"hatari ya mwaka 2016!"

Free Again

Senior Member
Dec 20, 2015
114
93
Ashukuriwe Mungu aliye tupa neema hii ya kuumaliza mwaka 2015, na sasa zimebaki siku chache kabla hatujaingia 2016!
Mwito wangu kwako mwana JF, fanya kila uwezalo kuwasamehe waliokukosea,kukuudhi au kukukwaza kwa namna moja au nyingine.lakini pia Mungu akupe wepesi wa kuomba msamaha kwa uliowakosea kwa namna yoyote ile! "TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE"
Kushindwa kusamehe na kubeba uchungu moyoni,ni hatari kwa afya na roho yako! Na istoshe unayekuwa na mzigo ni wewe na si yule aliyekukosa;sasa kwa nini usimwachilie tu?
Lakini pia na wewe kama umemfanyia mtu kosa au makosa,upo hatarini maana upo kwenye kifungo , kwanini usimuomba msamaha tu? Hutapungukiwa,hutaonekana mjinga,zaidi utaonekana mwenye hekima,myenyekevu na mwenye upendo na ndivyo ilivyo.
CHUKI/KUTOKUSAMEHE NI KIKWAZO CHA MAENDELEO,KIROHO NA KIMWILI.
Mungu akupe wepesi wa kisema "nisamehe" kwani ni hatari kuingia na uchungu 2016. Mungu awabariki na tuzidi kupendana!
 
Back
Top Bottom