Hatimaye Mahakama Kuu yaamuru DOWANS walipwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Mahakama Kuu yaamuru DOWANS walipwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 7, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Pamoja na kelele zetu zote, hatimaye mahakama kuu imesema Dowans lazima walipwe;

  James Magai

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutaka isitishe utekelezaji wa malipo ya Sh96 bilioni kwa Kampuni ya Kufua Umeme ya Dowans kutokana na kuvunja mkataba wa kibiashara kinyume na sheria.

  Kufuatia uamuzi huo, Tanesco sasa inatakiwa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha ambacho kwa ujumla kinaliongezea shirika hilo mzigo wa madeni.

  Tanesco kupitia mawakili wake Rex Attorneys iliwasilisha mahakamani hapo maombi mawili; kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama hiyo iliyotolewa Septemba 28, 2011 na kuomba kusimamishwa kwa utekelezwaji wa hukumu hiyo.

  Katika hukumu ya awali iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, mahakama hiyo ilikubali maombi ya Tuzo kwa Dowans iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), Novemba 15, 2010.

  ICC iliamuru Tanesco kuilipa Dowans fidia ya Dola za Marekani 65,812,630.03, kutokana na kuvunja mkataba wa kibiashara kinyume cha sheria. Mahakama Kuu Tanzania ilikubaliana na tuzo hiyo na kuipa kampuni hiyo nguvu ya kisheria.

  Hata hivyo, Tanesco haikuridhika na hukumu hiyo, badala yake ikawasilisha mahakamani hapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa kuipinga.

  Jana, kwa mara nyingine mahakama hiyo iliendelea kubariki Dowans kupewa tuzo hiyo na kutupilia mbali maombi ya Tanesco, ikiwamo pingamizi la utekelezaji wake.

  Katika uamuzi wake aliousoma jana asubuhi, Jaji Dk Fauz Twaib alikubaliana na hoja za Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama kwamba mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusimamisha utekelezaji wa malipo hayo baada ya hukumu ya ICC.

  Awali, wakili Fungamtama katika hoja zake, alidai kuwa maombi hayo yamefunguliwa chini ya Kanuni ya 11 (2) na ya 47 ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania ya mwaka 2009.

  Alidai kuwa kanuni hiyo ya 47 inatumika kwa maombi ambayo Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu nchini zina mamlaka ya kisheria lakini, katika maombi hayo ya Tanesco kusimamisha utekelezaji wa malipo hayo, mahakama kuu haina mamlaka hayo.

  Lakini, Jaji Dk Twaib alikubaliana na hoja za wakili Fungamtama kwamba kifungu cha kanuni ambacho Tanesco ilikitumia katika maombi hayo, hakiipi mamlaka Mahakama Kuu kusimamisha utekelezaji wa hukumu zake.

  Jaji Dk Twaib alisema kuwa, namna na masharti ya kusimamisha utekelezaji wa hukumu yalivyoainishwa katika kifungu (d) cha kanuni hizo za Mahakama ya Rufani.

  Alisema kama Wakili Fungamtama alivyoeleza kwa usahihi, kanuni hizo zinaihusu Mahakama ya Rufaa tu kama ilivyoainishwa vizuri katika Kanuni ya 3 ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa za mwaka 2009.

  “Mheshimiwa Jaji Mkuu anatambua msimamo wa kisheria uliowekwa katika maamuzi mbalimbali kwa misingi kwamba, mchakato wa rufaa unapokuwa umeanza kwa kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa, mahakama hii inakoma kuwa na mamlaka ya kusimamisha utekelezaji wa hukumu,”, alisema Jaji.

  Jaji Dk Twaib alisema mahakama hiyo inaweza kuwa na mamlaka hayo kabla kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

  “Mara tu taarifa ya kusudio la kukata rufaa inapokuwa imewasilishwa (kama ilivyo katika kesi hii), Mahakama Kuu inakoma kuwa mamlaka,” alisisitiza Jaji Dk Twaib na kuongeza:

  “Kwa misingi iliyoelezwa mahakama hii haina mamlaka ya kisheria kushughulikia maombi ya kusimamisha utekelezaji yaliyowasilishwa na muombaji (Tanesco)”, alihitimisha uamuzi wake Jaji Dk. Twaib.

  Sakata lenyewe Mwaka juzi jopo la majaji watatu wa ICC lilitoa uamuzi wa kuitaka Tanesco kuilipa Dowans Tuzo ya Sh96 bilioni, kutokana na madai ya kuvunja mkataba wa kibiashara kinyume cha sharia.

  Hata hivyo, uamuzi huo umekuwa ukipingwa na baadhi ya watu wakisema Dowans ilirithi mkataba haramu wa Richmond hivyo, mkataba huo haukuwa halali.

  Tanesco nayo kwa upande wake, katika maombi yake ilidai kuwa kama mchakato wa utekelezaji wa hukumu hiyo utaendelea, itaathiri uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza umeme nchini na hivyo kusababisha tatizo kubwa la ukosefu wa umeme nchini na hivyo kuathiri uchumi wa nchi kwa jumla.


  Haya Tujiandae kuchanga mchango watanzania wote tuilipe Dowans
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jamani wawalipe yaishe... kadizo!!!!
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Aliyewateua hao Majaji anataka Dowans ishinde sasa unategemea hukumu ya namna gani hapo?
   
 4. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45

  Re: Red mark
  Shirika la TANESCO halijawahi kuwa na pesa hata useme limeongezew mzigo mkuu. Mzigo ni wa mimi na wewe. Viongozi wa nchi hii nawakubali kwa jinsi wanavyocheza kama Gaucho. Wanajipasia mapande ili wakakutane nayo mbele
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hapa kuna watu wanataka kuigawana keni ya taifa waitumbue vizuri.
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  word sir
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,916
  Trophy Points: 280
  Kesi hii alitakiwa asimame werema,
  Ila kwasababu kulikuwa na malafide wamelipwa wapuuzi flani wajikoseshe ili watu flani wapige hela.
  Kidumu chama cha majambazi.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Deni + interest = Rostam Aziz
  Hakuna ujanja, kawashika pabaya
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,596
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  Laiti tungejuwa ni nani anayelipwa.Kwanini ilikuwa ngumu sana kumtaja mmiliki wake?hata mkuu mwenyewe aligoma kumtaja.Hilo linawezekana only in Tanzania.Kampuni inayoingia mkataba ba serikali halafu eti mmiliki hatajwi,na hbajulikani na wananchi.Na sasa analipwa,bado hatujui tunamlipa nani,only in Tanzania
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kesi ya ziwa Nyasa ikipilekwa mahakamani tegemea matokeo ya namna hii...
  Sheria, common sense na siasa ni vitu tofauti kabisa...
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Brigedia mstaafu Al Adawi
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  The Conspirancy of CCM!
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Samwel Sitta na Mwakiembe tunataka kusikia kutoka kwenu
   
 14. m

  malaka JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Du. Yaan ndio tunalipa hivihi? Inauma sana
   
 15. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Sometimes the Law is an ass.
   
 16. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  andhaa kanoon=the law is blind
   
 17. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Liwalo na liwe.
   
 18. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni kwanini walioishiriki kuandaa mkataba wa Richmond na Dowans wasishtakiwe kwa kuliingiza Taifa katika hasara kubwa hivi, hasa mwanasheria mkuu wa serikali waziri wa nishati na madini na wengine waliohusika directly and indirectly. Lakini sitashangaa kuona hilo kutofanyika kwa kuwa waliohusika ni watawala na wananchi ni mbumbumbu wala wengine hawajui nini kinaendelea Tz. Na wale wanaofahamu kidogo wanaona ni sawa tu kuilipa Dowans. Hii inaonesha uzalendo zero.
   
 19. p

  pembe JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Wanasheria ndio watujuze. Kwa namna mkataba ulivyoandaliwa huenda haman njia ya kukwepa/kukataa kulipa. Ndani ya mkataba owner wa Dowans yupo. Majai wetu kwa kufuata sheria zilizopo watakuwa wamefanya kazi yao inavyotakiwa. Kama wameenda kinyume vilio vyo Watanzania vitawamaliza mmoja baada ya mwingine. Mahali popote duniani HAKI prevails.
   
 20. p

  pembe JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  hawa washughulikiwe kwa uzembe lakini maadamu walishatuingiza mkenge kulipa hatuna ujanja. Wanatakiwa adhabu kali sana ila inashangaza si serikali si wabunge wote kimya! Rushwa kweli ni adui wa haki.
   
Loading...