Hatimaye serikali yakubali marekebisho ya muswada wa katiba mpya...

Sasa mibunge ya CCM ilivyokuwa inashabikia ule muswada!!!!!!!!

Mibongolala yote pamoja na kuwadi wao Werema! hamna kitu kabisa!
Sasa watawaambiaje wananchi juu ya matusi waliyowatukana wanachadema?......na bado marekebisho mengi yanahitajika kama namna bora ya kuunda bunge la katiba..na mambo mengi tu!
 
Mkuu nadhani mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na waziri wa sheria wanatakiwa wakinywee kikombe hiki! Inakuwaje wamshauri Rais na Amiri Jeshi wa Majeshi yenye silaha asaini muswada kuwa sheria na sheria hiyo kurudi bungeni kwa ajili ya marekebisho hat kabla haijatumika!? Nadhani watachukua hatua za kujitakasa kwa kuachia nafasi zao. Kumekuwa na shida nyingi huko kwenye sheria.

mkuu kimbunga
kuna jamaa aliwahi kunambia kuna sheria za wanasihasa na sheria za walalahoi, sijaelewa alikuwa anamaanisha nini, sitaki hata kujisumbua kujua tena, loh! hii kweli nchi ya kusadikika. hapo kwenye bold tusahau kabisa hiyo kitu, tena futa kauli yako wasije wakakusikia, teh teh teh teh!
 
mi naipongeza serikali kwa maamuzi hao angalau,ila si wanasiasa tu,iruhusu mikusanyako ya wananchi wenyewe bila wanasiasa na iratibiwe na wananchi wenyewe
 
Hahahaaa, mambo yameshaanza sasa. Mabua na Mahindi kuonekana hivi karibuni.

Huyu Lady na mtani wangu FF, naomba sasa tuanze Kumhurumia maana atataka ku-prove kuwa Black is White.

Ha ha ha ha ha! Obvious need no proof brother. Ni chizi tu atakayepoteza muda wake ku-prove Jua linatokeaga mashariki tena muda wa asubuhi!

I wish Regia were here! R.I.P my sister.
 
Sheria ilikuwepo lakini ukweli ni kwamba ilikuwa haijaanza kutumika. Sheria hiyo haijaanza kutumika kwa kuwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya haujaanza rasmi. Ndio maana kulikuwa na mikutano mingi tu ya hadhara ambayo ilikuwa inahamasisha wananchi huko mikoani ili waielewa sheria hiyo na hakuna aliyeshikwa wala kufunguliwa mashitaka. Mkoani Mara [Mh. Wassira na Mh. Mkono] waliambiwa kwamba walikuwa wanavunja sheria kwa kufanya mikutano hiyo.

Ni aibu kwa Rais kusaini mswada wa sheria halafu hata kabla haijaanza kutumika inarejeshwa bungeni kwenda kufanyiwa marekebisho, yawe ni marekebisho madogo au makubwa, bado huo ni upungufu na ndio maana Tanzania huwa tunaingizwa mikenge kwenye mikataba mingi sana ambayo serikali ina saini ama kwa kutosikiliza wataalam wanasemaje au kwa kutanguliza maslahi ya binafsi au kikundi/chama cha siasa.

CHADEMA walipotoka nje ya Bunge kususia mjadala, kila mtu aliwabeza kuanzia Spika mpaka wabunge wa mipasho. Bahati nzuri leo tumeona matunda ya kususa mjadala kwamba finally Rais ameona kwamba hoja zao zina mantiki. Uzuri mwingine ni kwamba JK alishaona hali ni tete na ndio maana wabunge wa CCM waliondoka kimya kwenda majimboni eti wanakwenda kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi pindi mchakato utakapoanza. Ukweli ni kwamba walienda kupima kina cha maji. TV zimeharibu sana ulaji wa CCM kwa kuwa wananchi wanaona na kusikia kila kinachoendelea bungeni na uzuri mwingine ni kwamba wananchi wanapima hoja za wabunge na kuona zipi zina mashiko na zipi ni mipasho.

Ni aibu kwa wabunge wote waliounga mkono mswada ule na kuongeza vipengele vya kijinga kabisa ili kuwakomoa wale wanaoonekana kupinga mchakato huo. Ninasubiri kwa shauku kubwa kuona hao wabunge kama watapinga hayo marekebisho yatakayopelekwa bungeni.

Bottom line ni kwamba hakukuwa na sababu yoyote ya Rais kusaini mswada huo kuwa sheria halafu wakati huo huo Ikulu inatangaza kwamba wananchi, vikundi, NGOs, vyama vya siasa na viongozi wa dini wanakaribishwa kupeleka maoni ya kurekebisha sheria. Sasa kama sheria ilikuwa ina mapungufu kiasi kwamba Ikulu inakaribisha maoni ya kuirekebisha, kwanini wananchi watangaziwe kupeleka maoni yao muda mfupi baada ya kusaini sheria hiyo?

Ni wakati muafaka kwa wabunge wa CCM kutafakari kwa kina kama wanatutendea haki wananchi kwa kuwa Rais na Mwenyekiti wa Chama chao amewaonyesha kwamba wao ni mazuzu ambao huwa wanapitisha kila kitu hata kama ni uozo. Mwaka 2015 siyo mbali sana watahukumiwa na wapiga kura wao na huenda Tume ya Uchaguzi itakuwa huru na itakuwa inatumia sheria ambayo inatawaliwa na uwazi zaidi na kwamba vyombo vya dola havitakuwa vinapendelea chama tawala.
 
Nikufahamishe nini zaidi, soma vizuri post yangu ipo crystal clear.

Mswada ulisha sainiwa kuwa sheria kwa hiyo chochote kitachofanyika kwenye sheria hiyo inakuwa ni marekebisho (amendment) ya sheria.
Naona hapa FF umelipata Li-Boko halali lenzako. Unalipeleka unavyotaka Li-Maamuma lako mwe!
 
Hivi rais haoni aibu kila anaposaini muswada na kabla ya muswada kuanza kazi unarudi bungeni!

sasa huo si utakuwa wendawazimu wa hao wabunge waliopitisha chenga kwenye chujio?
Green: Alisema anasaini kuwaridhisha wabunge wa chama fulani hivi, jamani mwacheni.

Yellow: Sijui watakaa kimya wakati wa kujadili marekebisho haya? maana waliupitisha pasipo na shaka wakati ule, kuwa ulikuwa sahihi.
 
Sheria haina muda wa kurekebishwa, kuwa sasa umewahi sasa umechelewa.

Nani aliokwambia sheria haijaanza kutumika? sheria ikisha sainiwa ujuwe unaitumia tayari, ulitaka itumike vipi? Unanchekesha!
JK , waziri wa katoba na sheria pamoja na mwanasheria mkuu ndo wanatuchekesha sana sisi raia, wabunge wakiongozwa na waziri mkuu pamoja na spika wao wanatushangaza na kutustaajabisha sisi wapiga kura wao kwakuwapelekea kina JK huo muswada wa kutukandamiza sisi, loh!
 
Mswada upi tena? kama kurekebishwa inarekebishwa sheria, mswada ulisha sainiwa na kuwa sheria.

Marekebisho ya sheria hayazuwii sheria hiyo kutumika kama ilivyyo, mpaka hapo marekebisho yatapokwisha fanyika bungeni na kupelekewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuyasaini hayo marekebisho. Ni vitu vya kawaida kabisa na ndiyo kazi za bunge, hakuna jipya wala cha ajabu hapo.

kwa mtu mwenye akili ya kawaida, hilo la marekebisho kwake ataona ni jambo dogo sana. Lakini hii ni mara ya pili mswaada unasainiwa kuwa sheria halafu hata miezi mitatu haijapita unarudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho. Wenye akili timamu wanajiuliza inakuwaje hilo litokee ndani ya muda mfupi hivyo? Ililitokea kwenye sheria ya uchaguzi na sasa limejirudia tena kwa mtawala yule yule...........hiyo inamaanisha nini kwa mhusika anayezipitisha kuwa sheria. Anatumia akii yake kufanya judgement au laa? Hiii inaashiria nini juu ya upeo wake wa kusikiliza na kufanya maamuzi? Kuna mengi sana ya kujiuliza ktk utendaji wa ofisi husika
 
mkuu kimbunga
kuna jamaa aliwahi kunambia kuna sheria za wanasihasa na sheria za walalahoi, sijaelewa alikuwa anamaanisha nini, sitaki hata kujisumbua kujua tena, loh! hii kweli nchi ya kusadikika. hapo kwenye bold tusahau kabisa hiyo kitu, tena futa kauli yako wasije wakakusikia, teh teh teh teh!
Mkuu hii kitu si masikhara kama inarudi bungeni isomwe na waziri wa sheria ambaye aliisoma kama muswada na ukapitishwa. kisha wabunge wachangie; huenda wabunge walioipitisha wakataa kurekebisha. Lakini kurudishwa bungeni ni mzigo kwa hao jamaa wawili. Pia wabunge ambao waliunga mkono asilimia mia moja! Kesho natafuta hansard nisome michango ilikuwaje ili niwabaini wabunge ambao waliunga mkono.asilimia mia moja.
 
Mswada upi tena? kama kurekebishwa inarekebishwa sheria, mswada ulisha sainiwa na kuwa sheria.

Marekebisho ya sheria hayazuwii sheria hiyo kutumika kama ilivyyo, mpaka hapo marekebisho yatapokwisha fanyika bungeni na kupelekewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuyasaini hayo marekebisho. Ni vitu vya kawaida kabisa na ndiyo kazi za bunge, hakuna jipya wala cha ajabu hapo.

ww mama lazima uharishe pumba hata sijui una matatizo gani?

Unakejeli hatua iliyofikiwa unadhani haya mabadiliko yamekuja hivi hivi tu. Kama si harakati za chadema nyie magamba si mngetuletea katiba ya ccm.

Hebu kuwa na akili japo kidogo!una mawazo ya kichawi chawi tu saa zote.
 
Ha ha ha ha ha! Obvious need no proof brother. Ni chizi tu atakayepoteza muda wake ku-prove Jua linatokeaga mashariki tena muda wa asubuhi!

I wish Regia were here! R.I.P my sister.

dah! mkuu hapa ndo umeharibu kbsa hii post, unajua ndo aliyeanzisha wazo la kwenda kumuona JK, aisee...
 
Nikufahamishe nini zaidi, soma vizuri post yangu ipo crystal clear.

Mswada ulisha sainiwa kuwa sheria kwa hiyo chochote kitachofanyika kwenye sheria hiyo inakuwa ni marekebisho (amendment) ya sheria.
Aaah mkuu hiyo najua. Nilikuwa nakupongeza kwa kuelimisha the so called great thinkers ambao hawawezi kutofautisha kati ya mswada (bill) na sheria (act). Pamoja na hayo vipi hii sheria haikuwa na sehemu ya waziri kutengeneza kanuni (regulations)? kama ilikuwepo je kanuni zilishatengenezwa? Je hii sheria ilishakuwa gazetted?
 
Hahahaaa, mambo yameshaanza sasa. Mabua na Mahindi kuonekana hivi karibuni.

Huyu Lady na mtani wangu FF, naomba sasa tuanze Kumhurumia maana atataka ku-prove kuwa Black is White.

Hakuna tofauti na maalim seif kupewa makamu wa kwanza..

naona mmefurahi sana waambie na wanachama wenzako wawe na adabu na rais ndio watafanikiwa lakini sio kususa ok..
 
Mkuu hii kitu si masikhara kama inarudi bungeni isomwe na waziri wa sheria ambaye aliisoma kama muswada na ukapitishwa. kisha wabunge wachangie; huenda wabunge walioipitisha wakataa kurekebisha. Lakini kurudishwa bungeni ni mzigo kwa hao jamaa wawili. Pia wabunge ambao waliunga mkono asilimia mia moja! Kesho natafuta hansard nisome michango ilikuwaje ili niwabaini wabunge ambao waliunga mkono.asilimia mia moja.
nahisi atamtuma naibu wake, sidhani km atasimama tena,
 
Back
Top Bottom