Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

Mwenyewe sina album, huwa nazisevu kwenye inbox yangu ya facebuku akija mgeni naopen anatizamaaa akichoka nalogofu
 
Kuna shida moja ninayoiona, baadhi ya watu kujaribu kuiga maisha ya wengine, mfano kuna baadhi ya watu kupitia taaluma yao huwahitaji sana kufanya hivyo kama waandishi wa habari, wapiga picha, wafanyaji wa biashara kwa njia ya mitandao(hapa wakiwepo wanaojiuza, jinsia zote). Sasa wengine kupiga picha wanajua ndio fashion/mtindo.

Binafsi sioni shida ya mzazi kuweka picha ya mtoto wake/wao kama familia katika mitandao ya jamii(kama kuna haja). Kutegemeana na nchi, maamuzi ya mzazi/mlezi hutumika hasa mtoto anapokuwa hajafika umri wa utu uzima, tatizo kinakuja pale umri wa mzazi ukiwa bado ni mdogo, au pengine mzazi ana umri mkubwa(adult) lakini hakuna (mental maturity).

Sasa hivi, hata vijana wadogo wanazijua simu(ofcourse it's not a crime), lakini nini wanachokutana nacho huko katika simu? Ni picha zisizo na maadili, video mbaya, n.k.

Watoto hujifunza kwa kuona/kusikia..mfano watoto hucheza na kuiga kwa kusema kaka/dada au baba/mama huwa anafanya hivi..au niliona hivi kwenye simu ya kaka/au kwenye TV. Kisha huiga na kufanya mwenyewe. Sasa miaka michache baadaye mtoto "anapoharibika" tunasema 'amelogwa', 'mtoto amenishinda', 'mtoto wangu sijui amekuwaje'.

Hakuna ubaya mtu kuwa katika mitandao ya kijamii, lakini tutegemee nini mtu akiwa huko na malezi yake hayakuwa mazuri! Niliwahi kukutana na baadhi ya watu (mabinti), ambao kila kitu walichokuwa wanafanya lazima wakiandike mtandao.. picha zinapigwa za kuonyesha miili yao, mara wamegeuka, mara wamebinuka n.k Nikajiuliza hii inafanywa ili iweje? Kwani usasa ndiyo huu?

Leo hii unajianika hovyo hovyo na mitindo ya nywele, nguo katika hiyo mitandao kwa njia ya picha, halafu kesho unakuja kuomba kazi?! Then ukikosa kazi ulalamike!

Kuna watu wanashinda mitandao ya jamii, yaani ukimwambia aende shule au umemwagiza anakuwa 'mzembe mzembe' lakini ameamka asubuhi saa kumi na mbili eti yuko busy anapost na kuchat mitandaoni(mf Facebook)!
 
Hauja nishawishi bado juu ya hayo madhara...labda kama unaweka picha za utupu za mtoto...
Otherwise any proud mother or father lazima apende ku show of their 'min me'
 
Hii inatokana na UPUMBAVU na kwa uchache umaskini wa fikra sanjali nakupata mambo kwa kubahatisha...
 
Wacha nionekane enzi za mwalimu.... Sitokaa nipost picha za mwanangu kwenye mitandao ya kijamii.... Labda wapost wengine akiwa kwenye mijumuiko ya watu kama Kanisani, shuleni na sehemu kama hizo...

#Period
 
Acha wapost mimi nafurahiaga ninapotaka kujua kama mtu fulani ana watoto au la ,ana wangapi au aliza na nan I inanirahisishia sana namburuza mtandaoni naoata na majibu papo hapo. Please endeleeni kuweka picha za madogo
 
Juzi nilikuwa nabishana na rafiki yangu mmoja kuhusu dada fulani .je alishaolewa ? Tukainhia mtandaoni tukaona na watoto wake hadi raha
 
niliposoma huu uzi umenifanya nikumbuke na kutakafari jinsi michael jackson hadi sasa jay z na kanye west etc wanavyopambana watoto wao wasipigwe picha na kuwekwa kwenye social netwok
 
niliposoma huu uzi umenifanya nikumbuke na kutakafari jinsi michael jackson hadi sasa jay z na kanye west etc wanavyopambana watoto wao wasipigwe picha na kuwekwa kwenye social netwok

Mmh,kanye hapambani mbona kila siku namuona north kwa wall ya kim. ....labda blue ivy ndo nimemmiss ngoja nikamchek kwenye wall ya mamaake
 
Ukiweka kwenye whasap profile ndio nzuri inachiteka vizuri
 
Mimi na rafiki yangu yupo Marekani * kwenye taasisi ya Elimu lakn mpaka sasa ameshindwa kutupostia picha za wanafunzi wake jinsi wanavyosoma
 
Back
Top Bottom