mzee wa kasumba
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 1,432
- 2,892
Kwa ambao wamebahatika kupita barabara hii ya Dar - Tunduma, ukitoka Mbeya kama unaelekea Mji mdogo wa Mbalizi kuna mahala huitwa IWAMBI.
Hapa unakutana na mteremko mkali sana ambao unashuka nao hadi mjini Mbalizi.
Ajali zimekuwa nyingi hususan kufeli breki kwa magari makubwa, kuacha njia na kuingia korongoni, ajali za kugongana uso kwa uso n.k.
Mamlaka zimeliona hilo na kulidhibiti katika mtindo huu ;-
Kwamba kwa sasa magari makubwa (ya mizigo) na mabasi madogo (daladala) hupeana zamu kupita eneo hilo kupanda na kushuka.
Yaani kuna muda yanaruhusiwa magari makubwa tu, na kuna muda huruhusiwa dala dala.
SHARAUTI sana kwa mamlaka husika.
ILA
Mtihani upo kwa madereva hawa wa daladala. Yaani muda wa kuruhusiwa kwao ukifika inakuwa ni fujo + wenge kiasi kwamba panaweza kusababishwa ajali nyingine baina yao wenyewe ama hata kwa watembea kwa miguu hasa wanaovuka vivukoni.
Yaani lile suala la kuachiwa kila mtu anataka kuwa wa kwanza kuwahi abiria kituo cha mbele, basi inakuwa tafarani.
Naiomba mamlaka nayo iliangalie hili, ingawa unaweza kuona ni la kawaida, ila madhara yanaweza kutokea hapo mbeleni.
Na huu ndio mwisho wa taarifa ya habari kutoka KASUMBA FM.