Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
15,352
Reaction score
24,994
Nianze kwa kukuuliza wewe mzazi; unapoweka picha ya mtoto wako kila hatua tangu akiwa mchanga hadi anaanza kutembea na kuanza shule, alikuomba au ulipata ruhusa yake?

Ingekuwa wewe umepigwa picha bila idhini yako halafu ukaikuta kwenye mtandao utafurahi?

Najua unampenda mtoto wako na ana haki zake za msingi pamoja na kuheshimiwa faragha yake popote alipo. Haiwezekani chochote anachofanya ukiweke kwenye mtandao.

Naomba kueleza madhara yanayoweza kutokea kwa kuweka picha za mtoto wako au wa mwenzako kwenye mitandao hasa mitandao ya kijamii kama facebook , instagram na mingineyo.

Kwanza fahamu kuwa kampuni karibu zote za mitandao ya kijamii zimesajiliwa Marekani, chache zimesajiliwa Ulaya na Asia, lakini karibu zote zinatumia sheria na sera za mataifa hayo.

Katika mataifa hayo wanasisitiza mtoto asijiunge kwenye mitandao ya kijamii hadi atakapofikisha miaka 13, wengine miaka 15 au 16 .

Kampuni zote za mawasiliano zina utaratibu wa kuhifadhi kila kitu kinachotokea kwenye shughuli zao za kila siku kwenye chombo maalumu cha kuhifadhi taarifa za mtandao (server). Kwa hiyo ukiweka picha za mtoto zinahifadhiwa huko hata kama utazifuta.

Hapo awali, nilisema mtoto anahitaji faragha yake, unaporusha picha za mtoto wako kwenye hii mitandao au mawasiliano yoyote, unaingilia faragha yake na huko mbele anaweza kukushtaki wewe au wengine walioingilia faragha yake.

Mtoto anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano .

Umeshawahi kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu kwenye mitandao hasa ya kijamii ? Unajua ni kwa nini?

Kwa sababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na ndugu zake.

Kama ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na mabazazi kwa sababu ya picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja akabakwa.

Kwa hisani ya mwananchi tunapata elimu

Hoja yangu:
Kwanini hii tabia imezuka sana wanandoa siku hiyo hiyo mama anaugulia maumivu badala ya baba kumhangaikia mama na mwanae yeye anafuta kamera iko wapi tena siku hizi mchina amerahisisha anamfotoa mtoto na kupost kwenye wall yake ili iweje? kwamba watu wajue na wewe ni kudume cha mbegu au una kizazi? matokeo yake ndo wazazi mnapotofautiana na marafiki zenu mnawatukana mpaka watoto, kuna wengne sijui mtandao gani yule dada anauza pichu anamtukana mtoto wa mwenzaje eti baboon hivi mnahisi watoto wanajisikiaje? unamharibia mtoto future yake bila kujua, ukifikiri ni fahari kuweka picha ya mwanao sijui facebook, twitter, instagarma na kwingne huko ni ushamba na ujinga, labda siku hizi kwa kuwa imekuwa issue sana kupata mtoto but is not fair

Nawasilisha hoja
 
Duh.
Kweli Mkuu siku hizi mtu mko nyumba moja badala ya kumsalimia hapo unakwenda Facebook unampa salam
Mtu na Mkewe badala ya kusifiana nyumbani wanakwenda Facebook, umependeza.

Hii ni shidaaa kweli. hasa miaka hii
 
Hahahahahaaa unaenda kumsifia facebook wakati umemuacha ndani, kumbe hata akipika chakula kitamu unaenda kumsifia facebook kwa faida ya nani? na ukichapiwa wa kumlaumu nani wakti umemsifia mwenyewe, na wakikorofishana hapo sisemi
 
Mutoto yangu sio jambazi wala mimi si fisadi kwanini nisijiachie nq chibebi changu kwa raha zote?

Afu umesahau mzazi ni trustee wa mtoto? only atakua charged kwa act alioifanya without good faith.
.....

Wazazi mafisadi na watoto wote wenye element za uhalifu hawastahili kutupia/kutupiwa mitandaoni kwa photo.
 
Mkuu, kule ni shida kila mtu anachofanya anaweka Facebook hadi unashangaa. Mimi nawe tuko pamoja lakini Tunakwenda kuongelea eti kwenye mtandao
Suala la picha hilo ndiyo aibu unakuta sasa hivi
kuna hii Mitandao iliyosema Facebook bure
sasa Mtu anakwambia niunge Facebook

Nenda Kariakoo pale sasa utacheka mpaka Mtu anakuja na simu anaungiwa huduma asiyoijua.
 
Duh.
Kweli Mkuu siku hizi mtu mko nyumba moja badala ya kumsalimia hapo unakwenda Facebook unampa salam
Mtu na Mkewe badala ya kusifiana nyumbani wanakwenda Facebook, umependeza.

Hii ni shidaaa kweli. hasa miaka hii
Halafu ingependeza kama ungeanza na kutusalimia ingawa umenipita pale njiani..
 
Fb tunaita uwanja wa fujo kila kitu cha mtu utapata kule kuna kichekesho nilikutana nacho bint mmoja ka post kabati La nguo, mhhhhhh sasa weekend imeanza subiri uone
 
Mutoto yangu sio jambazi wala mimi si fisadi kwanini nisijiachie nq chibebi changu kwa raha zote?

Afu umesahau mzazi ni trustee wa mtoto? only atakua charged kwa act alioifanya without good faith.
.....

Wazazi mafisadi na watoto wote wenye element za uhalifu hawastahili kutupia/kutupiwa mitandaoni kwa photo.
Najua utajisikia vizuri sana endapo utaambiwa mtoto wako ni mzuri au ni handsome boy, akiambiwa ni baboon utaelewa nii nasema, wanawake wengi wamejikuta katika mazingira magumu kwa kupost picha huko kwenye mitandao wengine tumeambia wamebakwa na wengine kuuawa hao ni watu wazima na walipost kwa hiari yao je akija kufanyiwa mtoto ambaye picha yake umepost wewe mtandaoni kwa kuwa ameumbika huko kuumbika kukamletea matatizo na akigundua kwamba hao waliomletea matatizo waliikuta picha facebook na aliyeweka huko ni baba yake au mama yake hiyo kwako unaiangaliaje? na hapa siongelei mafisadi kama unaowasema wewe
 
Fb tunaita uwanja wa fujo kila kitu cha mtu utapata kule kuna kichekesho nilikutana nacho bint mmoja ka post kabati La nguo, mhhhhhh sasa weekend imeanza subiri uone
Kuna post moja humu iko jukwaa la habari mchanganyiko yule dada anauza nguo za ndani vyupi vya wanawake na ana blog yake sijui anaitwa nani nimemsahau walikuwa wanatukanana na mwenzake yeye kamtukania mtoto wake na kumuita baboon unafikir mtoto alijisikiaje? hata kama ni mkubwa kiumri hii mitandaoo, wengine wanafua group la family wasapu ili wadiscus mambo ya familia mwisho wake ni umbea na usengenyaji hii mitandao imekuja kubomoa familia
 
Nimekutana nayo mkuu siku hizi kila kitu ni open mtu unamjua kwa fb tu post zake hayo magroup ndio kila kona hadi yanatumalizia charge from no where coz mtu anakujua na ana namba yako bac anakuunganisha
 
Fb tunaita uwanja wa fujo kila kitu cha mtu utapata kule kuna kichekesho nilikutana nacho bint mmoja ka post kabati La nguo, mhhhhhh sasa weekend imeanza subiri uone

hahahaha kabati languo ? kweli hajitambui
 
Mutoto yangu sio jambazi wala mimi si fisadi kwanini nisijiachie nq chibebi changu kwa raha zote?

Afu umesahau mzazi ni trustee wa mtoto? only atakua charged kwa act alioifanya without good faith.
.....

Wazazi mafisadi na watoto wote wenye element za uhalifu hawastahili kutupia/kutupiwa mitandaoni kwa photo.

hujamuelewa mtoa mada..!
yakija kukukuta ndo utaelewa anamaanisha nini..!
 
Najua utajisikia vizuri sana endapo utaambiwa mtoto wako ni mzuri au ni handsome boy, akiambiwa ni baboon utaelewa nii nasema, wanawake wengi wamejikuta katika mazingira magumu kwa kupost picha huko kwenye mitandao wengine tumeambia wamebakwa na wengine kuuawa hao ni watu wazima na walipost kwa hiari yao je akija kufanyiwa mtoto ambaye picha yake umepost wewe mtandaoni kwa kuwa ameumbika huko kuumbika kukamletea matatizo na akigundua kwamba hao waliomletea matatizo waliikuta picha facebook na aliyeweka huko ni baba yake au mama yake hiyo kwako unaiangaliaje? na hapa siongelei mafisadi kama unaowasema wewe

Nakupata vyema mdau.

After olu ukimuona mtu anambandika mwanae mitandaoni hovyo hovyo kisa mtoto huyo ni mzuri, mzazi huyo akapimwe akili. I know and i believe watu wanaosumbuliwa na ASD ndio wanakuaga na hiyo tabia.

My point ni kwamba si kila kubandika picha ya mtoto ni tatizo. na hapa ndipo nnapotofautiana na wewe.

As a general rule haifai kubandikq picha za mtoto mitandaoni. nachotaka uelewe ni kwamba there is no general rule without exceptions!

WHAT DO YOU THINK?
 
Baraza La wa Wakilisha znz (BLW)

Sijui na ninyi mnawasaidia ninyi rafiki zenu maana hatuoni hata mnachokifanya mpo tu sijui mnaogopana kwenye vibaraza vyenu vya kahawa pale mlandenge, malindi, mtendeni hua mnaongea mengi lkn mkikaa me ndani hamsemi kitu

Hebu na ninyi fanyeni uchunguzi wa serikali na matumizi ya hela za wananchi hali znzibar ni mbaya
 
Vipi tena mkuu bado una hangover za escroo
 
Back
Top Bottom