Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 15,758
- 15,361
HATARI KUBWA KWA USTAWI WA TAIFA
Heading inasomeka na inaeleweka. Tangazo la hatari huvuta hisia za wengi kama si wote, Kuna suala ambalo kwa kipindi kirefu nimekuwa nalifuatilia halafu nakosa majibu.
Juzi kati (I mean last week) Rafiki yangu alimpeleka mkewe kipenzi ktk chumba cha operesheni kuondoa uvimbe kwenye tumbo la uzazi. Ilinisikitisha ingawa aliyefanyiwa operesheni alikuwa anakaribia au amefikia umri wa kutopevusha yai la uzazi.
Miaka minne iliyopita ilikuwa mama yangu mzazi na katika miaka mitatu iliyopita nimeshuhudia wanawake ninaowafahamu wapatao tisa wakitolewa uvimbe katika tumbo la uzazi, operesheni hizi mara nyingi husababisha kuondolewa au kufungwa kwa uzazi kabisa.
Nakumbuka shuga mami wangu mmoja alitamani kunizalia mtoto (miaka sita iliyopita) ila kabla hajatimiza azma yake alipitishwa chumba cha upasuaji na kuondolewa kizazi, kisa kilikuwa ni uvimbe ndani ya kizazi.
USHAHIDI
Nilijaribu kumuuliza rafiki yangu mmoja miaka iliyopita ambaye ni mtaaluma wa udaktari, alinifafanulia kuwa tatizo la uvimbe katika tumbo la uzazi limekuwa likiwaandama wanawake hususani waliokwisha kujifungua au wale ambao wamechelewa kudevelop zygote (kushika mimba).
Ila kali ya mwaka ni mwezi uliopita ambapo rafiki wa mke wangu ambaye wanasoma wote chuo kikuu kimoja hapa nchini alipata zahama la operesheni ya kuondoa uvimbe ktk kizazi.
Tatizo lake lilianza na dalili ambazo wanawake wote ninaowafahamu waliopitia kisu cha kuchanja uvimbe walizipata. Dalili za homa na kuumwa tumbo ni dalili ambazo nazielezea hapa, mimi siyo mtaalam wa tiba wala masuala ya afya hivyo sidhani kama niko sahihi sana kuhusu dalili.
Msichana huyu (rafiki wa mke wangu) alipelekwa hospitali baada ya kuzidiwa na vipimo vyoote vikachukuliwa akagunduliwa kuwa ana uvimbe ktk kizazi chake.
Kwa kuwa umri wake ulikuwa ni mdogo I mean ndiyo kwanza anafikisha miaka ishirini, madaktari walianza kumtuhumu kuwa aliwahi kutoa mimba hapo awali, ukweli ni kwamba binti mwenyewe ni bikira na hajawahi kupandwa mbegu na mume yeyote hivyo ilimshangaza sana yeye na wazazi wake kwa kukutwa na hali hiyo ambayo imezoeleka kwa aina Fulani ya class ya wanawake, yaani waliokwisha kuzaa au waliochelewa kushika mimba.
Alifanyiwa operesheni ya kuondoa uvimbe ule na hivi sasa anaendelea vyema kupata nafuu, bahati ilikuwa upande wake kwani kizazi kimenusurika kunyofolewa. Na yule mke wa rafiki yangu ambaye ni mwanabodi mwenzetu humu anaendelea vyema baada ya kufanyiwa operesheni ya kutoa uvimbe katika kizazi chake.
Na pia leo hii chuoni pale lecture room niliwauliza wanachuo wenzangu kuwa endapo wanafahamu au kumfahamu mtu (mwanamke) yeyote ambaye amewahi kupata matatizo ya uvimbe katika kizazi, karibu darasa zima walikiri kuwa walishahusika katika kesi hii ya uvimbe, ingawa walinishangaa wakidhani labda nitatoa solution, ila nilifanya hivyo just kuweza kujenga hoja yangu hii na kuiweka JF ambapo we dare to talk openly.
HATARI YENYEWE
Hatari ninayoiona hapa ni namna ambavyo tatizo hili linakua kwa kasi, ninadhani kuwa labda hata wewe unaweza ukawa unawafahamu wanawake kadhaa ambao walipitia chumba cha upasuaji kuondoa uvimbe katika kizazi. Ninapata shaka sana kwa ukuaji wa kasi wa tatizo hili, nimejiuliza maswali mengi bila majibu,
• Je ni matokeo ya matumizi ya madawa ya uzazi?? (lakini wengine waliofanyiwa upasuaji hawajawahi kutumia hizo dawa)
• Je ni matokeo ya matumizi ya vyakula au bidhaa zilizokwisha muda?
I mean labda ni chakula kilichopita muda wake dukani, au cosmetics zilizokwisha muda, au juices na aina ya vinywaji ambavyo havina ubora utakiwayo (naamini wengi humu wanafahamu kuwa juice aina ya delmonte ya box huwa ina kawaida ya kuumuka ktk mazingira ya joto).
• Vipi kuhusu junk food? (sasa hivi chakula kikuu cha wabongo ni likely to chips-yai au kuku)
• Je inawezekana haya magari tunayonunua (mitumba) kutoka Dubai ambapo yanakuwa yanatoa moshi mchafu kwa ozone na ozone za matumbo ya kina mama?
•
Au inawezekana ni mpango madhubuti kwa malengo madhubuti ya jamii iliyozoea kuexploit kutumia mbinu hii chafu ili iweze ku-exploit na kuvuka lengo la exploitation?
Ninapata shaka sana kwa ustawi wa taifa la kesho maana kama muda unavyozidi kusogea na tatizo linaongezeka pasipo kushtukiwa, tunaweza tukawa ndiyo kizazi cha mwisho cha jamii yetu.
Ninaamini kuwa masuala kama haya yamo ktk uwezo wa serikali na vyombo vyake vya usalama kuweza kutuhakikishia sisi walipa kodi uhai na ustawi wetu kama TAIFA. Nimeiweka hapa pia iwe kama chanzo cha utafiti wa kina. Au iwezekane kuwa ni uoga wangu tu…..
Naamini kuwa kuna wanabodi waliobobea katika masuala ya afya na wanaweza kutupatia ufafanuzi wa suala hili, na kama kuna mwenye data azimwage humu ili kujua ni wangapi wanafahamu au wamekumbwa na zahama ya uvimbe katika kizazi?
INATISHA
INAKATISHA TAMAA
INAUMIZA AKILI
Prepared By: Msanii