wakuu habari za siku nyingi?
atafutae hachoki,baada ya kuzifukuzia kazi za serikali kwa muda mrefu hatimae nimepata kazi huko serikalin kwa Magufuli,nimekua miongoni mwa watanzania wachache tuliochaguliwa ktk nafasi ya economist grade ii katika moja ya wizara nyeti kabisa hapa nchini.so nawasihi tu wale ambao hamjapata kazi bado,msife moyo.Mungu ni mwema,wakati wako ukifika atakuinua tu..
Asanteni kwa Nyote tulioshirikiana kwenye hili jukwaa letu pendwa.
Burigi ndani ndani huko hakuna umeme wala mtandao, huko ni sauti za vindege tu.Mkuu Perry naona hapo wizarani umebanwa sana na majukumu umesahau hata kuja kutusalimia ndugu zako huku. Sijakuona muda mrefu sana.
Hongera sana Perry Nikikumbuka Zile Nafasi za TRA Ulizodondokea Pua Uka panic na kujishaua kuwa una Kazi Nyingine kumbe huna lolote na Sasa unafurahia Kazi ya Economist-Grade II yenye mshahara wa 716,000.
Mungu Akujalie Perry hapa katikati ulipunguza Mdomo na ndo imekua Silaha yako Nakutakia Utumishi Mwema mkuu Maana Umesota sana taangu mwaka 2013 kama Degree zingekua Zina Expire basi ya Kwako Ingekua tayari ilisha expire
Mkuu Hongera sana.