Bravo!Duterte tunaolalamika ni wafanyakazi tuliofanyakazi kwa uwezo uliotukuka na tumefikia kustaafu lakini mpaka sasa hivi hatuna jibu. Je sisi bila kuwa na uwezo wa kufikiri tungeweza kutumikia taifa hili kwa miaka zaidi ya hamsini ya kuzaliwa??? Hivi sote tunaolalamika ni vilaza tusio na uwezo wa kufikiri hata kama hatuna Phds lakini hao wenye nazo tumeattend lecture nao na wengine wametuomba notice wakiwa kwenye vikao vya chama na tuliwapa na tulifaulu kuliko wao na sasa tumekalia hapa bila kujua twende wapi.
Wapiga dili hawana shida walishajiwekea ila sisi tuliotumikia taifa kwa moyo na kuamini macomrades wetu tuliokuwa nao kwenye mvua watatukumbuka ndo tunahaha.
Mnaongea mkidhani kila mtu kala cake ya nchi hii mnasahau wengine tumo humu kujiongezea maarifa na kukutana na the Thinkers siyo kukutana na mipasho. Siyo kila anayeongea negative comment ni mpinzani au mla rushwa. Siyo kila anayeshangilia kila wanachosema viongozi ni waadilifu. Tunao wapiga dili ambao wamebewa mpaka leo na watabebwa sababu wanajua kuchezea upepo.
Mkuu hapa umeua kila kitu. Akili ni nywele kila mtu ana zake.Wapiga Dili wanahaha Kama Mapaka ya Rose Garden mkuu.
Mytake: Maisha ni Ufunguo wa Elimu.
Wewe kichwa sana sema tz haithamini michango na maoni ya watu kama ninyi.Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar - es salaam, Dr. Joel Silas ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha zilizoadimika mitaani kwa sasa hatimaye .
Kwamba hatua hiyo itarudisha fedha iliyopotea mitaani kwa sababu itasaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kwenye uchumi .
Chanzo - Nipashe .
Mytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
Wachache watakuelewaMytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
Mbona hujaelewa tu hiyo simple logic. Kazi ya benki ya kibiashara ni kuweka pesa za wateja ambao hawana kazi ya kuzifanyia pesa hizo wakati huo. Benki hiyo huwakopesha watu ambao wana kazi za kufanyia hizo pesa. Wanaokopeshwa huilipa benki hiyo riba kubwa, kwa mfano 20% kwa mwaka. Benki inamlipa yule aliyeweka pesa yake riba ndogo, kwa mfano 2% kwa mwaka, hivyo benki inapata faida ya 18% kwa mwaka kwa wewe kuweka pesa yako benki na benki kukopesha pesa yako kwa wengine wakaifanyie kazi. This is the buisness of all commercial banks.Sio kila Mhadhiri ana akili sawasawa.
Kukopa kwa serikali kwenye Bank za ndani kunarudisha vipi pesa kwenye mzunguko??
Kila mwezi serikali inakusanya (kama ambavyo wamekuwa wakituaminisha) 1Tril +, kwanini kwa kipindi chote hicho hizi zisitumike kurudisha pesa kwenye mzunguko??
Naona huyu Mhadhiri anatafuta kuteuliwa, maana wateule wengi siku Hizi ni wahadhiri.
Wasomi wamekaliwa na wanasiasa..hawaezi pindua jambo hata Liwe la ovyo wanapitisha tu kunusuru ugali waoKunawakati wasomi wetu ni janga kuliko kawaida wasomi badala ya kupeleka ushauri namna ya kunusuru uchumi anashangilia serikali kukopa
Elimu haina mwisho ila mawazo ya binadamu yana ukomo nae huyu msomi wetu mawazo yake ndo yalipo ishia
Wewe na huyo profesa mna walakini katika kuelewa athari ya serikali kukopa mabenki ya ndani. Kwanza Duniani kote serikali ikianza kukopa kwenye mabenki ya ndanì, huongeza inflation.Mbona hujaelewa tu hiyo simple logic. Kazi ya benki ya kibiashara ni kuweka pesa za wateja ambao hawana kazi ya kuzifanyia pesa hizo wakati huo. Benki hiyo huwakopesha watu ambao wana kazi za kufanyia hizo pesa. Wanaokopeshwa huilipa benki hiyo riba kubwa, kwa mfano 20% kwa mwaka. Benki inamlipa yule aliyeweka pesa yake riba ndogo, kwa mfano 2% kwa mwaka, hivyo benki inapata faida ya 18% kwa mwaka kwa wewe kuweka pesa yako benki na benki kukopesha pesa yako kwa wengine wakaifanyie kazi. This is the buisness of all commercial banks.
Pesa ikichukuliwa na aliyeikopa anaenda kuifanyia kazi. Kwa mfano atajenga hoteli, ataajili watu na kutoa huduma. Atanunua vyakula, vitapikwa na kuuzwa. Hivyo pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko. Waliojenga hiyo hoteli watapata pesa wakiwemo mafundi, vibarua, mama ntilie, wauza vifaa vya ujenzi, viwanda vya vifaa vya ujenzi, ma transporters wa vifaa vya ujenzi na hata bodaboda. Akianza kutoa huduma ya hoteli wauza nyama, samaki, maziwa, kuku na vyakula vingine watapata hela. Vivyo hivyo wazalishaji wa hivyo vyakula wakiwemo wakulima, wavuvi na wafugaji watapata hela pamoja na wasafirishaji wa hivyo vyakula. Huo ndio mzunguko wa fedha unaoletwa na benki kukopesha fedha. It is a long chain, directly ana indirectly.
Sasa serikali ikisema itakopa trilion 2 kutoka kwenye benki hizi za biashara kwenda kutekeleza miradi yake ya maendeleo huoni kuwa hiyo ni neema? Benki lazima zitachekelea maana zimepata mkopeshwaji mkubwa mwenye uhakika. Serikali ikichukua hela hizo itaenda kujenga barabara, reli na miundo mbinu zingine nyingi kama zilivyoainishwa kwenye bajeti ya maendeleo. Hivyo pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko huo huo nilioutaja hapo juu tena kwa kiwango kikubwa zaidi ya yule mkopaji binafsi mmoja mmoja. Wote wakakaohusika na hizo kazi za maendeleo directly or indirectly watajaa pesa. Hivyo kila mtu anayefanya kazi halali ataipata hiyo pesa ambayo ataiingiza kwenye mzunguko mitaani kwake na benki zetu za biashara zitapata hiyo riba zake za kukopesha kwa uhakika. Hakuna cha risk ya kutorejesha mkopo kama ilivyo kwa wakopaji binafsi.
Hiyo ndiyo logic ambayo professa amejaribu kuwaeleza, hamkumuelewa na badala yake mnajiona mnajua kuliko profesa. Si vizuri mnachofanya. Kitu kama hujaelewa uliza tu ueleweshwe.
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar - es salaam, Dr. Joel Silas ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha zilizoadimika mitaani kwa sasa hatimaye .
Kwamba hatua hiyo itarudisha fedha iliyopotea mitaani kwa sababu itasaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kwenye uchumi .
Chanzo - Nipashe .
Mytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
Huyo Prof Kala Maharage ya Wapi?
Yaani ukakope ununue ndege zingine halafu mtaani watu mtaani wapate hela kivipi?hawa wahadhiri wanamuogopa wakimkosoa utafukuzwa kazi,anatoa hoja ya kipuuzi sana,yeye anajua huo mkopa wa serikali ni kwa ajili ya nini?kama ni mshahara wa watumishi wa serikali au kulipa madeni ya nje mtu wa mtaani anapata vipi hiyo hela na huko mwaka mzima shughuli hizo zilikuwepo na bado hali ikawa mbaya.Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar - es salaam, Dr. Joel Silas ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha zilizoadimika mitaani kwa sasa hatimaye .
Kwamba hatua hiyo itarudisha fedha iliyopotea mitaani kwa sababu itasaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kwenye uchumi .
Chanzo - Nipashe .
Mytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
Sio kila Mhadhiri ana akili sawasawa.
Kukopa kwa serikali kwenye Bank za ndani kunarudisha vipi pesa kwenye mzunguko??
Kila mwezi serikali inakusanya (kama ambavyo wamekuwa wakituaminisha) 1Tril +, kwanini kwa kipindi chote hicho hizi zisitumike kurudisha pesa kwenye mzunguko??
Naona huyu Mhadhiri anatafuta kuteuliwa, maana wateule wengi siku Hizi ni wahadhiri.
Kusema ukweli ni kuwa huruWasomi wamekaliwa na wanasiasa..hawaezi pindua jambo hata Liwe la ovyo wanapitisha tu kunusuru ugali wao