Unaona wife wako kama umemuonea kumpuga kwa uzinzi, hata mimi ninakiri umemuonea.
Ndiyo maana umemuacha kishingo upande huku unajilaumu, roho inakusuta.
Ujue wengi wanaingia kwenye ndoa kwa madhumuni zaidi ya upendo ama ngono pekee.
Manufaa ya ndoa ni pamoja na kusaidiana mambo makubwa na madogo ya kimaisha, kupanuana akili na kushauriana, pamoja na kulindana nk nk.
Sasa mmoja wenu akikengeuka jambo flani mojawapo katika muunganiko wenu, yakupasa kurudi nyuma na kukaa naye chini kurekebisha dosari hiyo.
Mke ama mume haachwi kwa kosa moja, kama niivyo pasingekuwepo na ndoa za watu hadi kuzeeshana sasa!
Tayari hapo ulishauvaa uhakimu, umemuhukumu mwenzako saazingine kwa makosa yale yale unayopenda wewe kuyafanya.
Fikiria mara mbilimbili mrudie mkeo, kwa misukusuko ulompatia bila shaka atajirekebisha.