Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 414
Katika kuadhimisha miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alitoa msamaha kwa wafungwa 3,101. Katika msamaha huo yumo kijana Deus Mallya aliyeshitakiwa kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na bila ya kuwa na leseni na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa CHADEMA marehemu Chacha Wangwe. Ajali hiyo ilitokea katika eneo la panda mbili katika mkoa wa Dodoma........