Mwaka jana mwezi wa 9 nilipokea text WhatsApp kutoka kwa ndugu yangu (mdada) ya mchango wa harusi.
Mzee mzima nikajichanga nikarusha 50,000/- Mpesa kupitia kwa msela Wangu yupo bongo japokuwa nipo nje ya nchi.
Harusi ilikuwa mwezi 12 siku 4 kabla ya Xmas.
Nikasema mambo si ndo Hayo nikarudi Tz kusalimia home na harusi juu.
Harusi bab kubwa tulikula tukanywa soda na gambe la kufa mtu, hadi kwa sisi wadau wa rubisi na karobo na senene zilikuwepo.
Bibi harusi na farasi alipanda honeymoon Mauritius.
Khe Leo napata habari ndoa imekufa.
Kwa kweli nimesikitika ila kimoyomoyo nasema bora nilirudi kula kuku Wangu niliochangia.
50 yangu haikwenda bure.
Sent using
Jamii Forums mobile app