Hatimae jamii forum yanipa mke mwenye sifa zote

Kwanza kabisa poleni na majukumu ya kila siku hasa kwa mnaofanya kaz mpaka mwisho wa wiki.

Nianza na thread yenye kichwa "natafuta mwanamke wakunizalia mtoto kwa mkataba"ambapo nilipata e-mail 3 nilizoziona zinafaa na nikazileta kwenu kupitia kicha hiki"ni mkataba upi unafaa kumpata mtoto wa mkataba kutoka kwa wanawake hawa" hapa pia mlinishaur vizuz.Nilianza kuzifanyia kaz e-mail hiz kama ifuatavyo


1.safari yangu ya kwanza ilikua dodoma ambapo kwenyd majira ya saa tano nilionana na mgeni wangu hotelini,alikua ni bint mrembo aliyevalia suti nyeus na miwani ya jua akiambatana na mwanasheria wake,alinipokea vizur na baada ya kupata kifungua kinywa tulianza mazungumzo yetu

Tliongea mambo meng katika mkataba wetu na hata ivyo tulishindwa kukubaliana katika baadh ya mambo kama
-mimi kuacha kaz idara niliyopo
-mimi kuhamia dodoma kwasababu yeye hawez kuhama
-kufunga ndoa baada ya miez 6 kitu ambacho ni kigumu kwangu kwa mda huo na mambo mengind meng ambayo sintoweza kuyaandika yote.
Napenda kutumia fursa hii kukushukuru m**a**a kwa muda wako na ninaheshimu uamuz wako but hatutoweza kuwa pamoja

2.safar yangu ya pili ilikua katika jiji la mwanza (THE ROCK CITY),na mpaka kufikia majira ya saa moja jioni nilikutana na bint huyo mrembo kiumbo kuliko yule wa kwanza,ila kitu kimoja kilinifanya nisimpende kwasababu alikua amevaa ka-bucta kafupi mfano wa boxer tunazovaa wanaume hivyo kufanya sehemu kubwa ya mwili wake kuwa wazi,viatu alivaa high hills,alijipaka lipbam kwenye kope na lips,kucha za bandia mikononi n.k
kiujumla wanawake kama hawa kwangu binafsi huwa hawanivutii kwani na waona wanaonekana kama pepo/jini.(utanisamehe kwa kutumia neno hilo)
Tulikubaliana kila kitu na alikubali tuwe na mtoto bila malipo na alinielewa kuhusu mkataba wangu katika idara husika niliyokwisha kuielezea.Ni mtoto kutoka katika familia yenye uwezo na alisema anataka ndoa baada ya kujifungua ili aish na mwanamme anayezalisha,alisema anaweza kuudumi ujauzito na hatonitegemea kifedha
pamoja na mambo yote tuliyokubaliana lakini sikuona kama mwil wangu umeonyesha hisia zozote kwake hasa ni kutokana na mavaz yake japo ni bint mrembo,
natumia fursa hii kukushukuru kwa muda wako ila hatutoweza kuwa pamoja *e*m*

3.safari yangu ya tatu ni katika jiji la Dar es salaam na niliingia usiku ilipofika majira ya saa 12 mchana huu nilionana na mgeni wangu kwa mara ya kwanza na pind tulipogonganisha macho wote tulijikuta tukitabasam,kiukwel hisia zangu zilijionyesha kwa bint huyu kwani mnyama wangu alisimama ghafla hivyo niliingia maliwato/msalani kwaajili ya kumtuliza hasa ukitegemea nilikua nimevaa suruali ya kitambaa
Bint huyu alinipeleka mpaka kwenye chumba cha mkutano ndipo nilipo shtuka baada ya kuufungua mlango kwani nilikuta watu wamekaa kwenye meza kubwa mfumo wa pannel kama unapoingia kwenye interview tofaut na nilipokua nikizungumza na wale wengine.
Utambulisho ulianza na kulikua na mwanasheria,mchungaji,sister,kaka wa bint,boss wa bint na mfanyakaz mwenzake.

Katika mazungumzo yetu yaliyochukua saa 1 na nusu,walikubali niwe na bint huyu kama mchumba kabla ya kufunga nae ndoa baada ya mwaka mmoja(walinipa mda huu kwaajili ya kujipanga) na mambo yote yalikua kimaandishi,wakakagua vitambulisho vyangu vyote kuanzia pass ya kusafiria,ID ya chuo,kitambulisho cha kaz na vyote vikaambatanishwa kwenye mkataba,kiukwel hawa jamaa walikua sirious kama mimi nilivyokua.
Baada ya kusainishana nilibaki na bint kwa mda wa nusu saa tukiwa peke yetu na hapa ndipo nilipogundua uzur wa mwanadada huyu mda wote alikua akiangalia chini na kama akiniangalia aliachia tabasam ambalo lilitapakaa kwenye uso wake wote usiopakwa mkorogo kama yule wa mwanza,acha niwe waz blood pressure kwenye mnyama wangu ilikua kubwa sana so mda wote nilikunja nne kuuficha kwa wanaume mnafaham mtu ukivaa suruali ya kitambaa alafu jamaa aamke uone msala wake

Huyu ndio mwanamke atakaekua my one and only,ni kweli kua mke mwema anatoka kwa mungu ila hujui mtakutana nae wap,wengine msikitin,kanisani,chuoni,shuleni,mjini(posta),gengeni n.k ila mimi wa kwangu nimekutana nae kupitia jamii forum.
Boss wa mke wangu mtarajiwa kanipa cd yenye wimbo huu ambao mpaka sasa ndiyo ringtone kwenye cm Yangu
MUNGU IBARIKI JAMII FORUM,MUNGU WABARIKI WANA JAMII FORUM.
Ahsanteni
Duh! Wamekataaaa
 
Na muonea huruma huyo dada aliweka mkataba yeye anatafuta mke mwema wakati yeye mume feki asie na adabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom