Mlengo wa Kati
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 2,730
- 492
Hapo kwenye red; eti malumbano ya muda mrefu! Hivi wamefafanua ni malumbano baina ya nani na nani au pande zipi? Najua hakuna (serikalini au CCM) atakayethubutu kufafanua au wakifanya hivyo lazima wapindishe maneno.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni; CHADEMA itabaki katika historia kama miongoni mwa taasisi zilichochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko chanya ya kisiasa na kijamii katika taifa letu. Hivi taasisi kama CHADEMA zisingekuwepo sijui hii nchi ingekuwaje; nadhani CCM wangekuwa wametufanya kitu mbaya kupita maelezo!
Chadema haina sura ya Taasisi bado ni kampuni ya kifamilia(familia ya Mtei na Mwenyekiti wa Chadema Taifa kaoa mtoto wa Mzee Mtei). Ebu tafuta neno jingine badala ya Taasisi!