Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Angalizo: Facts are very stubborn things, hivyo ninachoandika hapa ni facts, yaani kitu halisi kilichopo na sio dhana, wala sio hisia, wala mambo ya kufikirika, hivyo yoyote atakayetofautiana na mimi kuhusu bandiko hili, naomba tutofautiane kwa hoja zenye facts, na sio hisia au kelele!. Kwenye bandiko hili naomba mzigatie kitu kinachoitwa "expressly" na "Impliedly"

Hatimaye Chama cha Wananchi, CUF, kimeamua kwa ridhaa yake chenyewe, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar, not expressly, but impliedly, nikimaanisha baada ya Tangazo la jana la Mwenyekiti wa ZEC, Jecha, kuwa hakuna chama wala mgombea aliyejitoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, it is now a fact kuwa CUF ni washiriki rasmi wa uchaguzi huo wa marudio, watake wasitake!, waseme, wasiseme, kilichopo mezani ni fact za ushiriki wa CUF.

Chaguzi zote zinatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, kama CUF walitimiza sheria zote, taratibu zote, na kufuata kanuni zote, kuwa wagombea halali wa Uchaguzi wa October, uchaguzi huu wa marudio, unarudia kila kitu kama kilivyokuwa ile October, hivyo CUF ingekuwa imedhamiria kwa dhati kujitoa, ilipaswa ifuate sheria zile zile, taratibu na kanuni za kujitoa rasmi!. Huku kujitoa kwa kuitisha Press Conference na kutangaza kujitoa, bila kufuata kanuni na taratibu rasmi za kujitoa, sio kujitoa maana hakutambuliki rasmi kama ni kujitoa, bali ni kuthibitisha kushiriki, impliedly, yaani CUF wanajitoa expressly kwa kauli na matamko ya kujitoa, huku wakifanya matendo ya kushiriki rasmi uchaguzi huo!.

Hivyo hata kama CUF itawachagiza wafuasi wake wasijitokeze kupiga kura, kitendo cha karatasi za uchaguzi, kuwa na picha na majina ya wagombea wa CUF, hii inamaana CUF imeshiriki rasmi uchaguzi huo, kwa lazima, itake isitake, na amini usiamini, kuna watu watajitokeza na kuwapigia kura wagombea wa CUF, hivyo matokeo yataonyesha CCM kupata ushindi wa asilimia 99% ya kura zote dhidi ya CUF yenye asilimia 01%.

Najua kuna wengi watachukizwa na bandiko hili, na wengine, watakereka ila hizi ndio facts zenyewe kuwa CUF imeidhia kushiriki!.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi ule, mimi ni miongoni mwa wanajf tunaojitokeza na kutoa ushauri wa bure wa the right thing to do!, ila kwa vile we are no bodies, tunaishia kupuuzwa, hata kuitwa wachochezi, hadi yanapotokea ndipo tunawakumbusha tulishauri nini na kimetokea nini!.

Jecha alipofuta uchaguzi ule, tukasema kitendo kile ni batili, Jecha hana mamlaka ya kufuta matokea ya uchaguzi, Jecha ni Mwenyekiti wa ZEC ila Jecha sio ZEC, kitendo cha Jecha kujigeuza ZEC na kutoa matamko batili, bila kupingwa rasmi na yoyote, hbuku mimi nilikuita ni kuridhia. Zanzibar inatawaliwa kwa mujibu wa katiba, iliyoweka misingi ya sheria, taatibu na kanuni, ikiwemo mihimili rasmi ya serikali ya SMZ, mahakama, na BLW, hivyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuufuta ubatili ule wa Jecha ni mahaka kupitia vufungu vya sheria. No body, did anything on this. Nikasema Zanzibar wameridhia. Kupinga rasmi sio kupinga kwa matamko bali kuchukua hatua rasmi.

Nilipouliza humu kuhusu hili, sikujibiwa
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote

Nikaja kuwaambia kuhusu hili,
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima ...
nikaishia kubezwa.

Sasa leo nawaambia CUF wameridhia, najua wa kubeza mtabeza, bezeni tuu, mwisho wa siku facts ndizo zitakazo simama mpaka mwisho!.

Hata hivyo mpaka hapa tulipofikia, CUF bado wanayo nafasi moja ya mwisho, na ndio karata pekee ya turufu iliyobakia nayo is to do the right thing which should have been since day one, nayo ni kwenda mahakamani kuusimamisha rasmi uchaguzi huu wa marudia kwa hoja za msingi kuwa uchaguzi wa October 25, ni uchaguzi halali, washindi wameishapewa vyeti halali vya ushindi, hivyo kuitaka mahakama itoa kitu kinaitwa "Executive Orders" za "exhibition, certiorary na mandamus" kuilazimisha ZEC kutangaza matokeo halali ya uchaguzi wa October 25, hivyo mshindi halali kutangazwa!.

I wish CUF all the best, au ushiriki mwema wa uchaguzi wa marudio, au to do the right thing!. huku kuendelea kupiga kelele kwenye media, hakutaisaidia CUF chochote, kwa sababu uchaguzi ukiishafanyika, na CCM kushinda, there is nothing more that CUF can do, na CCM ya Magufuli sio CCM ya Kikwete ya kukaa mezani, kubembelezana na kutafuta miafaka, CCM ya Magufuli ni "hapa kazi tuu!", hakuna tena kuleta fyoko fyoko kama walizomletea Kikwete.

Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa!.
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? | JamiiForums ...
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Alishinda...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. Waziri ...
Jumatatu Njema

Pasco
 
Ulichoandika ndio uhalisia...nilikwambia viongozi,wasemaji na wenye maamuzi ukawa ni wana"CCM";

1.Seif keshachukuwa 350M kaenda matibabu bila kuitisha press kwamba anaumwa nini?..ambapo wana CUF halisi walipaswa kujuwa yeye kamwaga Shein na Magufuli ili protokali ya nje ya nchi izingatiwe...yah pia alimwaga EL pale mikocheni.

2.uchaguzi wa marudio kisheria hausishi wagombea wapya wala kuengua waliopo...japo kisiasa waweza kuwarubuni wanachama wako kama ambavyo Seif,Zitto ne wengine walivyolaghai.

3.Seif na viongozi wengine CUF "mission" na vision" yao CUF kivitendo ni tofauti na nadharia.
4.Ukitumia akili ya kawaida huwezi kugunduwa huu mchezo.

5.Kosa kubwa ni kwa vyama vyote vya upinzani kutokuwa na utamaduni wa kukosowa maamuzi ya viongozi hata kwa waandishi wa habari,katiba za vyama haziruhusu viongozi kushitakiwa,ukimhoji unafukuzwa...hii ni faida kwa CCM kwani inahakikisha watu wao wanakuwa wafalme.

6.Angalau CCM wanaruhusu kwa wanachama ndani na nje kukosowa viongozi na kusigana mawazo...hii ni afya kwa chama.

Nawakilisha.
 
Hivyo hata kama CUF itawachagiza wafuasi wake wasijitokeze kupiga kura, kitendo cha karatasi za uchaguzi, kuwa na picha na majina ya wagombea wa CUF, hii inamaana CUF imeshiriki rasmi uchaguzi huo, kwa lazima, itake isitake, na amini usiamini, kuna watu watajitokeza na kuwapigia kura wagombea wa CUF, hivyo matokeo yataonyesha CCM kupata ushindi wa asilimia 99% ya kura zote dhidi ya CUF yenye asilimia 01%.
Inakera lakini huo ni mkweli mtupu! Unaokera ni huu ukweli usio haba manake heri ya mwaka 2001 palikuwa na kura za maruhani lakini kwenye uchaguzi huu so long as wagombea ni wale wale basi hakuna cha kura za maruhani! Hii ndio sababu kwanini kwenye uchumi huwa tunasoma Managerial Decision Making! Palikuwa panahitaji busara ya hali ya juu kufikia maamuzi ya ama CUF ishiriki au isishiriki kwa maana, hata wakisusia; CCM wala haiwasumbui... sana sana watafurahia tu! Isitoshe CCM tayari wana uzoefu huo wa kuongoza peke yao baada ya CUF kususia! Sidhani ikiwa CUF waliona walifaidikika nini kama chama baada ya kususia ule uchaguzi wa 2001. Ni sawasawa na leo hii CHADEMA wasusie uchaguzi kwenye majimbo ya Kilimanjaro na Arusha... watachosema CCM ni "Ahsante Mbowe!" Na kwa hili, watasema "Ahsante Seif (CUF?)"
 
Hawa ndio wanahabari wetu wanaotarajiwa kuielimisha jamii!!
Mwenzako kwa elimu hii hii ninayoimwaga humu, nachukuliwa na wazungu na kulipwa consultancy ya maana tuu, huku wabongo wenzagu wakinibeza!. Naamini kabisa, kama CUF wana akili japo kidogo, watajua nimesema nini humu na wanapaswa kufanya nini, lakini nao akili zao zikiwa ndio kama hizi zako, tusubiri tuu matokeo ya kushehekea ushindi!.

Na kwa kadri wanavyochelewa kuchukua hatua stahiki, ndivyo "the law of limitation" itakavyokuja kuwazuia to do the right thing!, amini nakuambia, CUF bado wako usingizini, by the time wanaamka, it might be too little too late!.

Pasco
 
Wanabodi,

Angalizo: Facts are very stubborn things, hivyo ninachoandika hapa ni facts, yaani kitu halisi kilichopo na sio dhana, wala sio hisia, wala mambo ya kufikirika, hivyo yoyote atakayetofautiana na mimi kuhusu bandiko hili, naomba tutofautiane kwa hoja zenye facts, na sio hisia au kelele!. Kwenye bandiko hili naomba mzigatie kitu kinachoitwa "expressly" na "Impliedly"

Hatimaye Chama cha Wananchi, CUF, kimeamua kwa ridhaa yake chenyewe, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar, not expressly, but impliedly, nikimaanisha baada ya Tangazo la jana la Mwenyekiti wa ZEC, Jecha, kuwa hakuna chama wala mgombea aliyejitoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, it is now a fact kuwa CUF ni washiriki rasmi wa uchaguzi huo wa marudio, watake wasitake!, waseme, wasiseme, kilichopo mezani ni fact za ushiriki wa CUF.

Chaguzi zote zinatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, kama CUF walitimiza sheria zote, taratibu zote, na kufuata kanuni zote, kuwa wagombea halali wa Uchaguzi wa October, uchaguzi huu wa marudio, unarudia kila kitu kama kilivyokuwa ile October, hivyo CUF ingekuwa imedhamiria kwa dhati kujitoa, ilipaswa ifuate sheria zile zile, taratibu na kanuni za kujitoa rasmi!. Huku kujitoa kwa kuitisha Press Conference na kutangaza kujitoa, bila kufuata kanuni na taratibu rasmi za kujitoa, sio kujitoa maana hakutambuliki rasmi kama ni kujitoa, bali ni kuthibitisha kushiriki, impliedly, yaani CUF wanajitoa expressly kwa kauli na matamko ya kujitoa, huku wakifanya matendo ya kushiriki rasmi uchaguzi huo!.

Hivyo hata kama CUF itawachagiza wafuasi wake wasijitokeze kupiga kura, kitendo cha karatasi za uchaguzi, kuwa na picha na majina ya wagombea wa CUF, hii inamaana CUF imeshiriki rasmi uchaguzi huo, kwa lazima, itake isitake, na amini usiamini, kuna watu watajitokeza na kuwapigia kura wagombea wa CUF, hivyo matokeo yataonyesha CCM kupata ushindi wa asilimia 99% ya kura zote dhidi ya CUF yenye asilimia 01%.

Najua kuna wengi watachukizwa na bandiko hili, na wengine, watakereka ila hizi ndio facts zenyewe kuwa CUF imeidhia kushiriki!.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi ule, mimi ni miongoni mwa wanajf tunaojitokeza na kutoa ushauri wa bure wa the right thing to do!, ila kwa vile we are no bodies, tunaishia kupuuzwa, hata kuitwa wachochezi, hadi yanapotokea ndipo tunawakumbusha tulishauri nini na kimetokea nini!.

Jecha alipofuta uchaguzi ule, tukasema kitendo kile ni batili, Jecha hana mamlaka ya kufuta matokea ya uchaguzi, Jecha ni Mwenyekiti wa ZEC ila Jecha sio ZEC, kitendo cha Jecha kujigeuza ZEC na kutoa matamko batili, bila kupingwa rasmi na yoyote, hbuku mimi nilikuita ni kuridhia. Zanzibar inatawaliwa kwa mujibu wa katiba, iliyoweka misingi ya sheria, taatibu na kanuni, ikiwemo mihimili rasmi ya serikali ya SMZ, mahakama, na BLW, hivyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuufuta ubatili ule wa Jecha ni mahaka kupitia vufungu vya sheria. No body, did anything on this. Nikasema Zanzibar wameridhia. Kupinga rasmi sio kupinga kwa matamko bali kuchukua hatua rasmi.

Nilipouliza humu kuhusu hili, sikujibiwa
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote

Nikaja kuwaambia kuhusu hili,
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima ...
nikaishia kubezwa.

Sasa leo nawaambia CUF wameridhia, najua wa kubeza mtabeza, bezeni tuu, mwisho wa siku facts ndizo zitakazo simama mpaka mwisho!.

Hata hivyo mpaka hapa tulipofikia, CUF bado wanayo nafasi moja ya mwisho, na ndio karata pekee ya turufu iliyobakia nayo is to do the right thing which should have been since day one, nayo ni kwenda mahakamani kuusimamisha rasmi uchaguzi huu wa marudia kwa hoja za msingi kuwa uchaguzi wa October 25, ni uchaguzi halali, washindi wameishapewa vyeti halali vya ushindi, hivyo kuitaka mahakama itoa kitu kinaitwa "Executive Orders" za "exhibition, certiorary na mandamus" kuilazimisha ZEC kutangaza matokeo halali ya uchaguzi wa October 25, hivyo mshindi halali kutangazwa!.

I wish CUF all the best, au ushiriki mwema wa uchaguzi wa marudio, au to do the right thing!. huku kuendelea kupiga kelele kwenye media, hakutaisaidia CUF chochote, kwa sababu uchaguzi ukiishafanyika, na CCM kushinda, there is nothing more that CUF can do, na CCM ya Magufuli sio CCM ya Kikwete ya kukaa mezani, kubembelezana na kutafuta miafaka, CCM ya Magufuli ni "hapa kazi tuu!", hakuna tena kuleta fyoko fyoko kama walizomletea Kikwete.

Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa!.
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? | JamiiForums ...
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Alishinda...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. Waziri ...
Jumatatu Njema
Pasco
Soma vizuri ibara ya 119(13) ya Katiba ya Zanzibar inayozuia kushtakiwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kisha uje upitie tena huu utumbo uliyoandika hapa.
 
CCM watashinda..Na CUF wanajua watashinda...Na ndio lengo la Uchaguzi kurudiwa ili CCM ishinde....CCM watapata hata asilimia 100...yeah...Na CUF wanajua....

Hapa kuna ishu inaitwa moral authority

Kwenu ninyi mnaliangalia kwa ukaribu.......lakini ina impact kubwa sana kwa CCM kulikoni kwa CUF....

CUF wamefanya maamuzi sahihi kabisa kukaa pembeni kwa miaka mitano...Come 2020 Watakuwa wamejiweka katika nafasi nzuri zaidi.....Watu wengi wametambua ushwetani wa CCM ...Na hii ni faida kwa CUF

Hakuna haja yoyote ya CUF kushiriki uchaguzi huu

Kitakachotokea na ndicho ZEC wanafanya...watayapanga matokeo na kumpa Seif asilimia kama arobaini na kitu...halafu watampa Umakamu wa Rais......

Hapo CUF itabidi wasimamie kauli zao...Msidhani kwamba things will be the same

Nawapongeza sana CUF wamekuwa very smart kwenye hili
 
Hivi CUF wakisusia uchaguzi na ccm ikachukua majimbo yote Zanzibar. Kisha ccm ikafanya transformation kubwa ya kiuchumi ikiwa chini ya CCM ngazi zote. CUF mwaka 2020 watakuja kusema nini?

CUF naona inapoteza zaid ya kugain.
 
ndo mana siku zote mtu unaambiwa nchi yenye demokrasia haina maendeleo zec wanaforce watu kukubali mfumo wa utawala wanaoutaka wao kwa kutumia kivuli cha demokrasia.
 
Hivi CUF wakisusia uchaguzi na ccm ikachukua majimbo yote Zanzibar. Kisha ccm ikafanya transformation kubwa ya kiuchumi ikiwa chini ya CCM ngazi zote. CUF mwaka 2020 watakuja kusema nini?

CUF naona inapoteza zaid ya kugain.
ccm ifanye Transformation ya uchumi ! bila shaka wewe kijana ni mgeni nchi hii .
 
Back
Top Bottom