Hata Ukirukaruka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata Ukirukaruka!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 4, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,546
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  [h=3]Hata Ukirukaruka![/h]

  [​IMG]
  Kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ambazo huweza kuzuia mimba. Pia kuna imani potofu nyingi kama si kukosa uelewa halisi wa namna ya kujikinga ili mwanamke asipate mimba na pia zipo njia ambazo watu hutumia na haziwezi kufanya kazi kamwe ya kuzuia mimba.
  Tuangalie baadhi ya imani potofu ambazo watu hutumia wakiamini wanaweza kuzui mimba kumbe ni kujidanganya mchana kweupe.
  NANYONYESHA HIVYO SIWEZI KUPATA MIMBA:
  Ingawa mwanamke anaponyonyesha anaahirisha (postpone) uwezekano wa kupata mimba, hii isikufanye ulemae. Unaweza kupata mimba hata kama unanyonyesha hivyo ni vizuri kutumia njia sahihi za kuzuia mimba.
  MWANAMKE HAWEZI KUPATA MIMBA KAMA HAJAFIKA KILELENI:
  Ufike kileleni au usifike, mwanaume akitoa sperms na zikafika kwenye yai mimba inaingia. Hata kama mwanaume atafika kileleni ili kutoa sperms kwa mwanamke haihitaji kufika kileleni ili kupata mimba.
  SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA NITAJIOSHA (DOUCHING)
  Baada ya mwanaume kumwaga sperms ndani ya uke si rahisi kuziondoa kwa maji kwani huwa zimefika kwenye cervix na huko hakuna kinaweza kuzuia usipate mimba.
  SIHITAJI KUJIKINGA KWA KUWA NIPO SIKU SALAMA.
  Kuna wakati homoni zinazohusika na mzunguko wa siku huweza kubadilika kutokana na umri au dawa mwanamke anatumia au stress na hivyo ni vigumu kujua siku salama ni ipi.
  SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA TUNAFANYA MAPENZI HUKU TUMESIMAMA AU MWANAUME YUPO CHINI MIMI MWANAMKE JUU.
  Unajidanganya, hata kama upo juu ya mwanaume sperms zinao uwezo wa kupanda mlima wowote kwa speed ya ajabu maana zinajua kile zinakitafuta yaani mimba.
  Naturally, hata kama ni wima au juu sperms zina namna yake ya kwenda bila tatizo na kufanya kila kinastahili, mimba.
  NAWEZA TUMIA BALLOON AU MFUKO WA PLACTIC KAMA SINA CONDOM.
  Condom ni tofauti na plastic bag au balloon, kwanza haviwezi ku-fit vizuri na vinaweza kupasuka muda wowote.
  Pia condom zimekuwa tested kwa ajili ya kufanya kazi tofauti na mchezo wa kijinga unaofanya.
  SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA MWANAUME ATATOA KABLA YA KUMWAGA MBEGU.
  Si njia sahihi kwani hata kabla ya kuingiza kuna kiasi fulani cha sperms huwa tayari zimeingia na zaidi kuna wanaume ambao uwezo wa kutoa hana na hata akitoa (withdrawal) anakuwa tayari alishamaliza habari.
  Kazi kwako!
  SIWEZI KUPATA MIMBA KWA KUWA NI SIKU YANGU YA KWANZA KULALA NA MWANAUME:
  Haijalishi ni siku ya kwanza au la kama ni siku ambayo unaweza kupata mimba basi mimba itapatikana tu.
  SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA NITAENDA HAJA NDOGO BAADA YA SEX
  Kwenda kukojoa hakuwezi kuondoa sperms ambazo zimesha enda kwenye uterus.
  BAADA YA SEX NIKIRUKARUKA SIWEZI KUPATA MIMBA
  Ruka tu kadri ya unavyoweza kama ni mimba itakuwa imeingia tu kwani kuruka juu baada ya sex hakuzuii kupata mimba bali zoezi tu la kawaida la kupunguza uzito na kujiweka fiti.
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  mhh iyo ukimaliza ku do unarukaruka.......nmeipendaaaaaaaaa INANSAIDIA SANA!!!!!!!
   
 3. M

  Mom 2b Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 1, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kurukaruka kutakusaidia kuwa fit phisically na co kuzuia mimba Rose!
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  itabidi kamba za kuruka ziingie kwenye kundi la contraceptives.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,546
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  haaahaaa sangara nimeeipenda hiyo
  nipe jina lamradi niandike bussiness plan faster
   
 6. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  nadhani tuite "ruka kamba uzuie mimba"
  ndani tuelezee kwamba ukiruka kamba baada ya njunji utazuia mimba na kufanya zoezi.
  faida mara mbili.
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,546
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  haaahaaaa hiyo sangara brela watatunyima reg ..tafuta fupi
  aya bana ngoja nielekee lunch nisije nyimwa unyumba usiku kwa kuchoka mwaya huku weye wala sangara
   
 8. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mie huwa natumia hiyoya Kurukaruka na inafanya kazi
   
 9. d

  dave80 Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unatisha na hili darasa lako,maana twapata japo dondoo moja mbili tatu
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  somo limeeleweka........................thank u 4 that..............
   
 11. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Noted mkuu. Hasa hiyo ya kurukaruka. Nikimpata my wife wangu nampa darasa ili tupange uzazi... Sante sana.
   
Loading...