Hatari ya anga za juu: Kuna vyombo vingine vinavyotishia maisha ya binadamu katika anga za juu vinavyoweza kuangukia dunia wakati wowote

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,616
32,723

Hatari ya anga za juu:Kuna vyombo vingine vinavyotishia maisha ya binadamu katika anga za juu vinavyoweza kuangukia dunia wakati wowote​

mABOMU YA MUDA
Ulimwengu haupo salama. Licha ya kuanguka kwa njia salama kwa roketi ya China kutoka anga za juu na kuwapa watu wengi afueni, bado kuna hatari kwani kuna zaidi ya vifaa na roketi za aina mbali mbali katika anga za juu ambazo zilipelekwa huko na nchi nyingi wakati wa programu za kufanya tafiti katika anga za mbali.

Maelfu ya vitu vilivyotengenezwa na wanadamu huzunguka dunia na vingi havifanyi kazi tena.
Kuna hatari uchafu huu katika anga za juu unaweza kugongana na satelaiti zinazofanya kazi, ambazo hutoa huduma muhimu kama GPS na onyo za hali ya hewa.

roketi
Kufuatilia na kutabiri tabia ya vyombo hivyo , Prof Moriba Jah na wenzake waliunda AstriaGraph - ramani ya karibu ya wakati halisi ambapo kila kitu katika anga za mbali kinafuatiliwa.

Anaelezea kuwa mfumo huo unafuatilia karibu vyombo 200 ambavyo ni kama mabomu ya muda yanayohatarisha maisha ya binadamu.
Vyombo hivyo ambavyo ni pamoja na roketi kadhaa vinaweza kuvunjika wakati wowote au kuzigonga setilaiti muhimu na kuvuruga kabisa maisha ya binadamu kando na kuangukia watu au hata miundo msingi muhimu kwa maisha yetu ya kila siku.

Prof Moriba anasema vyombo hivyo ni vingi sana na kunavyo takribani idadi ya vyombo 26,000 vyenye ukubwa mbalimbali kama vinavyolingana na simu za mkononi hadi vikubwa kama kituo cha Anga za juu cha kimataifa/ISS.

Vyombo hivyo vimekuwa katika anga za mbali kwa miongo kadhaa na nchi nyingi zilizovipeleka juu haziko tayari kugharamika kuviondoa kwa njia salama .

Hatari kwa binadamu​

Hofu kubwa kwa binadamu ni kwamba, wakati wowote ambao huenda hautajulikana na wengi ni uwezekano wa mojawapo ya vyombo hivyo katika anga za mbali kuanguka dunuani katika sehemu yenye watu wengi na kusababisha maafa.

Pia kuna hatari ambayo watafiti wanazidi kuifanyia uchunguzi ya matokeo ya chombo kimoja kuanguka na kuvigonga vyombo vingine hatua ambayo huenda ikasababisha hatari zaidi ya janga kubwa la vyumba vilivyochanika 'vikinyesha' kama mvua kutoka angani .

Hakuna kinga ambayo itaweza kutumika kuwazuia binadamu kujeruhiwa au hata kuuawa na hatari kama hiyo kwa sababu itakuwa vigumu hata kwa nchi zenye mifumo ya makombora kujikinga. Haitawezekana kwa kombora kutumiwa dhidi ya vifaa vikubwa ambavyo huenda vikakatika na kuwa vipande vidogo vidogo .

Uwezekano wa Kuanguka​

Swali la kuanguka kwa Chombo cha China kiliwaacha watu wengi wakijiuliza, je nini kingetokea kama mabaki hayo yasingeliangukia kwenye bahari?

Nini kingetokea katika ardhi na je China ingelipa fidia? Bila shaka kama mabaki ya roketi hiyo yangelianguka katika eneo la makaazi ya watu kungelikuwa na athari kubwa kwa uhai wa watu na mali zao.

Ifahamike kuwa si kosa katika sheria za kimataifa kwa vyombo vya safari za anga za juu kuangusha uchafu ama mabaki duniani, lakini hilo ni suala la kimaadili ambalo nchi nyingi wamekuwa wakilitilia mkazo ili kufanya dunia kuwa eneo salama lisiloathiriwa na shughuli za anga za mbali.

Kuhusu fidia na namna ya kushughulikia ajali kama hiyo, kuna mikataba miwili ya kimataifa ambayo ilipitishwa mwaka 1967 na mwaka 1972 ambayo inatoa muongozo wa nini cha kufanyika.

Mkataba wa mwaka 1972 ni juu ya dhima za nchi ambazo zinafanya shughuli katika anga za mbali pale endapo kuna jambo lolote litatokea kupitia vifaa vyake.

Nchi mbalimbali za Ulaya, Malekani na hata China zimetia saini mkataba huo. Kukubali dhima haimaanishi kuwa nchi imevunja sheria, bali inatambua wajibu wake wa kimaadili kwa kile kilichotokea na ipo tayari kushughulika janga ama ajali hiyo.

Takriban miaka 43 iliyopita, Canada ilitumia vifungu vya mkataba huo kuiwajibisha nchi ya Umoja wa Kisovieti (Urusi ya sasa).

roketi
Mwaka 1978, satelaiti ya Usovieti Kosmos 954 ilipata hitilafu ikiwa katika anga za juu na mabaki yake kuangukia katika eneo la kaskazini magharibi ya Canada, na kusambaza taka za sumu ardhini.

Awali Usovieti ilijaribu kukanusha kuwa satelaiti hiyo haikuwa yao lakini baada ya majadiliano wakakubali kulipa Dola milioni 6 za Canada. Hakuna ushahidi kama kiasi hicho kililipwa chote.

Hofu ya kuanguka kwa vyombo vingine vilivyopo angani sasa itazidishwa na ufichuzi huo kwamba kunavyo vingine 200 ambavyo wakati wowote vinaweza kugongwa na kuanguka vikiwa vipande au hata kugonga setilaiti muhimu kwa shughuli za maisha ya binadamu katika sayari yetu.

Je,ishawahi kutokea kifaa kuanguka?​

Mwezi Machi mwaka huu, sehemu ya roketi ya Marekani ya mradi wa Space X ilianguka karibu na makaazi ya watu.
Sehemu ya mabaki hayo ilianguka katika shamba huko Washington baada ya roketi hiyo kushindwa kurejea duniani kwa utaratibu sahihi.

Mabaki makubwa zaidi ya chombo cha juu cha Marekani yalianguka mwaka 1979. Nchi nyingi duniani kuanzia Ulaya mpaka Asia zilikuwa katika hali ya hofu juu ya madhara yake endapo mabaki yangeangukia katika maeneo yao.

Hatimaye tani 77 zilianguka baharini karibu na Australia. Mabaki ya chombo hicho yalitapakaa katika eneo la kilomita takribani 7,400 baharini, hali iliyomlazimu Rais wa Marekani wa wakati huo Jimmy Carter kuomba radhi.
 
Mkuu tupe hii taarifa ya "jua kutanuka" please.
Tukio la "Jua kutanuka" ni tukio linaloambatana na tukio jingine linalofahamika kama The End of the Sun.

Kulingana na studies zilizopo, Jua lilizaliwa, linaishi na ipo siku litakufa. Lakini kabla ya hapo, litapitia hatua ya kutanuka kwanza. Hii hatua ya kutanuka inafahamika kama "Red Giant Phase".

Wakati litakapokuwa likitanuka, litazimeza sayari za karibu ikiwemo dunia yetu.

Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu hili, tafuta somo la astronomy kuhusu The End of the Sun ama Red Giant Phase of the Sun.
 
Back
Top Bottom