Hatari niliyoiona mlima Iwambi - Mbalizi MBEYA

Ila ule mteremko toka kawetere kuitafuta mbeya,ile njia ingekua ina magari mengi kama mbeya To tunduma ingeua sana
 
Mawazo yako yanachukukiwa naamini watayafanyia kazi lkn nakushauri tena mkuu endelea na usichoke kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara wabadilike watumie barabara kwa nidhamu ili tupunguze ajali zinazoweza kuzuilika hasa hao waendesha gari za abiria maana umekiri mwenyewe wakiruhusiwa kwa awamu wanafukuzana na kusababisha ajali zinazoweza kuzuilika
Hawawezi kuelewa.
Dawa ni abiria kupambana.

Mimi nikishapanda daladala halafu dereva akaanza kufanya ligi za kijinga namwambia anishushe.
 
Wajenge tu.
Magari makubwa kila baada ya siku kadhaa unakuta limefeli break.

Mimi hiyo mitaa nashinda sana huko,ajali nyingi nazishuhudia.
Yaani pale kabla ya kufika relini unaposhuka Mbalizi ,lile korongo,tunapita tu kishujaa maana hatuna namna.

Wenye mamlaka waliangalie hilo.
Na pale ndio mauwaji point aisee
 
Ule mlima ni hatari sana.....ina maana serikali sikivu imeshindwa hata kujenga balcony pembeni mwa ule mlima.....???

Mbalizi umenikumbusha mbali sana.....mitaa ya DDC Kyle juu.....
 
e3f6024edcfb31c65b690be5afce7c9b.jpg
 
Na pale ndio mauwaji point aisee
Mwaka fulani jirani yangu mtaani ambaye alikuwa dereva alimwaga kadaladala kote korongoni.Walikufa karibia wote akiwepo yeye mwenyewe.

Yaani barabara ipo karibu na korongo,na pembeni hakuna japo vizuizi.
 
Kijana wangu juzi amenusurika kifo hapo Iwambi wao walikuwa kwenye hiece anatoka kibaruani wakagongwa kwa nyuma gari ikaingia mtaroni kwa bahati hakuna alie umia kimbembe kilikuwa kwa hizo Coster ki ukweli ilikuwa ajali mbaya na watu wengi walipoteza maisha
 
Ule utaratibu wa magari kupita kwa awamu niliwahi sema mimi humu kuwa unatengeneza balaa jingine.

Unakuta gari ndogo zinaruhusiwa kuanza kupanda mlima/kushuka wakati magari Makubwa bado hayajamaluzika.

Speed ya lori ni ndogo,ukilinganisha na daladala.
Wao wanaruhusu bila kujali utofauti wa speed,, matokeo yake sasa ni ajali kama iliyotokea Jana.

Madereva wa daladala nao ni vichaa.
Wakisharuhusiwa wanaanza kufukuzana hovyo, overtake bila tahadhari ili mradi awe wa kwanza kubeba abiria Iwambi.
Huu mchezo dereva wa daladala ameucheza Jana na umegharimu maisha ya watu wengi.
Walioona Jana jioni ile ajali inatisha.
Yote hiyo ni uroho wa kuwahi abiria Iwambi..gari inakimbia na kuovertake kwa kasi bila kujali,malori yanayoshuka yalikuwa hayajaisha.
 
Back
Top Bottom