Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.

Mkuu ni mimi ndioa ninachanganya watu bila sababu au ni CUF ndio imejichanganya kutangaza kususia uchaguzi kwa kauli bila matendo, huku majina yapo kwenye karatasi za kura na siku ya uchaguzi watapigiwa kura na kutangazwa wamepaya kura sifuri!.

Pasco
Wewe,mimi na wengine tunaelewa CCM ndio serikali na Serikali ndio CCM. CCM ndio dola na dola haitaki fyokofyoko. Kwa hiyo CCM imetuchanganya sote. Imekuchanganya wewe, imenichanganya mimi na wengi. Naamini CUF wanakataa kuchanganywa na chama dola na maigizo yake. Matendo ni fyokofyoko na hilo halikubaliki kwa watawala ambao hawapendi "kutawaliwa" na vyama vya ovyo ovyo! Watawala ambao wanapovaa sare zao za rangi za mboga mboga huwa wanapendeza.

Wakati mbakaji anapotumia nguvu ambazo zinatakiwa kuzuia ubakaji ni kweli unaye wa kukusimamia na kukuepusha usibakwe?

Wewe hujawasikia wenyewe wanasema siri-kali haitolewi kwa kuweka alama kwenye karatasi? Hizo karatasi si zilikuwepo pia na picha za hao hao tarehe 25.10.2015?

Nakumbuka mchangiaji mmoja aliandika "wanapobakwa na kubaki kimya haimaanishi kuwa wameridhia au wanahisi raha" na ikitokea wakifanya "fyokofyoko" wanajua malipo yake. Anahitajika mtetezi na watetetezi ni wewe, mimi na wote ambao wanapenda haki. Je jamii yetu inajali haki? Je jamii yetu inataka haki itendeke?
Nionavyo mimi ni kuwa bado jamii yetu imekumbatia unafiki. Unafiki ni adui mkubwa wa haki. Wale ambao wanaushawishi mkubwa wa kusimamia haki ndio wenye kunyima haki hizo. Pia wanatumia majukwa kuwachanganya watu.

Link For the sake of peace in the beloved Isles
 
Mkuu ni mimi ndioa ninachanganya watu bila sababu au ni CUF ndio imejichanganya kutangaza kususia uchaguzi kwa kauli bila matendo, huku majina yapo kwenye karatasi za kura na siku ya uchaguzi watapigiwa kura na kutangazwa wamepaya kura sifuri!.
Pasco
Jecha alishatangaza majimbo 31, haya atakayotangaza tarehe 20 au baada ya tarehe 20 ni maigizo tu ya DOMO-krasi ya CCM.
Link Home
 
Kama cuf wameamua kushiriki kwa mujibu wa maelezo yako naomba unipe maelezo ya tafsir hii kwann serikali iwalazimishe wafanyakaz wte kupiga kura kwa lazima na asiepiga kura atagukuzwa kazi jee katika uchaguz wa mwanzo hili lilikuepo (2) kwann kusiwepo tamko la tume juu ya midahalo kama ile ya mwanzo (kampen) kwa kipindi hiki kifup kwa mantiki hio jecha kaona pasipo kuwekwa jina la kiongoz anaependwa na wazanzibar na chaguo la wazanzibar maalim atajiharibia sifa na uwezo na hata kuishi kwa wasi wasi kama anavyoishi kwa wakat huu
 
Cha kushaangaza hapa mpira wao uwanja wao refa wao kamisaa pia wao lkn hawajiamin kwann sasa wakat wazanzibar hakuna hata mmoja asiejua kuwa Zanzibar ni nchi inayoendeshwa kibeberu hakuna demokrasia na hili aliliweka waz kiongoz wao mmoja wakat wa bunge la katiba almarhun asha bakar kuwa Zanzibar ni nchi ya mapinduz haipatikan kwa vikaratas sasa mpaka hapo mwenye macho haambiwi tazama nawakilisha
 
Kwa hio unaposema jecha katoa tamko rasm la wagombea wte kushiriki ktk uchaguz huo ni unafki maana ukweli unafahamika hakuna uchaguz Zanzibar bali kuna uchafuz
 
Wanabodi,

Angalizo: Facts are very stubborn things, hivyo ninachoandika hapa ni facts, yaani kitu halisi kilichopo na sio dhana, wala sio hisia, wala mambo ya kufikirika, hivyo yoyote atakayetofautiana na mimi kuhusu bandiko hili, naomba tutofautiane kwa hoja zenye facts, na sio hisia au kelele!. Kwenye bandiko hili naomba mzigatie kitu kinachoitwa "expressly" na "Impliedly"

Hatimaye Chama cha Wananchi, CUF, kimeamua kwa ridhaa yake chenyewe, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar, not expressly, but impliedly, nikimaanisha baada ya Tangazo la jana la Mwenyekiti wa ZEC, Jecha, kuwa hakuna chama wala mgombea aliyejitoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, it is now a fact kuwa CUF ni washiriki rasmi wa uchaguzi huo wa marudio, watake wasitake!, waseme, wasiseme, kilichopo mezani ni fact za ushiriki wa CUF.

Chaguzi zote zinatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, kama CUF walitimiza sheria zote, taratibu zote, na kufuata kanuni zote, kuwa wagombea halali wa Uchaguzi wa October, uchaguzi huu wa marudio, unarudia kila kitu kama kilivyokuwa ile October, hivyo CUF ingekuwa imedhamiria kwa dhati kujitoa, ilipaswa ifuate sheria zile zile, taratibu na kanuni za kujitoa rasmi!. Huku kujitoa kwa kuitisha Press Conference na kutangaza kujitoa, bila kufuata kanuni na taratibu rasmi za kujitoa, sio kujitoa maana hakutambuliki rasmi kama ni kujitoa, bali ni kuthibitisha kushiriki, impliedly, yaani CUF wanajitoa expressly kwa kauli na matamko ya kujitoa, huku wakifanya matendo ya kushiriki rasmi uchaguzi huo!.

Hivyo hata kama CUF itawachagiza wafuasi wake wasijitokeze kupiga kura, kitendo cha karatasi za uchaguzi, kuwa na picha na majina ya wagombea wa CUF, hii inamaana CUF imeshiriki rasmi uchaguzi huo, kwa lazima, itake isitake, na amini usiamini, kuna watu watajitokeza na kuwapigia kura wagombea wa CUF, hivyo matokeo yataonyesha CCM kupata ushindi wa asilimia 99% ya kura zote dhidi ya CUF yenye asilimia 01%.

Najua kuna wengi watachukizwa na bandiko hili, na wengine, watakereka ila hizi ndio facts zenyewe kuwa CUF imeidhia kushiriki!.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi ule, mimi ni miongoni mwa wanajf tunaojitokeza na kutoa ushauri wa bure wa the right thing to do!, ila kwa vile we are no bodies, tunaishia kupuuzwa, hata kuitwa wachochezi, hadi yanapotokea ndipo tunawakumbusha tulishauri nini na kimetokea nini!.

Jecha alipofuta uchaguzi ule, tukasema kitendo kile ni batili, Jecha hana mamlaka ya kufuta matokea ya uchaguzi, Jecha ni Mwenyekiti wa ZEC ila Jecha sio ZEC, kitendo cha Jecha kujigeuza ZEC na kutoa matamko batili, bila kupingwa rasmi na yoyote, hbuku mimi nilikuita ni kuridhia. Zanzibar inatawaliwa kwa mujibu wa katiba, iliyoweka misingi ya sheria, taatibu na kanuni, ikiwemo mihimili rasmi ya serikali ya SMZ, mahakama, na BLW, hivyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuufuta ubatili ule wa Jecha ni mahaka kupitia vufungu vya sheria. No body, did anything on this. Nikasema Zanzibar wameridhia. Kupinga rasmi sio kupinga kwa matamko bali kuchukua hatua rasmi.

Nilipouliza humu kuhusu hili, sikujibiwa
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote

Nikaja kuwaambia kuhusu hili,
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima ...
nikaishia kubezwa.

Sasa leo nawaambia CUF wameridhia, najua wa kubeza mtabeza, bezeni tuu, mwisho wa siku facts ndizo zitakazo simama mpaka mwisho!.

Hata hivyo mpaka hapa tulipofikia, CUF bado wanayo nafasi moja ya mwisho, na ndio karata pekee ya turufu iliyobakia nayo is to do the right thing which should have been since day one, nayo ni kwenda mahakamani kuusimamisha rasmi uchaguzi huu wa marudia kwa hoja za msingi kuwa uchaguzi wa October 25, ni uchaguzi halali, washindi wameishapewa vyeti halali vya ushindi, hivyo kuitaka mahakama itoa kitu kinaitwa "Executive Orders" za "exhibition, certiorary na mandamus" kuilazimisha ZEC kutangaza matokeo halali ya uchaguzi wa October 25, hivyo mshindi halali kutangazwa!.

I wish CUF all the best, au ushiriki mwema wa uchaguzi wa marudio, au to do the right thing!. huku kuendelea kupiga kelele kwenye media, hakutaisaidia CUF chochote, kwa sababu uchaguzi ukiishafanyika, na CCM kushinda, there is nothing more that CUF can do, na CCM ya Magufuli sio CCM ya Kikwete ya kukaa mezani, kubembelezana na kutafuta miafaka, CCM ya Magufuli ni "hapa kazi tuu!", hakuna tena kuleta fyoko fyoko kama walizomletea Kikwete.

Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa!.
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? | JamiiForums ...
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Alishinda...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. Waziri ...
Jumatatu Njema
Pasco
Ukweli wa uzi huu, utatimia kesho!, wengi mtakishuhudia hiki ninachokisema, japo wamedai kuwa hawatashiriki, kwa sababu wamesusa, tayari CUF kama chama kinashiriki kikamilifu, majina ya wagombea wao tayari yapo kwenye karatasi za kura!, na kesho watu watajitokeza, watawapigia kura, tofauti na uchaguzi wa October, matokeo ya uchaguzi wa kesho, CUF watashindwa vibaya, infact watapigwa chini rasmi!.

Tusubiri tushuhudie hiyo kesho.

Pasco
 
Mambo yamebana mnaamua kutunga story zisizo na maana.. Mkubali tu mnatumia nguvu zisizo na msingi wowote na dunia nzima imeliona hilo. Ni aibu sana kwa kweli
 
Hawa ndio wanahabari wetu wanaotarajiwa kuielimisha jamii!!
Naona Mnaota ndoto za mchana
ni aibu kusema mtu huyu ni mwandishi,shame.Hajui hata kutofautisha maneno,haelewi hata maana ya neno kuridhia.
Mambo yamebana mnaamua kutunga story zisizo na maana.. Mkubali tu mnatumia nguvu zisizo na msingi wowote na dunia nzima imeliona hilo. Ni aibu sana kwa kweli
Hayawi hayawi yamekua.
Kwa taarifa yenu:
1. CUF hawawezi kudai kuwa wamejitoa katika uchaguzi kwani katika uchaguzi wa marudio hakuna kuingiza wagombea wapya wala kuengua waliopo.

2. Kususia kupiga kura ni hiari. Siku ya kupiga kura una hiari ya kwenda au kutakwenda na ukienda una hiari ya kumpigia utakaye. Kutokwenda kupiga kura hakuna nguvu yoyote kisheria na kikatiba.

3. Maalim (na CUF) kazikwa na kauli zake mwenywe....1. Uchaguzi kipindi cha mkapa, hitilafu ilitokea kama 20% huko Pemba. CUF wakadai uchaguzi mzima urudiwe. Mkapa akagoma, ukatokea mtiti wa hatari, watu kukimbilia mombasa, na kelele hadi jumuiya ya kimataifa.

Safari hii, hitilafu imetokea pungufu ya 20%ya maeneo. Sasa Maalim akataka kuendelea (kama alivotaka Mkapa kipindi kile), akakabwa hapo hapo, wewe msimamo wako ni wa kurudia uchaguzi mzima. Sie twarudia wote kama ulivyosisitiza huko awali. Kumeza matapishi kukamshinda....mie nashangaa vile vikao alikaajr mtu mmoja pekee?
Hatari sana hiyo.

Halafu anataka Kikwete kisha JPM waingilie kati. Maneno yake yakamkaba kwani kila siku alikuwa akiwabeza hawana mamlaka zanzibar na zanzibar ni nchi kamili. Kikabuma...tena hadharani. Jamaa wakampa mkuu wa majeshi acheze nao.

4.Mziki utakuwa mtamu endapo utakuta kuna watu wamewapigia kura hao wagombea wa CUF....hili lilikitokea bezo lake litakuwa tamu.
 
wewe naye ni mjinga tu usiyejielewa,unasimamia nin?mbona wasimamizi wa kimataifa hawakuona kasoro hizo kwa kiwango hicho?kudhihirisha hilo ni pale kura za NEC zilipokubaliwa huku zile za ZEC zikikataliwa wakati muda na eneo la kupiga kura ni ulele na huhesabiwa jengo hilo hilo.
Ukiwa ccm lazima ujitoe ufahamu au uwe mpuuzi asilia ili uweze kuwaunga mkono kwenye upuuzi wao.
 
Una haja gani ya kutumia lugha kama hizo?
Basi wewe mwerevu umemsaidia nini maalim hadi sasa?
Wenzio yuko presidential suite Serena anapiga selfie kila baada ya panadol moja.
Endeleeni na "werevu" wenu na ndo maana mtapigwa na ccm kila siku.
 
ndio maana nasema ukiwa ccm lazima ujitoe ufahamu,hilo la presidential suite sio geni hata kidogo.Makamu wa Rais na Marais wote waliopita hutumia hotel zenye presidential suite wanapokuwa ugenini kwa sababu yoyote ile,iwe ugonjwa,ziara nk.Sasa wewe umeona ndiyo hoja,hiyo ni indicator moja ya kujitoa ufahamu mliyonayo wafuasi wengi wa ccm.Akili ndogo kutawala akili kubwa,rejea maneno haya ya msigwa.
Hujui hata impact ya CUF kususia uchaguzi kwenye siasa za zanzibar,waulize basi wenye uelewa kidogo ndio urudi hapa.
 
Mwenzako kwa elimu hii hii ninayoimwaga humu, nachukuliwa na wazungu na kulipwa consultancy ya maana tuu, huku wabongo wenzagu wakinibeza!. Naamini kabisa, kama CUF wana akili japo kidogo, watajua nimesema nini humu na wanapaswa kufanya nini, lakini nao akili zao zikiwa ndio kama hizi zako, tusubiri tuu matokeo ya kushehekea ushindi!.

Na kwa kadri wanavyochelewa kuchukua hatua stahiki, ndivyo "the law of limitation" itakavyokuja kuwazuia to do the right thing!, amini nakuambia, CUF bado wako usingizini, by the time wanaamka, it might be too little too late!.

Pasco
Usimuamshe aliyelala
 
Hivi CUF wakisusia uchaguzi na ccm ikachukua majimbo yote Zanzibar. Kisha ccm ikafanya transformation kubwa ya kiuchumi ikiwa chini ya CCM ngazi zote. CUF mwaka 2020 watakuja kusema nini?

CUF naona inapoteza zaid ya kugain.
transformation yoyote ni community participatory based-sasa wananchi wawakutaki maendeleo hayo hatatoka wapi
 
Ukweli wa uzi huu, utatimia kesho!, wengi mtakishuhudia hiki ninachokisema, japo wamedai kuwa hawatashiriki, kwa sababu wamesusa, tayari CUF kama chama kinashiriki kikamilifu, majina ya wagombea wao tayari yapo kwenye karatasi za kura!, na kesho watu watajitokeza, watawapigia kura, tofauti na uchaguzi wa October, matokeo ya uchaguzi wa kesho, CUF watashindwa vibaya, infact watapigwa chini rasmi!.

Tusubiri tushuhudie hiyo kesho.

Pasco

Unadhani wao hawajui hilo

Tatizo lako unadhani kuwa CUF ni wajinga woooote...wewe ndio una akili
 
Jecha alipofuta uchaguzi ni nani alikuwa amejaza fomu ya malalamiko?
Paschal jiongeze, kama kusoma hujui basi hata picha huoni?.
Paskali jibu hili swali

Unapigwa na pacha mmoja unaenda kumshtakia kwa pacha mwenzie?
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
  1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
  2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
  3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
  4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
  5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
  6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
  7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
  8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
  9. Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa?!. Utosheshaji Ulipogoma, Ukafutwa?!
  10. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
  11. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  12. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
  13. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Back
Top Bottom