Kutoka kwenye ukuta wa Bollen Ngetti Face Book nami nawasukumia bila kuongeza neno.
Kuna mambo mengine ukikutana nayo yanachefua na kutia kinyaa. Yani utadhani viongozi woooote wa Mkoa wa Dar es salaam wameenda likizo, hawapo au wameamua kusubiri ziara ya Rais Magufuli ndio aje kutoa maagizo baada ya kuwatumbua.
Kwa walio jijini Dar watanielewa sana. Ukifika maeneo ya Akiba, mbele ya Chuo Cha Biashara na Uhasibu (NBAA) mbele ya geti la kutokea nje (OUT) kuna chemba ya majitaka imefumuka hapo sasa ni mwezi mzima!
Maji yote machafu yametapakaa barabarani ni harufu mbaya kiasi kwamba hata Inzi wanaogopa kusogelea.
Kwamba wanaosogelea maji hayo ya kinyesi cha binadamu na walioyafanya kuwa manukato ni wanafunzi wa CBE, NBAA, wateja matajiri wanaokuja kula Great Wall Restaurant na mama lishe wanaowapikia wanafunzi hao pembezoni mwa njia ambao sasa wameshiba harufu hiyo ambayo kwa mimi nimeumwa tumbo la kuhara!
Kinachofurahiaha ni kwamba, Mkuu wa Mkoa yupo, DC yupo, Mkurugenzi wa jiji yupo, madiwani wapo, Dawasco wapo, kila aina ya viongozi wapo lakini sasa ni raha kumsubiri Rais Magufuli atoe maagizo ndipo pashughulikiwe! Dah!
Rais Magufuli si unipe U-DC wa Ilala walau kwa saa 4 tu niokoe afya ya wanafunzi wa CBE?! Kinyaa!
#TwendePamoja2025