Hata wanawake tunapenda mpira

Hata wanawake tunapenda mpira

Ndan ya box

Senior Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
159
Reaction score
44
Napenda mpira sana na mume hapendi wala hajui kuhusu mpira sisi leo hatareee kucheki peke yangu hainogi mpaka niende sehemu,hapo sisi nashindwa nianze vip kuomba ruhusa .

Wanawake wenzangu mnaopenda mpira mmeomba vipi ruhusa.
 
mimi nilikatazwa kuangalia mpira mpaka sasa nimeshazoe... nilikuwa namtoroka najifanya naenda kulala kumbe ndo kimoja hivyo afu huwa ina raha kuangalia huku unapata kinywaji aisee ila sasa ubovu wangu ampira aliokuwa kaka, drogba na makelel ndo naupenda ...... sasa hii inawezekana kama amuishi wote..
 
Bila shaka we ni team chelsea.
 
Inaitwa opposite attraction...mume anapenda tamthilia mke anapenda mpira na boxing.....Usikute hadi nyumbani mke anaua nyoka..mume karuka juu ya sofa...dunia hii ina mambo
hahahahahahaha THE BOSS umeonaa ee aisee acha tu niende akitaka asinifungulie mlango anune tu kombe la dunia linaanza leo,ngoja tu niombe likizo ya mwezi nisafiri nikacheki huko na wadau
 
Huu mpira wa safari hii na timing zake, mimi nimetayarisha ratiba kabisa, maana Gozi likisinzia likistuka ntaeulizwa mimi, na mimi ndio ntakuwa na kazi ya kumwamsha mechi za usiku wa manane maana ntaambiwa ikianza mechi nistuwe. Hapo sasa!

AlhamduliLllahi Gozi langu halina kutoka-toka usiku, naona anahangaika kuifuta futa mavumbi "video Projector", screen huko nje (uwani) limepigwa rangi mpya nyeupe, viti vimepanguswa kibao, masanduku ya soda yameshatolewa, najuwa leo kuna ugeni si wa kawaida huko uwanjani (uwani). Hili Gozi limemahanika utafikiri labda yeye ndio muandaaji wa World Cup.

Na mie leo ntaona ufunguzi kwenye BIG Screen.
 
Inaitwa opposite attraction...mume anapenda tamthilia mke anapenda mpira na boxing.....Usikute hadi nyumbani mke anaua nyoka..mume karuka juu ya sofa...dunia hii ina mambo
Hapana... mume anaogopa mende
 
We mwambie tu kuwa mume wangu eeh mi ndo nasepa utanifungulia !!
 
Inaitwa opposite attraction...mume anapenda tamthilia mke anapenda mpira na boxing.....Usikute hadi nyumbani mke anaua nyoka..mume karuka juu ya sofa...dunia hii ina mambo

ha ha ha dah hivi wanaume wa hivyo wapo? Niue nyoka ye akimbie??
 
Back
Top Bottom