Harusi bab kubwa ndoa chali

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
9,504
12,175
Mwaka jana mwezi wa 9 nilipokea text WhatsApp kutoka kwa ndugu yangu (mdada) ya mchango wa harusi.
Mzee mzima nikajichanga nikarusha 50,000/- Mpesa kupitia kwa msela Wangu yupo bongo japokuwa nipo nje ya nchi.

Harusi ilikuwa mwezi 12 siku 4 kabla ya Xmas.
Nikasema mambo si ndo Hayo nikarudi Tz kusalimia home na harusi juu.
Harusi bab kubwa tulikula tukanywa soda na gambe la kufa mtu, hadi kwa sisi wadau wa rubisi na karobo na senene zilikuwepo.

Bibi harusi na farasi alipanda honeymoon Mauritius.
Khe Leo napata habari ndoa imekufa.
Kwa kweli nimesikitika ila kimoyomoyo nasema bora nilirudi kula kuku Wangu niliochangia.
50 yangu haikwenda bure.

Updates:
Bwana harusi hakujua kama bi harusi ana mtoto wa miaka 5.
Dada kaniangusha.
Mi nilidhani anajua maana huyo mtoto kwenye harusi nilimuona.

Ishu kama hii ilimtokea dingi mkubwa miaka ya 80.
Alichoamua yeye niendelea na ndoa ila yule mtoto hakukanyaga kwa dingi mkubwa hadi alipofariki. (miaka kama 15 imepita hivi). Nilipokutana na huyu mtoto baada ya msiba (Alikuwa ni bro kwangu) sikuamini maana alikuwa Model na kwenye matangazo ya mabango mjini picha zake nilikuwa naziona ila sikuwa najua ni mtoto wa maza mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikama habari hii imekufurahisha sana mkuu....
Binafsi, sijawahi kufurahia ninapo ona ama kusikia kwamba wana ndoa wameachana. Sababu hadi wanafikia kufunga ndoa, lengo lao halikuwa kuachana. Na hata inapo tokea wameachana yawezakuwa sababu ni wao kupendana sana hata kusababisha tofauti hata waka achana.
And unaeza kuta wana ndoa wameachana ikingali bado wanapendana pia, na hii tafasiri yake ni kwamba sio kila wanao achana basi maana yake hawapendani.
 
Chanzo cha ndoa kufa ni nini mkuu?

Back
Top Bottom