Hati ya Mashtaka dhidi ya CAG Assad: Anachomokaje?


Status
Not open for further replies.
Mama Amon

Mama Amon

Senior Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
178
Points
500
Mama Amon

Mama Amon

Senior Member
Joined Mar 30, 2018
178 500
KANUSHO;

======

UPDSTES: 16 April 2019

Taarifa hii hapa chini imekanushwa. Ofisi ya Bunge imekanusha kuwa Spika Job Ndugai hajaandika barua inayotoa wito kwa CAG, Prof. Mussa Assad kujiuzulu ama kujieleza kwa mwajiri wake kwanini asiadhibiwe. Ofisi hiyo imewatahadharisha wananchi dhidi ya uzushi huo ikisema, ufafanuzi wa azimio dhidi ya CAG ulishatolewa.zaidi soma1555350169028-png.1072282


Magazeti ya leo yamemnukuu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitaja mashtaka yanayomkabili CAG Assad. Ni kama ametaja hati ya mashtaka yenye tuhuma mbili, kama ifuatavyo:

JOB NDUGAI,
SPIKA WA BUNGE,
OFISI YA SPIKA,
DODOMA.

14 APRIL 2019.

PROFESA ASSAD,
CAG WA TANZANIA,
DODOMA.

YAH: WITO WA AMA KUJIUZULU AU KUJIELEZA KWA NINI USIADHIBIWE NA MWAJIRI WAKO

Somo hapo juu lahusika.

Unapatiwa taarifa kwamba, unakabiliwa na tuhuma mbili nzito zifuatazo.

Tuhuma ya kwanza: Huku ukijua kwamba, Bunge ni taasisi inayojumuisha Wabunge, Mawaziri na Rais, ambapo Rais ndiye mwajiri na mteuzi wa CAG; na ukiwa unaelewa kwamba, Hati ya Majukumu ya CAG haisemi kuwa kutathmini utendaji wa taasisi ya Bunge ni kazi mojawapo ya CAG, ulichukua hatua ya kufanya tathmini ya utendaji wa Bunge; na hivyo, kumdharau mteuzi wako kwa kufanya kazi iliyo nje ya majukumu yako uliyokabidhiwa rasmi. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Tuhuma ya pili:
Huku ukijua kwamba, wewe sio msemaji wa ofisi inayohusika na kutathmini utendaji wa Bunge; alibeba jukumu la kuitangazia dunia kwamba, Bunge la Tanzania ni dhaifu kwa mujibu wa tathmini yako; na hivyo kutumia utaratibu wa mawasiliano unaolidhalilisha Bunge mbele ya wapiga kura na Jumuiya ya Kimataifa. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Wito: Hivyo, ndani ya masaa 48 baada ya kupata barua hii, unatakiwa kujitokeza mbele ya Mteuzi wako na kufanya mojawapo kati ya mawili kwa mdomo na kwa maandishi:

(a) ama kujieleza kwa nini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha;

(b) au kujiuzulu mara moja kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha.

Katika kutekeleza wito huu unashauriwa kusoma kwa makini ibara ya 144 ya Katiba ya Tanzania (1977) inayosema yafuatayo:

“144. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii. (3) (a) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi … atateua Tume Maalum… (4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini."

Uelewa wangu kama Spika ni kwamba, kulingana na uzito wa kosa ulilolifanya, na kwa kuwa umekubalia makosa yako hadharani mchana kweupe, mbele ya waandishi wa habari, suala la kukuondoa kazini kwa mujibu wa masharti ya Katiba yetu halihitaji tena kuchunguzwa, na kwa hiyo hakuna sababu ya Rais kuteua Tume Maalum.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

Job Ndugai,
Spika wa Bunge Tanzania.
 
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
4,999
Points
2,000
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
4,999 2,000
Pamoja na Ndugai kupewa makavu na hasimu zake,kiukweli jana ule ufafanuzi alioutoa ulikua makini sana ,ngoja nione mwisho wa sakata hili,japo wanasiasa wamepata mtaji
 
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
11,628
Points
2,000
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
11,628 2,000
Hili neno "Sio msemaji" ni dhaifu pia kwa watu wengi ambao huwa wakishindwa kujibu hoja wanakimbilia hili neno, na liko kwetu tu
Unamuuliza Askari kwanini crime zinaongezeka kila kukicha anakujibu eti Mimi sio msemaji seriously?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
18,050
Points
2,000
tindo

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
18,050 2,000
Pamoja na Ndugai kupewa makavu na hasimu zake,kiukweli jana ule ufafanuzi alioutoa ulikua makini sana ,ngoja nione mwisho wa sakata hili,japo wanasiasa wamepata mtaji
Ni hivi, bunge ni dhaifu, na yote hayo yamesababishwa na spika kujipendekeza kwa jiwe. CAG ana support ya umma na hawa wote wanaomgasi CAG akiwemo Spika na jiwe nyuma ya pazia ni wezi wa hela za umma fullstop.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,284,193
Members 493,978
Posts 30,816,726
Top