Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi ule, mimi ni miongoni mwa wanajf tunaojitokeza na kutoa ushauri wa bure wa the right thing to do!, ila kwa vile we are no bodies, tunaishia kupuuzwa, hata kuitwa wachochezi, hadi yanapotokea ndipo tunawakumbusha tulishauri nini na kimetokea nini!.

Jecha alipofuta uchaguzi ule, tukasema kitendo kile ni batili, Jecha hana mamlaka ya kufuta matokea ya uchaguzi, Jecha ni Mwenyekiti wa ZEC ila Jecha sio ZEC, kitendo cha Jecha kujigeuza ZEC na kutoa matamko batili, bila kupingwa rasmi na yoyote, hbuku mimi nilikuita ni kuridhia. Zanzibar inatawaliwa kwa mujibu wa katiba, iliyoweka misingi ya sheria, taatibu na kanuni, ikiwemo mihimili rasmi ya serikali ya SMZ, mahakama, na BLW, hivyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuufuta ubatili ule wa Jecha ni mahaka kupitia vufungu vya sheria. No body, did anything on this. Nikasema Zanzibar wameridhia. Kupinga rasmi sio kupinga kwa matamko bali kuchukua hatua rasmi.

Nilipouliza humu kuhusu hili, sikujibiwa
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote

Nikaja kuwaambia kuhusu hili,
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima ...
nikaishia kubezwa.

Sasa leo nawaambia CUF wameridhia, najua wa kubeza mtabeza, bezeni tuu, mwisho wa siku facts ndizo zitakazo simama mpaka mwisho!.

Hata hivyo mpaka hapa tulipofikia, CUF bado wanayo nafasi moja ya mwisho, na ndio karata pekee ya turufu iliyobakia nayo is to do the right thing which should have been since day one, nayo ni kwenda mahakamani kuusimamisha rasmi uchaguzi huu wa marudia kwa hoja za msingi kuwa uchaguzi wa October 25, ni uchaguzi halali, washindi wameishapewa vyeti halali vya ushindi, hivyo kuitaka mahakama itoa kitu kinaitwa "Executive Orders" za "exhibition, certiorary na mandamus" kuilazimisha ZEC kutangaza matokeo halali ya uchaguzi wa October 25, hivyo mshindi halali kutangazwa!.

Pasco
Ninafuatilia hii kesi ya Uchaguzi Kenya, kwa hoja zinavyotolewa, ni kama Tanzania hatuna Mawakili!. Kumbe alichokifanya Chebukat ni sawa na alichokifanya Jecha!.

Chebukat kajigeuza tume ya uchaguzi Kenya na kumtangaza Ruto kashinda. Jecha hakuwa na mamlaka ya kujigeuza ZEC na kufuta uchaguzi!.

Tofauti ya Kenya na Tanzania, sisi matokeo ya urais yakiisha tangazwa ni final and conclusive, hayawezi kupingwa mahakamani.

Kilichofanyika Zanzibar ile 2015 ndicho kilichofanyika Kenya. Mahakama Kuu inakwenda kufuta matokeo, zoezi la kuhesabu upya kurudiwa, kama Ruto ameshinda kweli, then atatangazwa baada ya kuhesabu upya kwenye majumlisho.

Kiukweli kabisa kwenye tasnia ya sheria, issues serious kama hizi ni kama hatuna kabisa mawakili!.

Tunapoelekea kwenye Mtangamano wa Africa Mashariki, ukifuka muda wa free movement of labor, kiukweli mawakili wa Kenya watakomba almost everything kutoka kwa mawakili lala wa Tanzania!.
P
 
Back
Top Bottom