Ndege isiyo na rubani ya Iran yazifukuza ndege za Marekani katika anga ya Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Ndege isiyo na rubani ya Iran yazifukuza ndege za Marekani katika anga ya Iran

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Iran amesema ndege isiyo na rubani ya Karrar imezionya mara kadhaa ndege za ujasusi za Marekani na ndege nyingine za kigeni na kuzitaka kuwa mbali na anga ya Iran.

Brigedia Jenerali Alireza Elhami alisema jana Jumapili kwamba ndege hiyo isiyo na rubani mara kadhaa imezilazimisha ndege za kigeni zenye watu na zisizo na rubani kubadili mkondo wao kwenye Ghuba ya Uajemi, Mlango Bahari wa Hormuz, na Bahari ya Oman.

Kamanda huyo amesema, baadhi ya ndege za kijeshi za kigeni zilitaka kujaribu uwezo wa ulinzi wa anga wa Iran kwa kubadilisha mwinuko wa safiri zao, bila kujua kwamba Karrar, ambayo imetengenezwa kikamilifu na wataalamu wa ndani, inaweza kuruka juu yao.

Elhami pia amebainisha kuwa Karrar imewekewa mfumo wa kisasa wa rada.

Droni ya Karrar, iliyotengenezwa na Kampuni ya Viwanda ya Kutengeneza Ndege ya Iran (HESA), ni miongoni mwa kizazi kipya cha zana za anga za jeshi la Jamhuri ya Kiislamu iliyoundwa kuzuia vyombo vinavyoruka vya maadui kuingia katika anga ya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amekuwa akitoa wito wa kufanyika juhudi kubwa za kudumisha na kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa Iran.

4c3p47ecd5dea12cuu5_800C450.jpg
 
Kusema kweli Ile ya ndani ya moyo,jamani wamarekani ni wachokozi.
 
Nguvu za kusaka sare za kijeshi mitaani?
Kagame kafyatishwa

Maharamia na magaidi wa Kibiti wametokomezwa

Mapinduzi ya Burundi yalizimwa na Rais akarudishwa madarakani ndani ya saa 24

Commoro Jeshi lilipindua utawala wa Kiraia likaondolewa madarakani

Congo M23 Walitokomezwa

hivi hizi role zingefanywa na Majeshi mengine msingesifia ?

Tutajieni hata Jeshi moja Barani Afrika lililofanya role kubwa ya kudumisha Amani nchini mwake na kufanya role kubwa maeneo mengine kama JWTZ?

tena hii mifano yote hapo juu ni mifano ya karibuni kabisa …sijakumbushia ya enzi za ukombozi
 
Kagame kafyatishwa

Maharamia na magaidi wa Kibiti wametokomezwa

Mapinduzi ya Burundi yalizimwa na Rais akarudishwa madarakani ndani ya saa 24

Commoro Jeshi lilipindua utawala wa Kiraia likaondolewa madarakani

Congo M23 Walitokomezwa

hivi hizi role zingefanywa na Majeshi mengine msingesifia ?

tena hii mifano yote hapo juu ni mifano ya karibuni kabisa …sijakumbushia ya enzi za ukombozi
😳😳😲😲
 
Nakubaruana mkuu
Nguvu ya jeshi haipimwi kwa idadi y drone

inapimwa kwa uwezo wake wa kudumisha amani na usalama ndani na kwny Mipaka y Nchi yake

Nchi zote zinazotuzunguka zinachoko choko na mitafaruku ya kisiasa kasoro Tanzania msidhan ni mambo ya bahati mbaya
🙏🙏
 
Back
Top Bottom