifa hizi
  • Storage 32GB
  • Ram GB 3
  • 📷 16 MP
  • Android 9.
  • 🔋 lake 5000mAh
OS yao i anaitwa funtouch yenye interface kama iphone flani yani tofauti na simu za android nyingine.

IMG_20210312_205222.jpg


320k nikalipa,hii pesa siijuitii,hii simu haijawahi kuniangusha ila mimi ndio nimeiangusha mara nyingi tu,mara ya mwisho ilianguka urefu wa 9ft haikuvunjika ila motherboard ikaanza kupinda,kioo chake kilivyokuwa kigumu kikapinda na hiyo mazabodi yake. Ilivyozidi kikajifumua upande lakini kikiwa kizima vilevile.

Kwa sasa imepita miezi 12 na siku zaidi ya 15,simu ina krek kidogo lakini haisumbui hata kidogo,hapa nasubiri android 10 muda wowote tutawekewa,sijawah kukaa na simu nyingine muda mrefu hivi.

Wewe mdau simu yako kukaa nayo muda mrefu ni ipi? Uliyoipenda sio kwa sababu ulikosa pesa ya kununua nyingine.
 
Nakumbuka Tecno H6 nilikaa nayo kma miaka mi 3 hivi nikapiga custom ROM maisha yalikua mazuri mpka ikaja kuzingua charging system.

Nyingine ni Samsung A50 ningekua nafikisha mwaka wa pili kuwa nayo ila wadau waliniibia waka jana October. Ni kati ya simu ambayo niliridhika nayo.

Sasa nimehamia Google Pixel, na hapa ndio sina mawazo ya kununua simu nyingine kabisa. Labda iharibike au ipotee. Lakini hii Pixel 3a ni uhakika haina shida yoyote kwa matumizi ya kila siku. Camera kali na unapata updates mapema sana. Sshv nipo kwenye Android 11, android 12 beta ipo tayari kma unaitaka mda wowote unainstall tu.
 
Hyo niliagiza nje kwa laki 5 hvi baada ya kila kitu. Hii niliibahatisha yaani kupitia jamaa mmoja aliyekua anatoka huko. Maana watu wanaziuza huku bongo used kwa laki 6 hadi 7.
Nimeona,ya ukweli sana, product ya wenye OS yao(Google)
 
Nilianzia Phillips, kisha nokia 3310 halafu nokia 6 botton maarufu enzi hizo, nikaibukia motorola L6, nikarudi nokia 6230i vintage then nokia N80, nikahamia blackberry kipindi hicho BBM ni maarufu sana, ilipoingia whatsap nikahamia sumsung, nikianzia S3, S5, nikahamia J series, nikaishia J7 nikaamua kuhamia ios, nikianzia iphone 5SE, nimekuwa nikipanda nazo hadi sasa nipo na mini iphone 12 na sumsung A70 sijawahi kujutia kuzitumia, nyingine hadi leo zipo nimezihifadhi zinafanya kazi! Ila Phillips niliipenda sana aisee
 
Nilianzia Phillips, kisha nokia 3310 halafu nokia 6 botton maarufu enzi hizo, nikaibukia motorola L6, nikarudi nokia 6230i vintage then nokia N80, nikahamia blackberry kipindi hicho BBM ni maarufu sana, ilipoingia whatsap nikahamia sumsung, nikianzia S3, S5, nikahamia J series, nikaishia J7 nikaamua kuhamia ios, nikianzia iphone 5SE, nimekuwa nikipanda nazo hadi sasa nipo na mini iphone 12 na sumsung A70 sijawahi kujutia kuzitumia, nyingine hadi leo zipo nimezihifadhi zinafanya kazi! Ila Phillips niliipenda sana aisee
Tunatofautiana kidogo sana sema iPhone ndio sikuwahi kuipenda kabisa
 
Back
Top Bottom