Tetra
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 1,520
- 764
Diana na Gidion (si majina halisi) ni marafiki wa tangu utotoni,urafiki wao sasa umekua hadi kuwa wapenzi! Naam ni wapenzi,ambao vijana wengine wanawamezea mate! Wanavyotembea,wanavyojaliana,na hata wanavyoheshimiana.Kila anaewajua Diana na Gidioni,anakiri upendo huu ni wa pekee sana,,pengine zawadi toka kwa Mungu.
::
Jumamosi moja walikuwa wameamua kujadili juu ya harusi yao.Kila mmoja anapenda kuishi na mwenzake ili atimize dhati ya moyo wake.
::
GIDIONI
Naomba uwe mwelewa Diana,harusi haiwezekani,na unajua jinsi gani nakupenda,pia sielewi ni jinsi gani naweza bila wewe.Lakini unamjua baba yako,alivyosema kuhusu mahari milioni 4,gari 2,ng'ombe 5 alisema anataka kuona faida ya kukusomesha,je uwezo huo familia yangu itautoa wapi?
DIANA
Sema hutaki kunioa tu,rafiki zangu wote wamekuwa na harusi kubwa.Tangu zamani nimeota ndoto za kutembea katikati ya watu,nikiwa nimevaa gauni la bibi harusi,ndugu na jamaa zetu,wakituangalia kwa fahari.Gari kubwa likitungoja kutupeleka kwetu,sherehe kubwa hotelini,LEO unasema..sem..a (Diana analia)
::
GIDIONI
(anatafakari,kisha anasema) Arusi kubwa,gari kubwa,gauni zuri,nani atalipa hayo yote?Kama tunapendana hasa,arusi siyo ya maana hasa.Diana we si mtoto tena,tuangalie mambo ya msingi!
::
DIANA
Mbona wanaume wenzako wanafanya hivyo! Hata watu husema,harusi hupata baraka za Mungu na ili tubarikiwe lazima tufunge ndoa halali,sema tu umepata mwingine!
GIDION
Ni kweli,watu wanasema kufunga ndoa huleta baraka,lakini unafikiri Mungu hawezi kutubariki ktk nyumba yetu tukimwomba? Naamini Mungu aweza kufanya hivyo maana yeye ni mwema.
.
Diana na Gidioni,hawakuendelea mbele,kila mmoja akitafakari jambo lake mwenyewe,kila mmoja aliondoka kimya.
::
NAAM,ikiwa familia moja wanadai mali kubwa kusherekea sherehe ya siku moja ilihali upande wa pili hauwezi kugharamia basi hao ni wachoyo.Maana familia hizi huwaacha vijana wakabiliwe na uamuzi usio wa haki.
=
Harusi sio nafasi ya kujigamba,na furaha ya ndoa haitegemei gauni la bibi harusi,gari wala idadi ya watu bali upendo moyoni.Hatukatai ndoa au harusi kubwa Lakini tuangalie uwezo kuliko kuwaacha wanandoa kuanza maisha ya ndoa kwa madeni.