Hii ya Kitanda hakizai haramu…………………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ya Kitanda hakizai haramu…………………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 30, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Msiniite mbea na sipigi chuku wala sifanyi fitna………………….

  Week end hii, nilimtembelea mzee mmoja ambaye nilitambulishwa na rafiki yangu anayeishi mkoani. Nakumbuka nilipokuwa huko mkoani nilibahatika kufahamiana na jamaa mmoja na katika mazungumzo yetu alinijuza kwamba anaye mjomba wake huku Dar na akanipa mzigo fulani niufikishe kwa huyo mjomba wake.
  Baada ya kuwa bize kwa majuma kadhaa, week end hii nikawasiliana na huyo mjomba wa jamaa yangu na baada ya kunielekeza kwake nikafunga safari hadi pale kwake. Nilikaribishwa vizuri sana na kwa kuwa ilikuwa ni weekend siku ya mapumziko, nilibahatika kuikuta familia yake, wote wakiwa hapo nyumbani. Baada ya kunitambulisha kwa mkewe, aliwaita wanae ili anitambulishe kwao.

  Walikuja wavulana wanne na wasichana wawili mdogo kabisa wa kike alionekana kuwa na umri wa 14 hivi na mkubwa kabisa wa kiume nadhani alifikia miaka 30 hivi. Alinijulisha kuwa wale wote ni wanae na huyo mkubwa ameshaoa na anajitegemea na wavulana wengine wawili hawajaoa lakini wanajitegemea pia. Pale nyumbani walikuwa wamebaki wale wasichana wawili na mvulana mmoja.

  Huyu mvulana ndiye ninayetaka kumzungumzia. Kati ya wale watoto wa yule mzee huyu alikuwa tofauti kabisa na wenzake........yeye alikuwa ni mweupe na nywele zake kama za shombe kama za kiarabu ingawa wazazi wake wote yaani mjomba na mkewe ni weusi tii kama mimi Mtambuzi.......Awali nilidhani ni mtoto wa ndugu yake lakini alimtaja kama mtoto wake wa nne kuzaliwa kati ya watoto wake 6 aliowazaa na mkewe.

  Anyway sikutaka kufanya udadisi. Lakini jana wakati nazungumza na huyu jamaa yangu wa mkoani kwenye simu kumjuza kwamba nimefikisha ule mzigo alionipa kwa mjomba wake.......kama vile alisoma mawazo yangu, aliniuliza kama nilimuona yule mtoto wa mjomba wake mwenye asili ya kiarabu.......nikamjibu ndio, na ndipo akaniambia kuwa yule mtoto alileta ugomvi mkubwa katika ndoa ya mjomba wake na almanusura ndoa yao ivunjike, ni busara za wazee tu waliinusuru ndoa ile kwa kigezo kwamba kitanda hakizai haramu..............

  Mungu aniepushe na balaa hilo kwa Mama Ngina............
   
 2. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hekaya za Abunuwas
   
 3. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  hahahahaaaaaaa.......sijui ntakuchekaje siku hiyo na kujidai mjanja kisha unaletewa burushi.
   
 4. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  nimeipenda hii,.....
   
 5. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hivyo vilikuwa vitanda vya zamani wakati kamati za ufundi zikifanya kazi ( wazee wa kusuluhisha mambo), siku hizi, hizi kamati hazina nguvu, wahusika mke/mme ndo wanapima na kutoa maamuzi. au mama ngina wako akichakachua utasubiri kamati ya ufundi ikuamulie?
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,980
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  kubwa katika dhana ya kitanda hakizai haramu ni kuwa mtoto asiadhibiwe kwa maamuzi ya wazazi wake ambayo hakushirikishwa katika kuyafikia....................kwa hiyo kama wako kwenye ndoa mtoto awe kazaliwa na mwaumme wa nje baba wa ndani kumtambua kama wa kwake.....................ninaamini kwa kufanya hivyo ni kumtendea haki mtoto
   
 7. tabibumtaratibu

  tabibumtaratibu JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 2,297
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  Mmmmmmmh!
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,980
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  kama umeipenda kutoka moyoni mbona hujampongeza kwa kumbonyezea kitufe..............................au hizo ni geresha zako?
  [MENTION]@vaislay[/MENTION]
   
 9. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wangu hata wazee waitwe talaka lazima
   
 10. S

  Shaabukda Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yawezekana msemo huo una busara kubwa tu hususani katika kumlinda mtoto dhidi ya unyanyapaa anaoweza kuupata kutoka kwa baba na hata pengine kukosa malezi mazuri. Zamani ilikuwa ngumu kiasi kupata parental status ya mtoto lakini kwa sasa DNA inaweza kumaliza utata kwa sehemu kubwa.
   
 11. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  hizi ni mbwembwe tu ruta, mbona hivyo!:frusty:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,679
  Trophy Points: 280
  Nitamsamehe akiwa muwazi!Huyo si mtoto wangu huo ni ukweli ambao hata kama nitajifanya mwehu kiasi gani siwezi kulibadili hilo.Nitahitaji nimjue baba wa mtoto ili niangalie kama ataweza kumhudumia mwanae,hata kama atakua hawezi ni lazima apewe taarifa kuwa ana mtoto,kisha nitamhudumia kama mwanangu.Huo ndio ukweli!
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  ndo maana ndoa za wazee wetu zilidumu....
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huyo mtoto akikua atajiona ni different kuliko wenzake na wazee wake hasa ikiwa hawana asili yeyote ya kiarabu au ya kiasia. Katika maisha yetu haya ni wengi tu wanalea watoto si wao bila kujua iwapo kama mama atatoka na mmatumbi mwenzake hizo tofauti za kimaumbile hazionyeshi na inabaki ni siri ya mama tu.

  So all the guys out there it not over yet..............
   
 15. J

  JOJEETA Senior Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah kweli kitanda hakizai haramu jaman,nina mjomba wangu kalea 1st born wake ambae mpaka kesho anajua kua c wake bt huyo huyo ndo anaem2nza ktk uzee wake huu.hiyo ni zaman vijana wa sasa hata ukicheat kwenye mahuciano b4 marriage una2pwa kulee
   
Loading...