Hata sielewi namna mambo yalivyo duniani

Hata sielewi namna mambo yalivyo duniani

St Augustino of Hippo alishawai kusema kuwa duniani ni mateso ila ukifa ndo utapumuzika
Unapumzika au unatoweka kabisa...
If we are no different to animals, mbona hatu apply hii kwa wanyama... Leo ukichinja kuku utawazia kuhusu uwepo wa kuku baada ya kumla? Kwann wewe binadamu kufikiri kuwa utaishi au kupumzika baada ya kifo?
 
Mtu mwenye huzuni na kukata tamaa hujiuliza hayo maswali,
Wewe ishi huwezi jua labda huku duniani ndio tunapoadhibiwa halafu tunarudi tena kuendelea na maisha ya huko tulipotoka, ukipata chance ya kuishi we ishi tu ukifa ndio utajua
Hayo ni maswali yanayoulizwa na ma genius na wanafalsafa nyakati zote za historia ya dunia
 
Hayo ni maswali yanayoulizwa na ma genius na wanafalsafa nyakati zote za historia ya dunia
Kuna watu huwa wanafikiri kuishi kwa kufuata kila kitu ni sawa, mtu yoyote anaye question reality ni kapuku...

Ila if we look throughout history all inventions came from curiosity of reality.. Kina Plato, kina Einstein, kina Newton.. They both questioned
 
Kuna watu huwa wanafikiri kuishi kwa kufuata kila kitu ni sawa, mtu yoyote anaye question reality ni kapuku...

Ila if we look throughout history all inventions came from curiosity of reality.. Kina Plato, kina Einstein, kina Newton.. They both questioned
Tanzania ni nchi ya uswahili na taarabu zaidi
 
Quran (51:56)
"Wa maa khalaqtul-jinna wal-insa illaa liya'buduun"

Maana: Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu Mimi.
 
Quran (67:2)
"Alladhii khalaqal-mawta wal-hayaata liyabluwakum ayyukum ahsanu 'amalaa."

Maana: Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri zaidi.
 
Quran (23:115)
"Afa hasibtum annamaa khalaqnaakum 'abathan wa annakum ilaynaa laa turja'uun."

Maana: Je, mlidhani kwamba tumekuumbeni bure tu na kwamba hamtarudishwa Kwetu?
 
Quran (29:64)
" Wa maa haadhihil-hayaatud-dunyaa illaa lahwun wa la'ib, wa innad-daaral-aakhirata lahiyal-hayawaan, law kaanuu ya'lamuun."

Maana: Na maisha haya ya dunia si chochote ila ni mchezo na pumbao. Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo maisha halisi, lau wangelijua.
 
Sheria za Mungu ni maelekezo ya matumizi (Instructions manual).

Kama ambavyo ukinunua simu waliyoitengeneza wanakuambia usiiweke kwenye maji,
usifungue inbuilt battery,
usiichaji na umeme mkubwa kuliko standard,
usidownload vitu kutoka vyanzo wasivyovitambua etc.

Kukuambia hivyo sio wanataka kukukomoa ushindwe kui enjoy kwenda swimming na simu yako ujipige picha ndani ya maji!

Au wanakukomoa usipate programs nyingine mpya mpya nzuri kutoka kwingine!

Basi na Mungu aliye design ulimwengu wake na vyote vilivyomo ana maelekezo ya matumizi kulingana na alivyo design.

Sheria za Mungu ni maelekezo ya matumizi, sio masharti ya kutukomoa.

Mpinzani wa Mungu alitokea kukataa ukweli huu.

Ndio Mungu akatuacha sasa tuko zetu swimming na simu zetu chini ya maji ghafla zimezimika hatuelewi,

wengine wamefungua battery simu imewalipukia hawaelewi,

wengine tumedownload zetu kila kilichotupendeza sasa tunashangaa message na email zinatumwa wakati sio sisi tumetuma hatuelewi...

Ni kweli hatuelewi au kujitoa ufahamu!

Cha kufanya kwa ambaye angependa kupata simu mpya ni kukubaliana na designer kuwa maelekezo yake ni sahihi, kisha kurudi kwake na kuwa wapole msubiri mpate simu zenu mpya kwani ameshalipia gharama za uharibifu wenu naye ameahidi atawapa simu mpya wote watakaorudi kwake.

"Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele.

Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe."

Yohana.3.16-17.BHN


Wabishi wataendelea kumtukana na kumdhihaki designer kuwa hajui kutengeneza, katengezeza kitu kibovu, huku wakitafuta njia mpya za kwenda kinyume na matumizi wakiharibu zaidi, huku wakijaribu kuigilizia design na kutengeneza yao mpya wanayofikiri ni bora...na muda hauko pamoja nao...
 
Back
Top Bottom