HATIMAYE: Mazda CX-5 imeingia Top 5 ya gari zinazoingizwa Tanzania kutoka Japan

Wakuu.

Mapenzi ya Watanzania kwa SUV pendwa Mazda CX-5 yanazidi kujionesha kwa Mtandao maarufu wa kuingiza Magari kutoka Japan kuiweka katika magari 10 yanayoingizwa sana Tanzania na kushika namba 4.
View attachment 2930349
Bado Subaru Forester, tako la Nyani na IST wako mbele yake ila inaonesha jinsi gari mwaka 2024 na 2025 inaweka kua ni mwaka mzuri kwa Mazda kujazana Tanzania.

Huyu Mazda CX-5 mwenyewe ni diesel SkyActive cc 2,200 SUV anaenda kama CIF $5,000 na kuendelea. TRA utacheki mwenyewe kwa kuangalia mwaka.

Hii ni fursa nzuri kwa mafundi wa magari kuanza kujiandaa kupambana na engine ya diesel ya uyu mjamaa, pia waingiza vipuri na wazee wa decorations wachangamkie fursa.

Mazda ata perfom vizuri zaidi akisaidiwa na Mazda Verisa, Mazda 2 (demio), Mazda 3 (Axela) na Mazda 6 (Atenza) na mdogo wake CX5 bwana CX3.
Hiyo list imetolewa na mamlaka gani?
 
Mwanangu nipo nae kariakoo anauza foresta yake ili avute hiyo mashine. Hii gari hata Mimi nimetokea kuipenda Sana

Ukiona mpaka foresta imeshika namba moja Tanzania ujue Hali imebadilika hasa Kwa wanazi wa Toyota, huwa nashangaa watu wa hapa jamiiforum wakiponda gari za kijerumani lkn ukiingia barabarani zimejaa kibao watu wanasukuma Tu....uwoga ni kitu kibaya sana maishani
Wewe utakuwa unaota na mahaba ya ushamba wa magari ya kijerumani. Mbona hakuna hata gari moja ya mjerumani hapo kwenye top 10?
 
Back
Top Bottom