Leo hii katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni yule mnyange wetu aliyekuwa rumande toka ijumaa hatimaye amepandishwa tena kizimbani na kupewa dhamana.,hii ni baada ya juhudi za toka jana za 'uncle' Hashim Lundenga.,kimwana sasa yupo uraiani..
hawa wasichana duh, kila mwaka wakitawazwa kuwa ma miss wetu lazima tusikie jambo tena linalohusiana na matendo ya aibu kwa jamii .... eti wawakilishi wetu looo.... ugomvi na ma - mabwana tu hakuna kingine wanaweza kufanya....yale yale ya kina wema sepetu.
Lundenga kazi unayo mzee....
jamani vipi kuhusu mpenzi wake naye katolewa dhamana na Hashimu Lundenga
kazi anayo kweli kweli mjomba L.
nashangaa ameshindwa vipi kutimiza utaratibu amabo waliuwekwa kuwa mis akimisbehave watamnyang'anya zawadi na kumvua taji (sijui misbehaving to wat degree )
Hizo ni siasa za uncle L, si unajua yeye ni dalali tu wa hawa warembo!!
Inaonyesha waamuzi wa Miss Tanzania 2009 kuna kitu wali-miss! Ni aibu kuwa na kina Miss kama hawa ambao wana act just on impluse badala ya vichwa vyao!!
mmmh!!!
haya hao wenyewe wako wapi na wanchukua hatua gani kurekebisha haya mapungufu basi!!!
hii kitu haina hata maana tena
hivi baada ya mashindano nothing happens eeh
they are just left kama makuku ya kienyeji yajiendee kuchakura yanapotaka
no gidence nothing
tusije tukakalia kulaumu hawa mabinti jamani, kwa umri wao mi naona bado wanahitaji sm kind of muongozo basi angalau. umaarufu wa kuja ghafla tena ktk umri huu nao ni tatizo
Kabisa, kwa nchi zinazojali pulic image ya brand yao 'Vodacom Miss Tanzania', sasa hivi hawa jamaa wangekuwa wanahangaika sana kupata wadhamini....katika hali ya kawaida huwezi peleka pesa yako kwenye shindano kama hili lililochafuliwa na washindi karibu wote isipokuwa yule miss tanzania mwenye asili ya kihindi...na pengine Lundenga angelazimika kubadili hata jina la mashindano yake, mfumo mzima wa uandaaji na vigezo vya kupata washindi ili kuleta heshima ya shindano lenyewe na washiriki kwa ujumla.