Hatimaye Subhash Patel amvaa Reginald Mengi

DIKTETA

Member
Mar 28, 2008
55
1
Jana tarehe 30 april Ndg Subhash Patel kupitia kwa wakili wake Julius Lugazya kawafungulia kesi wahariri na magazeti yao ya nipashe na guardian, wakurugenzi wa radio uhuru na ITV pamoja na mwenyekiti wao Mengi kwa kashfa za kumuita fisadi papa na kudai alipata Mchuchuma kwa mizengwe. Anawataka waombe radhi ndani ya siku saba na wamlipe fidia ya shs bilioni kumi.
 
Mengi alijiandaa kuongea yale aliyoyasema, sio kuwa aliropoka tu. Hivyo huyu fisadi papa ni bora aende mahakamani au akae kimya kukubali tuhuma sio kuomba aombwe radhi. Hii ni ajabu kweli, yaani umetuhumiwa na kukashifiwa, then unamuomba mtu akuombe radhi?
 
Don't you wish you could have an opportunity to punch one of mafisadi? Unamtandika moja barabara, wao si wanaendaga kutibiwa nje? Atapona tu.
 
Jana tarehe 30 april Ndg Subhash Patel kupitia kwa wakili wake Julius Lugazya kawafungulia kesi wahariri na magazeti yao ya nipashe na guardian,wakurugenzi wa radio uhuru na ITV pamoja na mwenyekiti wao Mengi kwa kashfa za kumuita fisadi papa na kudai alipata mchuchuma kwa mizengwe.Anawataka waombe radhi ndani ya siku saba na wamlipe fidia ya shs bilioni kumi

Mchezo unaelekea kuwa mtamu sasa...hebu tukae mkao wa kula, tushuhudie yatayojiri! I hope masaa 48 ya RA aliyompa Mengi yamepita, nini kitafuata???...
 
Huyu ndiye aliyekuwa mweka hazina wa kamati ya mtandao wakati wa kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa CCM yeye ndiye alikuwa anakusanya na kusambaza mabilioni yaliyotumika katika kuhonga wajumbe ili kununua kura za kumbeba jamaa ili aingie IKULU.
 
Huyu ndiye aliyekuwa mweka hazina wa kamati ya mtandao wakati wa kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa CCM yeye ndiye alikuwa anakusanya na kusambaza mabilioni yaliyotumika katika kuhonga wajumbe ili kununua kura za kumbeba jamaa ili aingie IKULU.
No no no no no hapana huyu bwana hajapata kuwa mweka hazina wa mtandao hata siku moja ila ni rafiki mkubwa wa tangu utotoni wa muungwana.
 
Huyu ndiye mfadhili mkuu wa biashara za JK....anasimamia ujenzi wa kijiji chake huko Msoga hill ......ni mtu wake saaaanaa.
 
Duuh! Mchuchuma ya toka enzi zile inatua kwa mtu mmoja kimtindo. Tutaona yote mwaka huu
 
Halafu watanzania wengine wanasema Mengi alichemsha...hii ni "serious game"..so don't hate the player..
 
Hawa jamaa inaonekana hawana pa kuchomokea na ni wagumu kweli wa kuelewa Mengi alishasema kuwa kama wanaona kuwa wamesingiziwa basi waende mahakamani na sio kumwomba Mengi awaombe msamaha na lazima wawe wanaogopa kwenda mahakamani kwani kufungo nje nje kwani kibao kitawageukia tu.
 
hawa jamaa inaonekana hawana pa kuchomokea na ni wagumu kweli wa kuelewa Mengi alishasema kuwa kama wanaona kuwa wamesingiziwa basi waende mahakamani na sio kumwomba Mengi awaombe msamaha
na lazima wawe wanaogopa kwenda mahakamani kwani kufungo njenje kwani kibao kitawageukia tu


Vitisho vya kwenda mahakamani mbona tulishavizoea? Ingekuwa kutishia kwenda mahakamani ndio kwenda Dr. Slaa alivyo wasanula Mwembeyanga angeishaozea Keko! But waaaapi bwana? Yupo anapeta na kuendeleza libeneke kama kawa.

Kwahiyo hata kwa Mengi watatisha weee... tunataka waende waache makelele na waende.
 
Subash... ndio aliemjengea JK hekalu la pale Bagamoyo... ni mshikaji wake walisoma wote primary...
 
Subhash Patel nadhani si sahihi awe kwenye chungu cha mapapa. Namfahamu huyu bwana kwa miaka mingi kama mhangaikaji/mjasiriamali asiyecheza faulo.
 
Mengi ameisha, atawajua kama ni mabohora au ni mabaniani afu wacheni kumtomeza Mengi na kumshangilia, sasa joto analiona peke yake hata CCM wamemtenga.
 
Mzee Mengi anazungumza kwa 'metaphor' amewataja mafisadi papa ambao ni dam dam na JK, kwa lugha nyingine Mengi amemtaja JK kama mlinzi wa mafisadi papa, aminini msiamini, this time kibao kinamgeukia Mengi, lets wait and see.
Japo Mengi ni Mafia, mapapa ni mamafia na JK nyuma yao!.
 
Subash... ndio aliemjengea JK hekalu la pale bagamoyo... ni mshkaji wake walisoma wote primary...

Subhash ni family friend wa Salma na Mrisho.

JEETU%2BPATEL.jpg
 
Mie hasira zinanipanda sana kuona hawa mafisadi papa wa kiasia wanakoroma ndani ya nchi yetu....yaaani..wee acha tu....Hawa jamaa hata Idd Amini aliona kwamba wanadhoofisha uchumi wa nchi yake na kuamua kuwafukuzia mbali....tatizo lao wakichuma nchini kwa ufisadi ..wanahamishia mali zao nje ya nchi...wala nchi haifaidiki na mali zao.....wananiudhi......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom