Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #41
Nilidhani hii mada imefungwa, lakini kwa vile bado inaendelea (kuonyesha ni jinsi gani hili linatugusa) nimeonelea nijibu mambo kadhaa.
a. Nchi nyingi tunazozitaja kuwa ni mfano wa nchi zisizoruhusu watu wasio na asili ya kundi la wengi wasiwe marais zina sababu ya hali hiyo. Historia ya nchi hizo ni ya kibaguzi. Marekani, Uingereza, Uarabu n.k zimejengwa kwa misingi ya kibaguzi. Jamani Wamarekani ni wabaguzi tangu mwanzo wa kuundwa Taifa lao!! Waarabu ni wabaguzi tangu enzi na enzi,!! Nchi hizo zimejengwa kwa misingi ya kibaguzi!! Hivyo unapoona nchi hizo haziruhusu au kushabikia kuwapa wazawa wenye nasaba tofauti za uongozi wa juu ni kwa sababu ya historia yao!!! Hata hivyo, Marekani imepiga hatua kubwa, kwa kujaribu kukubali watu weusi kushika nafasi za juu za uongozi!! Hivi sasa Condoleezza Rice ni wa nne katika kushika kiti cha Rais wa marekani in case!
b. Kufikiri kuwa kwa vile nchi zilizoendelea zinaendelea kubagua basi ni sawa na sisi kubagua ni mawazo ya hatari! Hatuwezi kujenga Taifa kwa njia za kibaguzi kwani hatima yake wanaobaguliwa iko siku wataasi!!! Mmeyaona Afrika ya Kusini, Ufaransa, na mmeyaona Rwanda/Burundi etc! Hakuna kitu chochote kinachohalalisha ubaguzi wa rangi/kabila /nasaba kwenye utawala wa nchi ya kidemokrasia! Je watu weusi ni bora zaidi kuliko watu wengine? Je kuwa mweusi ni kibali cha kuwa mtawala mzuri!!!?
c. Njia pekee ya kuhakikisha kuwa hakuna "mtanzania asiye mweusi" au "mzawa" anachukua madaraka ya juu ya nchi ni kuhakikisha watu hao wanaondolewa nchini kwa nguvu au kwa lazima. Tunaweza kufanya hivi kwa kuwafukuza (deportation) au kuwamaliza (extermination)!! Hatuwezi kusema Watanzania wote ni sawa na kuwa sisi hatubagui mtu au watu kwa misingi ya rangi, dini, kabila n.k lakini wakati huo huo tunapigia debe ubaguzi ulio de facto! Kwa sababu hiyo, kina SAS na wote waliotajwa na Olga wanatafutwa na kuondolewa nchini au wanapigwa alama kwenye nyuso zao!!! Aidha sisi ni taifa lisilo na ubaguzi wa aina yoyote ile de facto au de jure ama ni Taifa lenye kuficha hisia za kibaguzi.
d. Kwa vile Watanzania wenzangu hapa wanaonyesha kuanza kusahau tulikotoka ni bora niwakumbushe kidogo. Hili suala la rangi na nasaba siyo geni. Tarehe 9 Disemba 1968, Mwalimu Nyerere alitumia sikukuu ya Jamhuri kuzungumzia mambo ambayo inabidi yabadilishwe. Kati ya aliyozungumzia ni suala la ukabila na ubaguzi wa rangi. Katika sehemu ya Hotuba hiyo Mwalimu alisema hivi:
"...kuna hii minong'ono. Baadhi ya watu wetu wanahisia mbaya dhidi ya wazungu au waasia, siyo kwa sababu ya dhambi hawa watu wametenda, bali tu kwa sababu watu hawa ni Wazungu au Waasia. Ndugu zangu, msisikilize hii minong'ono. Watendeeni watu kwa kadiri ya matendo yao, kama watu binafsi, na siyo kwa kufuata rangi zao!"*
Mwalimu alimalizia hotuba hiyo kwa kusema:
"Kama kweli tumekubali kanuni kuwa 'binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja' basi hatuna budi kuamini -tena kwa wepesi zaidi'- kuwa Watanzania wote ni ndugu zangu, na Tanzania ni moja"! *
Mawazo hayo ya Mwalimu hayakuanza wakati huo. Kabla ya hapo alishalizungumzia hilo la rangi si mara moja tu bali mara nyingi. Mwezi Juni 1961 (JKN akiwa ni Waziri Mkuu) aliandika makala kwenye gazeti la shule ya sekondari ya weupe pekee ya Natal South Afrika. Kati ya baadhi aliyosema ni haya:
"...there is one thing which is quite certain. Africa will belong to Africans. I believe that this word 'Africans' can include all those who have made their home in the continent, black, brown, or white.......people stand as individual citizens, asking only for rights which can be accorded to all other individuals (in that society - M. M. Mwanakijiji)This means forgetting colour, or race, and remembering humanity. On this basis of equality I believe Africa has a good future for all her people!"
Miaka mitatu kabla ya hapo, Mwalimu akihutubia kwenye Baraza la Kutunga Sheria tarehe 15 October 1958 Mwalimu alizungumzia tena hili la rangi.
"What do we want in this country? What we want in this country is that every citizen of Tanganyika (Now Tanzania - M. M. Mwanakijiji) irrespective of his race, as long as he owes allegiance to Tanganyika, is a complete and equal citizen with anyone else"*
Inakuwaje tunasahau mafundisho hayo ndani ya miaka chini ya hamsini?
e. Ndugu zangu, hii ndiyo kanuni ninayoipigania na ninayoijenga hoja. Kama hatujajifunza kitu chochote toka kwa Mwalimu, tujifunze hili, kuwa Tanzania haiwezi kufanikiwa kama viongozi wake au baadhi ya viongozi wake wanasera za kibaguzi au kiupendeleo wa rangi, kabila, au nasaba.!! Kiongozi au mtanzania yoyote anayetaka kutumikia Taifa letu ahukumiwe kwa vigezo vya uwezo, elimu, tabia, n.k isipokuwa vigezo vya rangi, kabila, dini, n.k!
g. Ni kitendo cha kutukejeli kudhania kuwa kwa vile sisi sote ni weusi basi ni lazima tukubaliane na hoja za kutetea weusi wakati hoja hizo ni za kibaguzi. Sihitaji mtu kuniambia kuwa kwa kufanya hivi au vile naonyesha Uafrika wangu au weusi wangu! Kuwa mtu mweusi siyo kibali au leseni ya kuwa kiongozi bora au kustahili kuwa kiongozi!!! Kama kuna mtu Msukuma anayegombea Ubunge lakini hana elimu, uwezo, nia, na kipaji cha kuongoza kwanini apewe nafasi ya kugombea Ubunge dhidi ya Mhindi au Mwarabu ambaye ana elimu, uwezo , nia na kipaji cha kuwatumikia wananchi kisa tu huyo mtu ni Msukuma!? Hili halikubaliki, haliwezi kukubalika, na halitakubalika kamwe!!
h. Kama kuna kiongozi au kikundi cha viongozi ambao wana sera za kibaguzi na kiukandamizaji, viongozi hao hawana nafasi katika Taifa letu na ninatoa wito waachie ngazi kwani wao ni kansa na donda lisilo na tiba!! Hawawezi kutuletea maendeleo zaidi ya kutujaza chuki! Watu hao hawastahili kulipwa mishahara inayotokana na kodi za wananchi wote.
i. Hili la kukubali kuwa na viongozi weusi alimradi tu ni weusi ndo limetupatia viongozi wengi bomu ambao nikianza kutaja majina yao nitapata kichefuchefu!
j. Mwisho nasema hivi, kama kuna kiongozi yeyote wa CCM ambaye alitumia nafasi yake kumtupa nje SAS kwa sababu ya rangi yake na nasaba yake, kiongozi huyo aondolewe au ajiuzulu!!! Hakuna kuna samehewa kwa anayetetea ubaguzi!!! Kama JK na kundi lake walihusika kwa namna moja au nyingine (we have some ideas who did what...) kumbagusa SAS kwa misingi ya damu na rangi yake, JK awe wa kwanza kumtaka radhi SAS na kuhakikisha kuwa anaitumikia nchi yake tena bila ya hofu ya kujiona mgeni!!!! JK afanye hivyo kwa ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!
* - Uhuru na Maendeleo
* - Uhuru na Umoja