Hatari Mlima Kitonga!

Hatari Mlima Kitonga!

Kassim Awadh

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
884
Reaction score
187
Wakuu siku si nyingi nimepita njia hii Dar-Tunduma,eneo la Kitonga vibao vyote vya alama za barabarani vilivyokuwa vinaonyesha na kuhadharisha hali ya barabara kama,kona kali nk vimeondolewa/ibwa.

Naiona hatari inayokuja kwa madereva wageni wa njia kupata matatizo kwa kukosekana alama za tahadhari eneo hilo lenye mteremko mkali. Ni biashara ya chuma chakavu? Tanroads mkoa Iringa mpo?
 
kwa jinsi kitonga ilivyo hamna haja ya vibao coz yenyewe inajionyesha ni hatari.
 
...pale mahala panatisha sana.
 
Hatari sana hiyo,tanroads iringa wangechukua hatua za haraka

Jambo moja huwa nashangaa,,watendaji hawa wana vitendea kazi vyote mpaka gari VX la meneja mkoa tanroads kumwezesha kutembelea barabara zote chini yake lkn wap! mpaka yatokee madhara ndo wanastuka! Huwa nakumbuka hata shimo lililosababisha ajali ya Dr mwakyembe mlima Ihemi,mara baada ya ajali lilizibwa fasta!
 
Tuangalie pande zote, ikiwa kila Tanroad wakiweka alama vibao vinaondolewa, vinaibwa, wafanye nini?
Tuchangie na mawazo mbadala ya kukomesha wizi pia.
 
Tuangalie pande zote, ikiwa kila Tanroad wakiweka alama vibao vinaondolewa, vinaibwa, wafanye nini?
Tuchangie na mawazo mbadala ya kukomesha wizi pia.

...labda viwekwe vya plastiki.
 
Badala ya kuweka vya chuma Waweke vya Zege.
Yaah! Hapo umeongea. Nimeona mhandisi aliyejenga barabara ya tabora- shinyanga-mwanza kaweka vya zege na vimedumu hadi leo. So nadhani itasaidia sana
 
Yaah! Hapo umeongea. Nimeona mhandisi aliyejenga barabara ya tabora- shinyanga-mwanza kaweka vya zege na vimedumu hadi leo. So nadhani itasaidia sana

Wa-Tz sisi wajinga sana kwa kila eneo yaani hatufai! Hivi navyo mkuu wanabandua vile vibati wanapeleka kwenye vyuma chakavu. Nzega-Shy-Mza zimebaki nguzo nyingi sana hazina alama hasa eneo la mkoa wa Shinyanga. Tanroads waweke sheria kali ikipotea alama 1 tu wenye viwanda vya nondo eneo hilo wanalipishwa hao ndo wanavnunua
 
Hii biashara ya vyuma chakavu na uharibifu wa makusudi wa mali za umma (mara nyengine kwa uharibifu tu kama vile kung'oa vibanda vya simu na posta), uko sehemu nyingi ulimwenguni ambako hakuna sheria au zikiweko hazitekelezwi.

Tatizo ni hilo la kutokuwa imara na sheria zetu. Bado nakumbuka kesi ya mtoto wa Kimarekani aliyekamatwa anatema ubani barabarani Singapore, ambapo adhabu yake ni viboko. Rais Clinton alipoingilia kati kumtetea raia wake walimwambia, hii ndio sheria yetu, hata wewe ukija ukafanyanya hivyo hivyo tutakuchapa. Kwa ufupi, tuwe na sheria kali na tuzitekeleze, ili mtu afikiri mara 100 kabla hajafanya ujinga wake.
 
Na ile lami ilivyotandikwa kama mkeka! Kwa kweli nahofia speed zaidi. Heko kwa wale polisi wanaovizia pale kati na tochi yao, mweh!
 
Back
Top Bottom