Wewe,mimi na wengine tunaelewa CCM ndio serikali na Serikali ndio CCM. CCM ndio dola na dola haitaki fyokofyoko. Kwa hiyo CCM imetuchanganya sote. Imekuchanganya wewe, imenichanganya mimi na wengi. Naamini CUF wanakataa kuchanganywa na chama dola na maigizo yake. Matendo ni fyokofyoko na hilo halikubaliki kwa watawala ambao hawapendi "kutawaliwa" na vyama vya ovyo ovyo! Watawala ambao wanapovaa sare zao za rangi za mboga mboga huwa wanapendeza.Mkuu ni mimi ndioa ninachanganya watu bila sababu au ni CUF ndio imejichanganya kutangaza kususia uchaguzi kwa kauli bila matendo, huku majina yapo kwenye karatasi za kura na siku ya uchaguzi watapigiwa kura na kutangazwa wamepaya kura sifuri!.
Pasco
Wakati mbakaji anapotumia nguvu ambazo zinatakiwa kuzuia ubakaji ni kweli unaye wa kukusimamia na kukuepusha usibakwe?
Wewe hujawasikia wenyewe wanasema siri-kali haitolewi kwa kuweka alama kwenye karatasi? Hizo karatasi si zilikuwepo pia na picha za hao hao tarehe 25.10.2015?
Nakumbuka mchangiaji mmoja aliandika "wanapobakwa na kubaki kimya haimaanishi kuwa wameridhia au wanahisi raha" na ikitokea wakifanya "fyokofyoko" wanajua malipo yake. Anahitajika mtetezi na watetetezi ni wewe, mimi na wote ambao wanapenda haki. Je jamii yetu inajali haki? Je jamii yetu inataka haki itendeke?
Nionavyo mimi ni kuwa bado jamii yetu imekumbatia unafiki. Unafiki ni adui mkubwa wa haki. Wale ambao wanaushawishi mkubwa wa kusimamia haki ndio wenye kunyima haki hizo. Pia wanatumia majukwa kuwachanganya watu.
Link For the sake of peace in the beloved Isles