komedi
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 204
- 17
Kinyozi mmoja mndengereko aliamua kuoa mchaga ili akizaa watoto wawe na harufu ya kichaga ya kuijua pesa kwa sababu alihisi yeye hakuwa nayo kabisa. Alifanikiwa kupata mtoto wa kiume akamwita jina lake Masawe.
Siku moja mtoto akiwa na miaka minne aliamua kumjaribu mbele ya wateja wake na kumpa achague kati ya shilingi 200 na shilingi 500. Mtoto Masawe akachagua shilingi 200 akaiweka mfukoni na kuondoka. Yule Kinyozi akakasirika sana na akawa akiendelea na zoezi hilo kwa miaka miwili bila mafanikio.
Siku moja alitembelewa na mteja mchaga, akamlalamikia juu ya jambo hilo na kudai kuwa amezaa mtoto na mwanamke mchaga lakini huyo mtoto hana hata harufu kidogo ya uchaga. Wakakubaliana na mteja huyo mtoto aitwe na zoezi lile lifanyike tena. Kama kawaida yake mtoto Masawe alipopewa shilingi mia 200 na shilingi 500 akachukua shilingi 200 na kuondoka.
Baadaye yule mteja mchaga akakutana na mtoto Masawe akiwa na wenzake anacheza na kuamua kumuuliza. '' hivi Masawe kwa nini ukipewa na baba yako sh 200 na sh 500 unachagua sh 200?'' Mtoto akajibu, '' siku nitakayochagua sh 500 ndio utakuwa mwisho wa huu mchezo!''