Hatimaye Mahakama Kuu yaamuru DOWANS walipwe

Aliyewateua hao Majaji anataka Dowans ishinde sasa unategemea hukumu ya namna gani hapo?

Lakini ndo huyo huyo aliyewateuwa majaji walimvua Mh. Kafumu na mwenzake wa Sumbawanga ubunge. Hiyo kesi hata ungeipeleka wapi hatuwezi kushinda. Kosa tililolifanya katika kuingia mkataba haliwezi kuhalalisha kuvunja mkataba kinyemera kama tulivyofanya.
 
Hii imeishakula kwetu wananchi. Sisi ndo tutalipa huu mzigo, wezi wote bado wapo CCM wanadunda na wanajulikana.

Watanzania usiwe wagumu kufamya maamuzi 2015 dhidi ya dhuruma hii ya CCM!
 
ukiwa mtumwa hata ufanyaje utaendelea kuwa mtumwa hili naliona linaendelea kudhihilika kwa tanzania yetu maana haiingi sehemu kubwa ya kesi zinazohusu serikali wanashindwa kuna nini hapo?????
 
wakilipwa nasubiri kuona MWAKYEMBE na SITTA wakijuzulu la sivyo nitaamini wamwhongwa vyeo ili wawasaliti watz

namsubiri SITTA kwa hamu. mzee wakuropoka achukue maamuzi magumu kama kweli ni mzalendo kama anavyodai na kujisifu na kukandia wenzake
 
USD 65,812,630.03 (aprox. USD 66M) zingenunua x-ray ngapi? vyumba vingapi vya madarasa vingejengwa? madawati mangapi yangenunuliwa? vitanda vingapi vingenunuliwa kwa ajili ya wangonjwa wanaolazwa kwenye hospitali nchini? Matreka mangapi yangenunuliwa?

Mwisho, nani anamiliki Dowans? Kodi ya watanzania inalipwa kwa nani?
 
Tulisema sana humu, kesi hii TANESCO haishindi hata iende mahakama ya mbinguni. Dowans walitimiza masharti yote waliokubalina na TANESCO, walileta mitambo, inafanya kazi. Halafu uje useme sikulipi ondoa mitambo yako? huo tulisema ni upunguani wa hali ya juu.

Sasa wajiandae kulipa hizo na gharama za kesi na malimbikizo ya riba toka walipokaidi amri ya ICC. Itabidi walipe mara mbili ya hizo kwa ujinga tu wakutaka kudhulumu.

Zitto na Rashid Idriss na wengine tulioona mbali kuhusu hili sakata, tulisema, tukubali tu kuinunuwa hiyo mitambo iwe yetu na hili sakata liishe kwani kupinga ni kujitafutia matatizo, na kweli, Dowansa wakashitaki Kimataifa wakashinda, tukasema tena walipwe tu, watu wakajifanya wajanaja eti wakaenda kushtaki Uingereza, huko nako wakapigwa chini.
 
Lakini ndo huyo huyo aliyewateuwa majaji walimvua Mh. Kafumu na mwenzake wa Sumbawanga ubunge. Hiyo kesi hata ungeipeleka wapi hatuwezi kushinda. Kosa tililolifanya katika kuingia mkataba haliwezi kuhalalisha kuvunja mkataba kinyemera kama tulivyofanya.
Ile ya mahanga na lema?
 
Dowans ilipwe kwa maslahi ya nani katika taifa hili??? Serikali ya CCM mkimlipa tu Dowans wala msijisumbue hata kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
 
Kwa kweli suala hili ni tete. Juzi nimekwenda kununua umeme wa sh 5000 nikapewa unit 1 tu. Hakika kulipa Dowans ni kutuumiza sisi wananchi na wala siyo wafanyakazi wa Tanesco ambao huishi kwenye nyumba za serikali na umeme bure. Please wadau mzigo huu ni wetu lazima serikali itueleze waliosababisha tatizo wanafanywaje?? Kwanini wasifilisiwe hela hiyo ilipe Dowans??
 
Kwa hiyo Samuel Sitta ataendelea na msimamo wake au atasema anaiheshimu mahakama au atakaa kimya!!?
Huu ni upuuzi kwa kuwa hukumu ya hiyo case ilijulikana maana wangewezaje kutengua maamuzi ya ICC wakati pande mbili zilikubaliana ndio atakuwa msuluhishi wa mambo yao?
Kwa mara nyingine, wamepoteza pesa zetu (kuwalipa mawakili) tena.
 
Mhe Sitta inabidi ufunguke wazi juu ya huu ujambazi wa fedha za umma bila taifa kupata tija inayoendana na malipo daiwa toka kwa hii kampuni ya kitapeli ya Dowans.

Kwa hiyo Samuel Sitta ataendelea na msimamo wake au atasema anaiheshimu mahakama au atakaa kimya!!?
Huu ni upuuzi kwa kuwa hukumu ya hiyo case ilijulikana maana wangewezaje kutengua maamuzi ya ICC wakati pande mbili zilikubaliana ndio atakuwa msuluhishi wa mambo yao?
Kwa mara nyingine, wamepoteza pesa zetu (kuwalipa mawakili) tena.
 
nilidhani nimesikia Mahakama Kuu imesema HAINA MAMLAKA ya kuzuia utekelezaji wa Hukumu ya mahakama ya kimataifa/nje! Sijasikia mahakama ikisema lazma Dowans walipwe, isingeweza kusema wakati kesi haijasikilizwa na mahakama za Tanzania,
 
USD 65,812,630.03 (aprox. USD 66M) zingenunua x-ray ngapi? vyumba vingapi vya madarasa vingejengwa? madawati mangapi yangenunuliwa? vitanda vingapi vingenunuliwa kwa ajili ya wangonjwa wanaolazwa kwenye hospitali nchini? Matreka mangapi yangenunuliwa?

Mwisho, nani anamiliki Dowans? Kodi ya watanzania inalipwa kwa nani?

Kutopatikana kwa majibu sahihi ya maswali haya kunaniuma sana. Nakumbuka JK anawambia wanaccm wenzake kuwa naye hajui..wakambigia makofi mkutanoni Kimwaga. Baadae kidogo nikasikia sijui mmiliki ni mwaarabu fulani... Kichefuchefu...
 
Tulisema sana humu, kesi hii TANESCO haishindi hata iende mahakama ya mbinguni. Dowans walitimiza masharti yote waliokubalina na TANESCO, walileta motambo, inafanya kazi. Halafu uje useme sikulipi ondoa mitambo yako? huo tulisema ni upunguani wa hali ya juu.

Sasa wajiandaae kulipa hizo na gharama za kesi na malimbikizo ya riba toka walipokaidi amri ya ICC. Itabisi walipe mara mbili ya hizo kwa ujinga tu wakutaka kudhulumu.

Zitto na Rashid Idriss na wengine tulioona mbali kuhusu hili sakata, tulisema, tukubali tu kuinunuwa hiyo mitambo iwe yetu na hili sakata liishe kwani kupinga ni kujitafutia matatizo, na kweli, Dowansa wakashitaki Kimataifa wakashinda, tukasema tena walipwe tu, watu wakajifanya wajanaja eti wakaenda kushtaki Uingereza, huko nako wakapigwa chini.

Leo nakubaliana na wewe. Hapa tumeumizwa na wana CCM wenzako wanaohasimiana kwasababu ya kutaka kugombea urais!
 
Endapo kweli Dowan italipwa kodi zetu hizi za kuungaunga tu,

Je, WaTanzania tuwaeleweje Waheshimiwa Sitta na Lowassa katika hili na kwamba kati yao ni nani hasa aalikua akichezea akili umma wa nchi hii????????

Ukweli wa wenye kunufaika na Dowans sasa tuueleweje; je ni lao kwa pamoja??????????
 
Back
Top Bottom