Hati ya Mashtaka dhidi ya CAG Assad: Anachomokaje?


Status
Not open for further replies.
Mama Amon

Mama Amon

Senior Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
179
Points
500
Mama Amon

Mama Amon

Senior Member
Joined Mar 30, 2018
179 500
KANUSHO;

======

UPDSTES: 16 April 2019

Taarifa hii hapa chini imekanushwa. Ofisi ya Bunge imekanusha kuwa Spika Job Ndugai hajaandika barua inayotoa wito kwa CAG, Prof. Mussa Assad kujiuzulu ama kujieleza kwa mwajiri wake kwanini asiadhibiwe. Ofisi hiyo imewatahadharisha wananchi dhidi ya uzushi huo ikisema, ufafanuzi wa azimio dhidi ya CAG ulishatolewa.zaidi soma1555350169028-png.1072282


Magazeti ya leo yamemnukuu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitaja mashtaka yanayomkabili CAG Assad. Ni kama ametaja hati ya mashtaka yenye tuhuma mbili, kama ifuatavyo:

JOB NDUGAI,
SPIKA WA BUNGE,
OFISI YA SPIKA,
DODOMA.

14 APRIL 2019.

PROFESA ASSAD,
CAG WA TANZANIA,
DODOMA.

YAH: WITO WA AMA KUJIUZULU AU KUJIELEZA KWA NINI USIADHIBIWE NA MWAJIRI WAKO

Somo hapo juu lahusika.

Unapatiwa taarifa kwamba, unakabiliwa na tuhuma mbili nzito zifuatazo.

Tuhuma ya kwanza: Huku ukijua kwamba, Bunge ni taasisi inayojumuisha Wabunge, Mawaziri na Rais, ambapo Rais ndiye mwajiri na mteuzi wa CAG; na ukiwa unaelewa kwamba, Hati ya Majukumu ya CAG haisemi kuwa kutathmini utendaji wa taasisi ya Bunge ni kazi mojawapo ya CAG, ulichukua hatua ya kufanya tathmini ya utendaji wa Bunge; na hivyo, kumdharau mteuzi wako kwa kufanya kazi iliyo nje ya majukumu yako uliyokabidhiwa rasmi. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Tuhuma ya pili:
Huku ukijua kwamba, wewe sio msemaji wa ofisi inayohusika na kutathmini utendaji wa Bunge; alibeba jukumu la kuitangazia dunia kwamba, Bunge la Tanzania ni dhaifu kwa mujibu wa tathmini yako; na hivyo kutumia utaratibu wa mawasiliano unaolidhalilisha Bunge mbele ya wapiga kura na Jumuiya ya Kimataifa. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Wito: Hivyo, ndani ya masaa 48 baada ya kupata barua hii, unatakiwa kujitokeza mbele ya Mteuzi wako na kufanya mojawapo kati ya mawili kwa mdomo na kwa maandishi:

(a) ama kujieleza kwa nini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha;

(b) au kujiuzulu mara moja kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha.

Katika kutekeleza wito huu unashauriwa kusoma kwa makini ibara ya 144 ya Katiba ya Tanzania (1977) inayosema yafuatayo:

“144. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii. (3) (a) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi … atateua Tume Maalum… (4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini."

Uelewa wangu kama Spika ni kwamba, kulingana na uzito wa kosa ulilolifanya, na kwa kuwa umekubalia makosa yako hadharani mchana kweupe, mbele ya waandishi wa habari, suala la kukuondoa kazini kwa mujibu wa masharti ya Katiba yetu halihitaji tena kuchunguzwa, na kwa hiyo hakuna sababu ya Rais kuteua Tume Maalum.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

Job Ndugai,
Spika wa Bunge Tanzania.
 
kandamatope

kandamatope

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Messages
247
Points
250
kandamatope

kandamatope

JF-Expert Member
Joined May 19, 2018
247 250
Sentafu ngugai
Winga teleza shavu la kulia mwakyembe
Shavu la kushoto mgogo kabudi
Striker fosi jiwe
Bila kusahau nyanda Tulia
Bench la ufundi yupo katibu wa bunge
CAG pamoja na kupata washangiliaji kibao kutoka timu ya matamko bila vitendo
Muda si mrefu CAG Ataishiwa pumzi kabisa labda aombe poo kwa jiwe akiwasikiliza wapiga kelele bila vitendo jiwe anaweka katiba kando anapita shortcut CAG CHALIII.... anaebisha hainue kidole juu..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Messages
1,107
Points
2,000
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2013
1,107 2,000
Sentafu ngugai
Winga teleza shavu la kulia mwakyembe
Shavu la kushoto mgogo kabudi
Striker fosi jiwe
Bila kusahau nyanda Tulia
Bench la ufundi yupo katibu wa bunge
CAG pamoja na kupata washangiliaji kibao kutoka timu ya matamko bila vitendo
Muda si mrefu CAG Ataishiwa pumzi kabisa labda aombe poo kwa jiwe akiwasikiliza wapiga kelele bila vitendo jiwe anaweka katiba kando anapita shortcut CAG CHALIII.... anaebisha hainue kidole juu..


Sent using Jamii Forums mobile app
Ungependa iwe hivyo kwa maslahi ya Mama Tanzania? Kilangila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
2,034
Points
2,000
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
2,034 2,000
Uelewa wangu kama Spika ni kwamba, kulingana na uzito wa kosa ulilolifanya, suala la kukuondoa kazini kwa mujibu wa masharti ya Katiba yetu halihitaji kuchunguzwa, na kwa hiyo hakuna sababu ya Rais kuteua Tume Maalum.
Huyu ndugai ni mgonjwa wa akili!
Tuseme anamlazimisha rais afanye anavyotaka yeye?

Hapana, ni dhahiri kwamba anafanya kazi aliyotumwa kuifanya.

CAG kujiuzulu siyo njia sahihi. CAG akomae tu wamfukuze kazi. Hapo ataondoka na heshima yake kamili.
 
T

TIBIM

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2017
Messages
7,010
Points
2,000
T

TIBIM

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2017
7,010 2,000
Fupi anapenda sana ligi CAG sio saizi yako anamuona CAG sawa na Mzee au Lema. Fupi ni sawa na pilipili isiyowasha hata machoni..Dhaifu ni neno LA kikaguzi aeleweshwe,sie mwatuita wanyonge na atukasiliki nyie kuitwa dhaifu tu mwarusha ngumu.
 
mkamanga original

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2015
Messages
205
Points
250
Age
40
mkamanga original

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2015
205 250
Uchaguzi umekaribia, wabunge wana stress na nafasi zao, hivyo kipindi hiki tuwaache
 
B

Babeli

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2015
Messages
4,725
Points
2,000
B

Babeli

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2015
4,725 2,000
Ameshindwa kumfutia ubunge lissu sasa anamtafuta CAG, jamaa anapenda sana wenzake wafukuzwe kazi
mnaacha kuangalia.chanzo cha.kosa na.kwanini limetendwa mnakimbilia ku sympasize na.CAG sasa hivi mnamuonea huruma.wakati.mwanzo mlikuwa.mnamshangilia akazidi.kuw jeuri..mmempoteza ndugu yenu..
 
B

Babeli

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2015
Messages
4,725
Points
2,000
B

Babeli

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2015
4,725 2,000
CAG na Ndungai wakae wayaongee haya, wote ni watumishi wa wananchi, hizi drama zinatupotezea muda wa kujadili mambo ya muhimu kwa taifa kama vile matumizi mabaya ya Vote 20.
hahahahaa mmeyaona.yamefika.pabaya ndio.mnaanza kujifanya kutafuta suluhu. mwambieni.CAG ujanja mwingi mbele.kiza..ndio haya.saaa. asiyefunzwa na mamaye ulimwengu humfunza..ndiyo.hayo..
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,284,203
Members 493,978
Posts 30,817,212
Top