Hatimaye apata mnunuzi wa Bikra yake...

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Yule msichana wa Romania Alina Percea aliyatangaza kuiweka bikira yake kwenye mnada nchini Ujerumani miezi michache iliyopita amefanikiwa kupata mteja baada ya mnada huo kuisha na mwanaume mmoja raia wa Italia kufikia dau la euro 10,000.​


Alina Percea mwenye umri wa miaka 18 aliinadi bikira yake kwenye tovuti moja nchini Ujerumani miezi michache iliyopita.Alina alipanga kuzitumia fedha atakazopata baada ya kuuza bikira yake kwaajili ya kujisomeshea chuo kikuu na kuisaidia familia yake masikini iliyopo nchini Romania.Mnada huo ulifikia tamati siku ya alhamisi kwa Muitaliano mmoja ambaye hakutajwa jina lake kuibuka mshindi katika dakika za mwisho mwisho za mnada huo."Nasubiri kwa hamu, nilifikiri dau lingepanda juu zaidi lakini hata hivyo nina furaha" alisema Alina.Alina aliwasili Mannheim, Ujerumani mwezi januari akitokea kwao Romania na aliamua kuingia kwenye mnada huo baada ya kushindwa kupata kazi.Mnada huo uliingia dosari wiki tatu zilizopita baada ya mwalimu wa shule ya zamani ya Alina kudai kuwa Alina sio bikira.​


Hali hiyo ilipelekea Alina ambaye kabla ya mnada huo alipimwa bikira yake, ilimbidi afanyiwe majaribio kwa mara ya pili kuthibitisha bikira yake.Daktari aliyemfanyia majaribio hayo alitangaza katika kikao na waandishi wa habari kwamba "Alina kweli ni bikira na hajawahi kufanya mapenzi".​


Alina aliamua kuinadi bikira yake baada ya kuona mafanikio aliyoyapata mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan mwenye umri wa miaka 22 ambaye alipata mteja wa bikira yake aliyoinadi kwenye tovuti moja nchini humo aliyefikia dau la dola milioni 3.5." Hakuna mtu aliyeniambia nifanye hivi, ni matakwa yangu binafsi" alisema Alina."Sijui ni lini au wapi nitakutana na mshindi wangu, lakini nafurahia kusafiri iwapo atalipia gharama za usafiri"."Tutaenda hotelini katika wiki chache zijazo na tutatumia usiku mmoja pamoja, na kama tukipendana tunaweza tukakaa pamoja na usiku wa pili"."Tunaweza tukatumia kondomu au kama atafanyiwa vipimo vya magonjwa ya zinaa niko tayari kumeza vidonge vya kuzuia mimba"."Natumaini jamaa ataelewa kuwa mimi ni bikira hivyo atanihudumia vizuri" alimalizia kusema Alina.​


source:FULL SHANGWE
 
Duu, duniani kuna MAMBO. Kuishi kwingi, kuona mengi. Everything ON-SALE now.
 
Ningeileta mimi watu wangesema ooh fiksi unatuzingua haya semeni na hapo sasa...ila mwanangu huyo mtoto kacheza kinoma maana huko bongo watu wanachana hiyo kitu kwa chipsi mayai au bureee kabisa.

Huyu dada atakuwa MJASILIAMALI TU si bure.
 
Ningeileta mimi watu wangesema ooh fiksi unatuzingua haya semeni na hapo sasa...ila mwanangu huyo mtoto kacheza kinoma maana huko bongo watu wanachana hiyo kitu kwa chipsi mayai au bureee kabisa.

Huyu dada atakuwa MJASILIAMALI TU si bure.

Lakini hiyo pia inatupa picha kuwa europe kuna masikini wa kutupwa......kijamii isingekubalika kwetu na hata yeye nadhani angependa akutane na ampendaye..lakini kumuuzia muitaliano, na ninavosikia ni wataalamu wa mambo yetu yale hatataka na ile nyengine kweli??
 
atamueleza nini mume wake? but anyway, watu siku hizi hawaulizii tena...how times have changed
 
By the way...kuna hii hapa...sijui kama mmeiona:
MwanajamiiOne said:
Alina aliamua kuinadi bikira yake baada ya kuona mafanikio aliyoyapata mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan mwenye umri wa miaka 22 ambaye alipata mteja wa bikira yake aliyoinadi kwenye tovuti moja nchini humo aliyefikia dau la dola milioni 3.5.

Hii imetoka leo kuhusu huyu Natalie:

Natalie Dylan's' online virginity auction falls through

By staff writers
The Daily Telegraph
June 01, 2009 12:35pm

0,,6652447,00.jpg
"Natalie Dylan" ... the 22-year-old student who is auctioning her virginity online

A 22-year-old woman who auctioned her virginity online is back on the market after an Australian man who paid to meet her has been banned by his wife.
The 22-year-old California virgin who auctioned off her virtue online for over $4.7 million has yet to meet her winning bidder in the flesh - because his wife won't let him, reports The New York Post.

Natalie Dylan (not her real name) admitted the deal had fallen through.

Last week, she got a phone call from the 38-year-old Australian real-estate businessman, who said he had to back out.

"I told him to go back into marriage therapy," sniped Dylan.

The Aussie cad then sheepishly asked for his $300,000 plus deposit back.
Dylan said no hard feelings; it would be returned.

Now Dylan, who launched the online campaign last spring through the Moonlite Bunny Ranch - a legal brothel in Nevada - is back on the auction block.
Hii imetoka leo. Kakosa dola zake baada ya mke kumtolea nje...hahahaha!
 
Dili akina dada wa Bongo. Wekeni ndimu mkawazingue Jamaa huko unyamwezini hahhahaaaaaaaaaaaaaaaa Ndimu ziko wapi? MwanajamiiOne hapo vipi???
 
Dili akina dada wa Bongo. Wekeni ndimu mkawazingue Jamaa huko unyamwezini hahhahaaaaaaaaaaaaaaaa Ndimu ziko wapi? MwanajamiiOne hapo vipi???
Mh Fugwe hapo chacha pagumu mwenzangu weza umbuka wajitia kuweka ndimu (kama inafanya kazi sijui) afu wajifanya bikira. Ukishajinadi na bei ikafika ukipelekwa kunako mwenzangu ah badala ya kuwa mgeni hukawii kujisahau mara viuno wazungusha weye, unaparamia na kuanza kubusu wewe ah bikra gani huyu mzoefu!!


Mteja atashtuka tu!!
 
Hii ndo capitalistic mentality!! Na thinking outside the box. Huyo aliyepata Euro 10K naona amewahi kukata tamaa. Angepata nyingi zaidi.

Tatizo la hiyo kitu ni publicity iliyozunguka hapo. Lakini kama ingekuwa hakuna publicity lazima angeishia katika mojawapo ya Ikulu za third word countries na angepata mshiko wa nguvu zaidi.

Hao wanaotolewa nje na ma Mrs wao waliingia kwa kubahatisha?? Nadhani kama mkewe hakumpa hiyo kitu, yaani alikuta mke ni bara-bara ya rami, hahitaji kuangalia nyuma. Kama mke ataenda mahakamani akubali yaishe!!
 
wanasema technologically advanced methods of self selling.... kiufupi, ukahaba wa hali ya juu
 
Nami naomba kunadi ubikra wangu. Mi ni mwanaume sijawahi kukutana na mwanamke. Wanawake humu jamvini pandeni dau mniopoe. Siriaz!
 
Nami naomba kunadi ubikra wangu. Mi ni mwanaume sijawahi kukutana na mwanamke. Wanawake humu jamvini pandeni dau mniopoe. Siriaz!

............ Duh asa we unatafuta mengine siriaz!!

Si unajua tena wateja siku hizi wameongezeka na ni wa jinsia tofauti!!
 
Ingekuwa credit crunch haijanipiga ningeenda kubid hii bikira. Kwa dau lililotolewa hapa najua ningeshinda. Halafu ningemwambia binti '' haya sasa hiyo bikira ni mali yangu, tafadhali nitunzie mpaka ukimpata mtu anayetaka kukuoa''. Ningekuwa radhi kulipa ''storage charges''.
Akitokea mtu anayetaka kumuoa binti, ningempa zawadi ya bikira siku ya harusi yao.
 
Ningeileta mimi watu wangesema ooh fiksi unatuzingua haya semeni na hapo sasa...ila mwanangu huyo mtoto kacheza kinoma maana huko bongo watu wanachana hiyo kitu kwa chipsi mayai au bureee kabisa.

Huyu dada atakuwa MJASILIAMALI TU si bure.
hehehehe
tatizo ni kwamba jamii ya bata haiwezi kua kuku asilani
 
Back
Top Bottom