Mwenyekiti wa chadema ameshaachiwa na sasa watu wamembeba juu juu Arusha
Nakubaliana na wewe Mkuu, CCM hawasomi alama za nyakati, wanatumia vyombo vya dola wakidhani wanammaliza kisiasa CDM kumbe wanapandisha chati........Peoples'........!!!Nilianza kumsikia kwa mbali alipochaguliwa kuwa mbunge Hai mwaka 2000
Alipata umaarufu zaidi alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA (2004?)
Alipata umaarufu sana alipogombea uraisi mwaka 2005, zaidi kwa kuanzisha styles za helkopta na magwanda, ambazo ni maarufu hadi leo
Alikuja kuvuma tena sana wakati wa operesheni sangara.
Katika uchaguzi uliopita, hakuvuma sana (kwa sababu ya kuwepo Slaa katika uraisi?)
Alikuja kuvuma zaidi wakati wa kuundwa kwa kambi ya upinzani
Aliendelea kuwa midomoni mwa watanzania katika matukio tofauti kwa kiwango tofauti hadi Ijumaa tarehe 3 June 2011
Kwa siku tatu mfululizo Kuanzia Ijumaa jioni, hadi leo asubuhi, Freeman Aikaeli Mbowe amengeza mstari mwingine katika historia yake ya kupigania wanyonge Tanzania. Mstari ambao kwa wanaofuatilia vyombo vya habari na kusikiliza maoni ya watu ya kisiasa, bila shaka unastahili kuandikwa bolded zaidi, na kwa font kubwa zaidi, angalau kuliko mistari yote iliyowahi kuandikwa siku ya nyuma...
waswahili tunasema utabaki na labda. CDM kuiona ikulu bado ni ndogo ya zuzu.
Wanadanganywa, wanadanganyika. ndio maana mara mgogoro uvccm na imara wanatumiwa na cdm kuvuruga amani.
kwani kabila kubwa la wakazi wa Arusha ni wafugaji.
wanaongoza nchi kwa mazoea ya siasa za chama kimoja, sasa ndiyo matokeo yake haya - kujichanganya changanya kwa mihimili hii mitatu.
sasa hivi chadema ina support kubwa ya wananchi - na hii kamata kamata ndiyo inawamaliza CCM kabisa - "killing themselves softly"
Asiyejua kwamba Watanzania walio wengi wameichoka CCM ndio yuko kwenye usingizi wa pono. Suala ni je CCM wataweza kuiba hela za umma kuwawezesha kuchakachua tena 2015 na je CDM wataweza kujipanga kulinda kura zao? Na jinsi mambo yanavyoenda CDM wako na advantage.
Dola inayotamka Bungeni (through PM) kuwa mafisadi wakiguswa nchi itasambaratika? hiyo sio dola hata kidogo ila kundi la matapeli.Yapo kila Wilaya , na maji yake yanawasha balaa, ukimwagiwa yale maji hakuna la zaidi ya kukimbia tu. Na sio maji tu, jamaa wana silaha za kijeshi pia full masinonda kwa lolote. Hiyo ndio dola sasa
wakimaliza miaka mitano watakuwa hawana tena hamu ya kuongoza tz, sasa hivi wanaona aibu kuachia ila moyoni wanatamani sana kuachia ngazi
wee unapimaje umaarufu,mbona alikua rumande sasa amepiganiaje hiyo haki,na kama ni hivyo kuwekwa rumande ndio umaarufu basi mch. mtikila ndie jembe zaidi kuliko yoyote tanzani.
Duh, wewe kweli hujui ku analyse mambo, hiyo ni kinyume chake sasa ! Jamaa wamemdhalilisha sana na hata wabunge wenyewe wamesema. N aelewa kuwa suala la bajeti ni suala la bunge sio la mbowe, sasa hapo pipoz powa inahusika vp?. Jamaa wamemkamata kama ndege, wameenda kumlaza sakafuni, wamemsafirisha usiku hakupata usingizi huoni heshima imepungua?. Na isitoshe hili ni suala la kisheria wala CCM haihusiki hata chembe, wenzake wao walienda mahakamani wakamdanganya mwenzao amedhalilika sana .
wee unapimaje umaarufu,mbona alikua rumande sasa amepiganiaje hiyo haki,na kama ni hivyo kuwekwa rumande ndio umaarufu basi mch. mtikila ndie jembe zaidi kuliko yoyote tanzani.
waswahili tunasema utabaki na labda. CDM kuiona ikulu bado ni ndogo ya zuzu.