Hatimaye Uhuru Kenyatta akubali wakenya wafuate njia za Magufuli za kuishi na Corona kama wanavyoishi na HIV na Malaria

oneflash

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
808
586
joto la jiwe,

Mfano wa kuigwa na nani?. Curfew bado iko, maeneo ya burudani na vileo bado yametingwa, shule bado zimefungwa, kuvaa barakoa kwa umma ni lazima, kupima na kuwalaza waathiriwa n.k. kwa yale nimetaja ni kinyume na msimamo wa jiwe!
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
5,740
5,996
Greetings friends all over the region !

Nimekutana na hii article imeniacha ktk swali happens for kenyans

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
19,533
25,058
joto la jiwe,

Huu ni upotoshaji wa wazi. Kenya, kwa hotuba ya Kenyatta leo:

1. Vilabu vyote vya pombe vimepigwa kufuli.
2. Curfew ya usiku 2100 - 0500 iko kazini
3. Anasisitiza kutojidanganya kama nchi zisizokuwa na demokrasia kuwa hawana Corona. Anasema hawana Corona vipi?
4. Kasisitiza Corona siyo siasa
5. Kwenda kanisani au sokoni leo si kama ilivyokuwa juzi.
6. Ametaka wastaafu wa afya pia kurejea kazini.
7. Nk, nk.

Yote haya #1 na #2 kwa siku 30.

Haya ndiyo ya Magufuli hayo? Au ndiyo kujitekenya na kucheka wenyewe?

Mbona mnaweweseka hivyo hata kwa ku fake news?

Source BBC Swahili leo.
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,506
2,645
Huu ni upotoshaji wa wazi. Kenya, kwa hotuba ya Kenyatta leo:

1. Vilabu vyote vya pombe vimepigwa kufuli.
2. Curfew ya usiku 2100 - 0500 iko kazini
3. Anasisitiza kutojidanganya kama nchi zisizokuwa kuwa na demokrasia kuwa hawana Corona. Anasema hawana Corona vipi?
4. Nk, nk.

Yote haya kwa siku 30.

Haya ndiyo ya Magufuli?

Mbona mnaweweseka hivyo hata kwa ku fake news?

Source BBC Swahili leo.

Kwenye hii ishu ya korona huyo nyamera anaongelea demokrasia au tumbokrasia?
 
Sherlock

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
1,373
1,329
"Sisi kama taifa, hatuna nguvu ya kuficha chochote. Kuna wengine ambao wana huo uwezo lakini sisi twajivunia kuwa demokrasia" - President Uhuru Kenyatta

#UhurusToughChoices

Screenshot_20200727-185746.png
 
komora096

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
20,513
5,601
Mfano wa kuigwa na nani?. Curfew bado iko, maeneo ya burudani na vileo bado yametingwa, shule bado zimefungwa, kuvaa barakoa kwa umma ni lazima, kupima na kuwalaza waathiriwa n.k. kwa yale nimetaja ni kinyume na msimamo wa jiwe!..
Utamfanya huyi jiwe la joto atokwe na povu.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
19,533
25,058

MY TAKE: Wale waliokua wanabisha kwamba "Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na Corona" bado Wapo?. Tanzania baba lao, Magufuli akili kubwa Sana.

Fake news kwa maslahi ya nani?

Apumzike kwa amani mzee wetu rais mstaafu Mkapa. Mzee wa muwazi na ukweli.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
7,121
17,881
Madagascar, Morocco wame-lockdown nchi juzi. Unasemaje juu ya hao? Wamefuata njia ya nani?

MY TAKE: Wale waliokua wanabisha kwamba "Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na Corona" bado Wapo?. Tanzania baba lao, Magufuli akili kubwa Sana.
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,855
13,219
Mfano wa kuigwa na nani?. Curfew bado iko, maeneo ya burudani na vileo bado yametingwa, shule bado zimefungwa, kuvaa barakoa kwa umma ni lazima, kupima na kuwalaza waathiriwa n.k. kwa yale nimetaja ni kinyume na msimamo wa jiwe!..
Achana nao hawa, hutawaelewa virahisi. Ukisikia Tz ni kichwa cha mwendawazimu usije ukadhani wanasingiziwa. Kwao Corona sio 'health issue' ni security issue na political issue, yaani ni suala la kiusalama na kisiasa sio kiafya. Mmoja wao akidhubutu kutoa ripoti zinazokinzana na za serikali kuhusu Corona anajipata matatani.

Magazeti nayo yanafungiwa, wataalamu wa afya kwa uoga wamebaki kimya. Mwendo ni wa kutumia janga la Corona kutafuta kiki za kisiasa na kumsifia 'mtakatifu' kwa vitu vya kipumbavu na sanasana kuwakomoa wapinzani. Imekuwa ni production moja kali ya filamu ya comedy.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
23,168
38,665
Achana nao hawa , hutawaelewa virahisi. Ukisikia Tz ni kichwa cha mwendawazimu usije ukadhani wanasingiziwa. Kwao Corona sio 'health issue' ni security issue na political issue, yaani ni suala la kiusalama na kisiasa sio kiafya. Mmoja wao akidhubutu kutoa ripoti zinazokinzana na za serikali kuhusu Corona anajipata matatani. Magazeti nayo yanafungiwa, wataalamu wa afya kwa uoga wamebaki kimya. Mwendo ni wa kutumia janga la Corona kutafuta kiki za kisiasa na kumsifia 'mtakatifu' kwa vitu vya kipumbavu na sanasana kuwakomoa wapinzani. Imekuwa ni production moja kali ya filamu ya comedy.
Hamkusikia Uhuru aliposema kwamba watu walitegemea kwamba ningetangaza total lock down kutokana na hali ya maambukizi ilivyo lakini hilo haliwezikani, hiyo ni sera ya nani kukataa kutangaza knockdown kama sio Magufuli?

Mwenzi mmoja uliopita Uhuru alisema kwamba baada ya siku 21 kama maambukizi yataongezeka kwa kasi atalazimika kurudisha counties za Nairobi, Mombasa katika "knockdown", iweje amebadilisha uamuzi huo wakati hali ya maambukizi ndio inazidi kuwa mbaya zaidi?

Wacheni kujaribu kuficha, ukweli ni kwamba Uhuru anaiga Magufuli hatua kwa hatua, hakukuwa na sababu yoyote ya kutokurudisha Nairobi Katina "lock down" kama alivyoahidi, iweje kipindi hiki ambacho maambukizi ndio yaneongezeka Kwa kasi anafikiria kufungua anga la Kanya na kuruhusu watalii?, huko ni kumuiga Magufuli.

Vipi huyu pia anaficha ukweli?

oneflash

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
808
586
Ha

Hakuna kitu sisi tunajifunza kwa Tanzania. Tunafanya mambo kivyetu. Hata sisi tunaweza sema Afrika kusini wametuiga kwa kuweka curfew. Burundi wanasisitiza sasa Kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa. Madagascar nao ndio hao na lockdown.
 
kennedy0000

JF-Expert Member
Apr 14, 2012
3,979
3,158
Mfano wa kuigwa na nani? Curfew bado iko, maeneo ya burudani na vileo bado yametingwa, shule bado zimefungwa, kuvaa barakoa kwa umma ni lazima, kupima na kuwalaza waathiriwa n.k. kwa yale nimetaja ni kinyume na msimamo wa jiwe!..

Forgive them. They can't understand English.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom