Hatimaye serikali yakubali marekebisho ya muswada wa katiba mpya...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1
 
bado wametekaenya sehemu ndogo sana,mamlaka ya kifalme hayaja guswa kwa nini?
 
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1
Hapo kwenye red; eti malumbano ya muda mrefu! Hivi wamefafanua ni malumbano baina ya nani na nani au pande zipi? Najua hakuna (serikalini au CCM) atakayethubutu kufafanua au wakifanya hivyo lazima wapindishe maneno.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni; CHADEMA itabaki katika historia kama miongoni mwa taasisi zilichochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko chanya ya kisiasa na kijamii katika taifa letu. Hivi taasisi kama CHADEMA zisingekuwepo sijui hii nchi ingekuwaje; nadhani CCM wangekuwa wametufanya kitu mbaya kupita maelezo!
 
Mwisho wa siku watalainika tuu. Maana huwezi ukaamua kuongoza nchi kichwa kichwa! Lazima mawazo ya watu yaheshimiwe!
 
kwa hiyo hayo ndio yalikuwa makubaliano ya Rais na CDM? Haya tusonge mbele
 
Thanks to Chadema, lakini bado tunahitaji marekebisho mengi kama ya kumpunguzia rais madaraka na kulipa Bunge kuwa na nguvu kuliko Rais.
 
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1

Hapo kwenye red hicho ni kipengere kati ya vipengere 72 vinavyotakiwa kurekebishwa. Hongera cdm kwa kufanikisha muswada kurudi bungeni.
 
sasa huo si utakuwa wendawazimu wa hao wabunge waliopitisha chenga kwenye chujio?
 
Mswada upi tena? kama kurekebishwa inarekebishwa sheria, mswada ulisha sainiwa na kuwa sheria.

Marekebisho ya sheria hayazuwii sheria hiyo kutumika kama ilivyyo, mpaka hapo marekebisho yatapokwisha fanyika bungeni na kupelekewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuyasaini hayo marekebisho. Ni vitu vya kawaida kabisa na ndiyo kazi za bunge, hakuna jipya wala cha ajabu hapo.
FF tuelimishe manake watu hatujui tofauti kati ya mswada na sheria! We are great thinkers!
 
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,hii yote ni matunda ya cdm chini ya makamanda makini kama Lisu na bado.Peeeeeeeoooooopleeeees!Poweeeeeeeeer
 
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1

Usanii 100%, wanaruhusu kufanya mikutano lakini kifungu cha adhabu bado kipo. Kama nia ni kuondoa criminal element kwenye hiyo sheria ingekuwa busara na adhabu iondoke.

Hakuna cha kuchekelea hapo.
 
Baada ya malumbano ya muda mrefu hatimaye serikali imekubali marekebisho ya mswada wa katiba..hasa kifungu cha kuwaruhusu wanaharakati na vyama vya siasa kuweka mikutano na wanachama wake ili kujadili namna ya kushiriki kwenye mswada huu.Marekebisho haya yatapelekwa kwenye kikao kijacho cha bunge.

Source:TBC 1

Mkuu, si ungeyataja baadhi ya hayo marekebisho ya muswada wa katiba mpya tuyajue!

Na kile alichosaini Rais ni nini?
 
Back
Top Bottom