Hatimaye Nicole Joy Berry apata dhamana

Hatimaye Nicole Joy Berry apata dhamana

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,446
Reaction score
6,698
Anaandika mwanadada Nicole Joy Berry kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Habari, Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote wenye Nia njema nami. Naomba sana Taarifa za MICHANGO YA FEDHA kwa Nia ya kunisaidia kivyovyote ZIPUUZWE!

Mimi nina ndugu, marafiki na watu wa karibu ambao hawashindwi kufanya "JAMBO" Lakini ilibidi taratibu zote zifuatwe! Mtu yeyote Asidanganye uma kuwa Nahitaji michango, kila kitu kipo Sawa na Niko salama Nang'aa kuliko zamani, kuku na makange ya Jela yameninawirisha!

Sio sahihi mtu yeyote kuweka mdomo na pua yake kwenye kesi inayoendelea mahakamani, waliopokea pesa wanazidi kurudisha na Haki yangu nimepatiwa!

Nawasihi sana SIHITAJI MICHANGO YEYOTE KUTOKA KWA MTU YEYOTE. KIONJO!!! Yamkini kuna mtu yeyote alinisolola kwa njia yeyote ile, kuanzia wasanii wanafki, marafiki feki na wanaonigeza sauti na kenge WOOOOTE! NAKUAHIDINI nitakurudia si punde.

Naomba muda nishushie ujelajela na kimoeti cha baridi kwanza

nicole.png
 
Kama sio nyumba ndogo ya mtuu kwa sasa
 
Huyu nae atulie kimya, ko sponsa kumtolea dhamana ndo abwate hivyo?
Muhimu tumejua uhalisia wake, na hatusikii tena porojo zake za kujiona ana pesa, kumbe TAPELI.

Ila lokole nae sijui hajaenda shule, uandishi wake mbovu na hayo maandishi makubwa km anafoka, anaboa tyuuh.

Vidampaa muendage shule, mxxxiiiieeew.
 
Back
Top Bottom