Hata wanaume hubeba mimba

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,784
730,077
Unaweza kudhani ni story za vijiweni lakini kwa wale wenye watoto tayari kati yao wanaweza kujua nazungumzia nini
Mimba ni matokeo ya muunganiko wa manii ya mwanaume na mayai ya kike, na baadhi ya mimba huja na changamoto mbalimbali kama kuumwa mara kwa mara, kichefuchefu, kutapika unaposikia harufu fulani, kupenda ama kuchukia aina fulani ya vyakula nk nk
Hizi changamoto humtokea mwanamke lakini kwa bahati mbaya sana kuna wakati kibao humgeukia mwanaume na shughuli huanzia hapo
 
kitambii89.jpg

Subiri kuna lift
 
Kuna mkaka Alinisimulia kua wakati baby mama wake mjamzito nae alikua ana experience dalili zote za ujauzito... Hadi siku mdada aanajifungua mkaka alipata homa ya haja mpaka pale mtoto alipotoka. Kwa maelezo yake anasema inatokea kama siku mimba ikitungwa na mdada akaamka kabla ya mwanaume basi anakuachia dalili za mimba... Unakua na kichefuchefu, kupenda vitu vichachu na udongo n.k
Sijui kama ni ukweli
 
Mimi niliteseka miezi mitatu ya mwisho yote, siku ya kujifungua yale masaa kama matani kabla niliumwa na tumbo mpaka nilikuwa hoi siwezi tembea, mwenzangu alikuwa mzima anadeki nyumba, chupa ya mtoto ilipasuka akiwa nyumbani wala hamna habari, alichukuliwa kupelekwa hospitali akiwa mzima wakati mimi nikiwa nyumbani hoi, alipoanza uchungu wa kujifungua tu, mimi mzima, nikaitwa kuchukua mtoto wangu.
 
Kuna mkaka Alinisimulia kua wakati baby mama wake mjamzito nae alikua ana experience dalili zote za ujauzito... Hadi siku mdada aanajifungua mkaka alipata homa ya haja mpaka pale mtoto alipotoka. Kwa maelezo yake anasema inatokea kama siku mimba ikitungwa na mdada akaamka kabla ya mwanaume basi anakuachia dalili za mimba... Unakua na kichefuchefu, kupenda vitu vichachu na udongo n.k
Sijui kama ni ukweli

Labda ndo wale wehu wa mapenzi kila akifanya mwenzie na yy uyo,..
 
Back
Top Bottom