Hata kama kitanda hakizai haramu.

Hata kama kitanda hakizai haramu.

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,195
Mnajua sisi wanaume tunaumia sana kulea mtoto ambae unaambiwa ni wako lakini kwa macho ukimuona tu unajua hapa nimebambikiwa kufanana kafanana na Mangi muuza duka.

Ni sawa kitanda hakizai haramu lakini mnapochepuka chepukeni na box za Condom mbona zinatolewa kwa msaada tu zile za MSD.

Hivi mnajua machungu ya kulea mtoto ambae unajua kabisa siyo wako lakini kusema tu unashindwa unabaki kumezea,

Alafu sasa watoto wa namna hii wanakuwaga ving'ang'anizi kinyama kuliko ata yule ambae unahisi ni mtoto wako wa damu.

Ukiamka kenyewe ndio ka kwanza kukulilia alafu kama una kagari kanapenda sana ukape funguo na kukimbilia huko ukipigishe starta kirizike.

Yaani wanakujaga na Moto kinoma .

Lakini tufanye nini sasa mmeshatupatia basi hatuna budi kuwalea lakini muwage na huruma ata kidogo ,

Ukiona mtoto wa kiume kafa ujue kafa na Mengi moyoni.
 
MKUU YAMEKUKUTA NINI??
Haya mambo yapo sana uswazi kwetu,ma wenye tabia ya kubambikia watu watoto ni wanawake wa kimakonde
 
Mimi nikagundua TU ndo nakuacha Hakuna Cha mswalia mtume Wala kristo..pita hivi na Mimi nipite kushoto.na kwa taarifa yako mke wangu Kama unasoma comment yangu Sasa hivi nakupa tahadhari maana Sasa hivi najiandaa nitafute hela nikampime huyu mtoto wetu DNA
 
wewe kweli zero IQ..

Uzi wako uliokuwa unatafuta mchumba umeusahau.??
 
Uzi gani nimetafuta mchumba mkuu umesoma vibaya nilisema Zero iq sasa nataka kuoa hiyo haimaanishi kwamba natafuta mchumba mkuu.
wewe kweli zero IQ..

Uzi wako uliokuwa unatafuta mchumba umeusahau.??
 
Siyo mimi mkuu ila wewe nakuona hapo kwenye Avatar yako kipindi hicho unakimbilia kujirutubisha kwenye yai.
tena inabidi ajisifu aliogelea nakuwashinda mabilioni wenzake. Na hapo alipatikana baada ya mshua kutoa sauti ya kukoromaa huku akinyong'onyea ka mlenda
 
Umechezewa rafu na adhabu unapewa wewe. Ndiyo mechi za kimaisha hizo. Ukilea mtoto wa kupachikiwa shukuru aliyekuchezea faulo maana unakua unalea malaika. Wewe lea tu, Mungu atakulipa kwa wema wako.
 
Back
Top Bottom