Hatimaye RunX imeingia Mwanza

Hatimaye RunX imeingia Mwanza

Hongera na pole kwa changamoto ya taa za LED. Ushauri wangu ni ukipigwa taa kali usiziangalie badala yake angalia kati kati ya kioo chako.

Ikibidi punguza na mwendo ili uweze kubaki kwenye lane yako. Ukiziangalia hizo taa lazima utazifuata, kwasababu gari linaenda pale unapoangalia wewe.

Ila pia wasiliana na dereva mwenzako, ukiwa bado mbali kidogo mpigie flash light mbili atapunguza taa zake. Asipopunguza ndio ufanye niliyokuambia hapo juu
 
Atapitia kigoma vp akuletee na mawese na watoto wa kiha mwenye nyashi za kibantu
 
Pole kwa changamoto. Kuna miwani alikuwa anauza MR TOYOTA na member mmoja humu ni kwa ajili ya night vision ukiwa barabarani. sijui kama bado anazo mtafute.
 
Unalalamika mataa makali halafu unataka uyaweke na wewe , akili ya maharage
Ndiyo upeo wa juu wa kufikiri wa Mtanzania huo. Ni kulipizana. Ili na yeye awe anawamulika mpaka wahame njia 😂😂😂
 
Mtoa mada nakushauri Tu hata ufunge taa za namna gani bado usiku utapata shida Tu..... jitahid utembee mchana Tu Mimi nimefanya safari nyingi Sana za usiku Ila nimeacha kitambo sanaa na hizo mambo.

Mara nyingi safari za kutoka mwanzo kuja DAR naanza SAA 10 usiku ili asubuhi inikute nzega
Na ile njia inahitaji umakini sana!
 
Kama umefika leo jitahd utembelee delux, villar park, las vegas kona ya bwiru.. Hutajuta kuwa mwanza!
Huyu ni mshua anatembelea maeneo tulivu. Huyu wa kwenda Malaika beaches, Midlands, Hadjens rooftop, Tilapia sehemu kama hizi ambapo unakutana na CEOs, CFOs, MDs n.k
 
Baa
Dah hii kitu ilifanya niache kabisa safari za usiku. Madereva ma bus wakikupiga hiyo mbele huoni kitu. Ila pongezi za dhati kabisa ziende kwa madereva ma lorry hao jamaa wakikuona tu unakuja wanapunguza taa vizuri tu ila kama utakomaa na mitaa yako watakumulika kiasi kwamba watahakikisha wanaona mpaka ndani mpo wangapi
Balaa Sana
 
Huyu ni mshua anatembelea maeneo tulivu. Huyu wa kwenda Malaika beaches, Midlands, Hadjens rooftop, Tilapia sehemu kama hizi ambapo unakutana na CEOs, CFOs, MDs n.k
Hahahaa ayseee jana nilikuwa Tunza beach chimbo langu la muda wote ni hapo...
 
Safi sana mkuu. Sema umetubania baadhi ya vitu:
1. Mafuta.
2. Wastani wa speed.
3. Vituo vingapi.
Okay
1. Mafuta nimepiga 230K
2. Speed wastan 110Km/h
3. Vituo nimesimama kusalimia wanangu dom,Singida na igunga basi
 
Dah hii kitu ilifanya niache kabisa safari za usiku. Madereva ma bus wakikupiga hiyo mbele huoni kitu. Ila pongezi za dhati kabisa ziende kwa madereva ma lorry hao jamaa wakikuona tu unakuja wanapunguza taa vizuri tu ila kama utakomaa na mitaa yako watakumulika kiasi kwamba watahakikisha wanaona mpaka ndani mpo wangapi
Ayseee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom