Hati ya kiwanja kwa watoto chini ya kiaka 18

Hati ya kiwanja kwa watoto chini ya kiaka 18

leiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
661
Reaction score
1,592
Habari ya muda huu ndugu mwanajamii,

Naomba kueleweshwa na anaejua taratibu za kupata hati ya kudumu ya kiwanja alichonunua mzazi akaandika jina langu. Kiwanja kilinunuliwa nikiwa na miaka minne tu, enzi hizo kabla ya uwepo wa NIDA. Miaka 38 baadae, nataka kubadili ile hati ya karatasi ya kulipia kila mwaka kwenda hati ya wizara.

Hatua zote za awali zimeshafanyika ila mkwamo upo mkoani ambapo wanataka mkwanja mrefu kwa stori kuwa ni jambo lisilowezekana kisheria hivyo Kuna namna wanataka kupindisha ili hati itoke.
Swali langu ni je, katika mazingira tajwa napaswa kufanyaje kupata hati bila kutoa rushwa?
 
Mode please edit heading isomeke MIAKA badala ya KIAKA
 
ukiona hadi umefika msimu wa sabasaba na haujapata utatuzi usikose kutembelea banda la ardhi kwenye maonesho ya sabasaba ukiwa na nyaraka zote husika --- kila la kheri
 
Back
Top Bottom