Hili nimewahi kulifikiria pia.
Historia na Biblia vyote vinaeleźea kuwa watu wa kale waliishi miaka mingi sana. Historia ikisema zaidi ya miaka elfu moja (1,000) huku Biblia ikisema binadamu aliyeishi miaka mingi aliishi miaka 930 ambaye ni Adam.
Musa anakufa na miaka 120 akiwa mwenye nguvu... Kutoka kwa Adam hadi kwa Musa ni miaka mingi sana, zaidi ya 2,000. Na Musa hakufa kwa uzee ndo maana Biblia inasema alikuwa akiwa mwenye nguvu.
Kutoka kwa Adam, Musa na sasa binadamu wa dunia ya leo ni takribani miaka 6,000 kwa mjibu wa Biblia ila lifespan (umri wa kuishi) umetoka miaka 930 ya Adam hadi 80 ya mwanadamu wa sasa (Na hii miaka 80 mtu anafika kachoka kweli kweli)
Hii inanipatia picha kwamba, miaka 100 au 200 ijayo, mtu kufikisha umri wa miaka 50 hadi 60 itakuwa jambo gumu sana (Kama tunavyoona Covid ikawatafuna wazee zaidi, na wengine ni watu wa miaka 40+ tu)
Je, hii inakupa picha gani baada miaka 1,000 ijayo??
Pia tutazame mabadiliko ya miili yetu kwa sasa.... watoto wanawahi sana kubalehe na kuvunja ungo. Si ajabu kwa sasa kuona binti wa miaka 8 au 9 kashaanza kubalehe. Zamani kidogo ilihitaji miaka 12 hadi 15 kwa mtoto wa kike kuingia balehe.
Tazama pia maumbo ya wachezaji mpira wa miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa 2000 ni tofauti kabisa na maumbo ya wachezaji mpira wa kizazi cha sasa.
Extinction ipo, japo ni miaka mingi ijayo, kadri tunavyozidi kuwa wengi ndivyo umri wa kuishi unavyozidi kupungua pia... kama ambavyo hatujui mwanzo wa dunia ndivyo ambavyo hatutojua mwisho wa dunia.