Harufu Mbaya ya Ufisadi Katika Daraja la Kigamboni

Harufu Mbaya ya Ufisadi Katika Daraja la Kigamboni

Kwa jinsi ninavyo ijua serikali ya Ccm, mradi mkubwa kama huo lazima kuna ujanja umefanyika. Kiuhalisia hizo gharama zipo juu sana, tuweke pembeni hisia zetu na mapenzi yetu kwenye vyama vyetu vya siasa kisha tulitazame hili kama watanzania na siyo wana Ccm au wana UKAWA.
Hata kama wameiba ila walau tumeona kitu
 
Tukisema 'watanzania ni wajinga' (ujinga ambao Mwalimu alikesha kuupiga vita) haina maana kuwa wajinga ni wananchi tu bali huenda viongozi wao ni wajinga zaidi. Ingelikuwa kama wanaoiba zaidi kama mfano awamu ya nne wanaishi zaidi ya miaka ya kawaida tungesema sawa lakini sote life span yetu ni equivalent.
Daraja la Kigamboni eti wanasingizia 'CAVITIES' ndio zimeongeza gharama utadhani hawakufanya feasibility study!
 
Hakuna hata shilingi iliyoibiwa bwana! Hujui mradi huo ulikuwa unasimamiwa na vyombo viwili makini sana.
NSSF ambako alikuwepo alhaj mtu mkamilifu na mcha Mungu ambaye watu wameshasema anakimbilia utakatifu.
Na serikali chini ya wizara ambayo ilikuwa na waziri mwadilifu haijapata kutokea hapa nchini. Waziri huyo kwa sasa tumempa mamlaka mengine na tumekubaliana tusihojihoji ila kumsifia tuu
 
Ni Dr Dau huyu huyu aliyeitwa na Magu kufungua daraja au mwingine?
 
Suspension bridge are very expensive ukitaka kufananisha labda lifananishe na akashi bridge la Japan lililotumia mabilioni ya dola na miaka 10 kujengwa wkt lina km 2 tu.

Don't compare suspension bridge with normal bridge sbb ni kma apples n oranges
Tunaangalia uwalisia
 
Daraja la show Kigamboni limegharimu bilioni zaidi ya 200+. Halafu serikali hii inasema inatenga bilioni chini ya 50 kwa ajili ya reli ya kati. Hivi hii ni akili au makamasi?
 
WASTANI WA GHARAMA ZA UJENZI WA MITA 1 TZ NI =417,065,440/-

Lakini China ni
62,372,872/- tu. Kwa mita 1.

Gharama ya Tz zimefanywa kuwa kubwa kuliko ya China kwa zaidi ya 660%.

Gharama ya ziada Tz ukilinganisha na China ni 212,815,541,000/-

Na, Solomon Michael Kambarangwe

Nifuateni....twende pamoja kwa ufafanuzi.

Ndugu wananchi wenzangu, kwa mtu anayejielewa na kufuatilia mambo ya nchi yetu hata tofautiana na mimi kuwa watendaji wa chama cha mapinduzi (CCM) mara nyingi yaani kwa 99% hawawezi kufanya maunuzi bila kuibia Watz masikini kupitia manunuzi hayo

Yaani wao ni tabia na jadi kwao na mara nyingi asiyekubali kuchakachua kupitia shughuli za ofisi ya umma hupata maadui wa makada wa ccm.

Nimefanya udadisi wa gharama za ujenzi wa daraja la Kigamboni baada ya kuelezwa gharama iliyotumika na kulinganisha gharama za ujenzi wa daraja la kupita baharini nchini China lenye urefu wa Km 41.3 refu sana kuliko la Kigamboni.

Baada ya ulinganifu huo nimegundua kuwepo kwa kila dalili ya ufisadi mkubwa sana ktk ujenzi wa daraja la Kigamboni japo viongozi wa serikali ya ccm hawataki hilo lisemwe.

BAADHI YA KUMBUKUMBU ZA UFISADI WA SERIKALI YA CCM KATIKA MANUNUZI NA UTEKEREZAJI WA MIRADI

1. Manunuzi ya Magari hewa yenye thamani ya 4.3 Bilion CAG report ya 2009

Ilidaiwa na wakala wa manunuzi wa magari ya serikali kuwa yalizama baharini yakisafirishwa kutoka Japan.

Kamati ya bunge ilienda kuthibitisha ikakuta hakuna hata karatasi wala ofisi ya wakala huyo. Ila viongozi wa umma waliishakuwa kimya na pesa zilimezwa na mafisadi.

2. Mradi wa ujenzi wa Magorofa Pacha ya BoT ulidaiwa kugharimu zaidi ya Bilion 522.4 Tshs. Gazeti la MwanaHalisi la April 20, 2011 lili-report.

Wizi huu ulifanyika wakati wa serikali ya Mkapa.

3. Manunuzi ya Radar

Bei halali ya Radar sokoni ilikuwa Pound 12 Mil ila serikali ilidai imenunua Radar kwa Pound 40 Mil. Yaani mafisadi wa ccm waliongeza na kuibia Watz Pound 28 Milion

Kwa Sh.ya Tz ikiwa £1 = 2300 wakati huo

28,000,000 X 2300
=64,400,000,000/- Tshs ziliibwa kupitia manunuzi hayo.

Hiyo ni mifano michache tu inayoeleza ufisadi wa kutisha wa viongozi kupitia CCM.

China wamefungua daraja lenye urefu wa km 41.3 baharini na limegharimu USD 1.4Bilion

Daraja letu la Kigamboni lina urefu wa mita 600 baharini na limegharimu USD million 136

China: 1,400,000,000÷ 41300=
33,898.305085 USD, kwa Ujenzi wa mita moja ya Daraja China.

136,000,000 USD :- 600= 226,666 USD

Gharama ya kila Mita 1 kwa Tshs.

1840 X 226666
417, 065,440/-Tshs

Gharama ya kutengeneza 1 moja ya daraja Kigamboni.

Na
417065440X 600
=
250,239,264,000/-

Yaani 250.3 Bilion Tshs. kwa Ex.Rate ya 2840 Tshs sawa na dola 1 ndiyo ilitumika kujenga na kukamisha daraja la Kigamboni.

Kwakutumia uwiano sahihi wa China kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni lililojengwa na Wachina, ilitakiwa kuwa hivi:

33,898.305085 x 600= 20,338,980 USD sawa

20,338,980 X 1840
=37,423,723,200 Tshs

Yaani Bil.37.4 Tshs.

Ndiyo ilitakiwa kugharimia daraja la Kigamboni kwa mujibu wa gharama halisi kwa kulinganisha na gharama iliyotumika Uchina kutengeneza Mita 1 ila gharama iliyotumika Tz imekuwa juu ya ile ya Uchina kwa zaidi ya 660%.

TOFAUTI YA GHARAMA

250,239,264,000 - 42,423,723,000
=212,815,541,000/-

Maana yake, gharama ya kutengeneza daraja la Tz Kigamboni zaidi ya ile ya China (Inflated value) ni 212,815,541,000/- Tshs.

MAONI YANGU

1. Kufanyike uhakiki/audit na chombo huru ya matumizi ya fedha za umma kubaini ukweli maana haiwezekani gharama za Tz ziwe juu ya gharama za uchina.

2. Ikibainika kuwa ni kweli, adhabu ya wanaofanya ufujaji wa fedha za umma namna hii wanastahili kunyongwa hadi kifo.

Share ujumbe huu na wananchi wengine ili tudai haki ya matumizi sahihi ya fedha za umma na kuwaeleza watawala wajue hatutaki uovu ktk matumizi ya fedha za umma unaoathiri maisha ya wanyonge.

Wakati unatafakari hayo....kumbuka:-

*ukosefu wa ajira

*hali mbaya ya huduma ya afya.

*hali mbaya ya huduma ya elimu.

*vijana wanakosa mikopo n.k

Toa maoni yako kuhusu ufisadi na watendaji kuongeza gharama kwenye makaratasi wakiibia wananchi na mazoea ya chama cha mafisadi kulinda na kuhifadhi mafidadi papa ila wakifanya kushugulikia mafisadi vidagaa.

Je, Magufuri si alikuwa Waziri katika serikali iliyopita?

Aliishauri nini serikali ktk hili? Je, hii cost inflation anaifumbia macho? Ameridhika nayo?
Kwanini usilinganishe Daraja la Kigamboni na Daraja la Akashi huko Japan ambalo ni "suspension bridge" pia lenye wastan wa urefu mara nne ya Kigamboni lililoigharimu Dola billion 3.6 (trioni 7.5 za kitanzania)? Shughulisheni akili zenu siku nyingine kwani kwa akili hizo hazitawapeleka katika nchi ya uchumi wa kati mnavyotaka.
 
DARAJA LA KIGAMBONI

CHINA LONGEST BRIDGE
Kwa wenye kufahamu hesabu walinganishe links hapo juu tusiwe tunapotosha ukweli na kubakia kwenye siasa, aliyeanzisha Uzi hayupo realistic bado yupo kisiasa.
Daraja la Kigamboni gharama yake ni US$ 136 million kwa urefu wa mita 680 sawa US$ 200,000 kwa mita ambayo ni Tzs 440milioni kujenga mita moja kwa rate US$ 1 =Tzs 2200.
Daraja la China kama ilivyo kwenye link hapo juu imejengwa kwa
UK £5.5 billion sawa US$ 8.24billion kwa urefu mile 26.4 sawa na
km 42.24
Km 42.24 ni sawa mita 42,240
US$ 8.24 billion ukigawanya kwa mita 42240 unapata gharama ya kujenga hiyo daraja la China ni US$ 195,312.5
kwa mita moja saws Tzs 429.7 million na tofauti ni sisi tuna import technology wakati wenzetu wanatumia technology yao ya ndani.
Mleta Uzi uweke link kuthibisha hayo unayoyasema.
Update:- Naona hiyo link hafunguki nilivyotajia lakini habari hiyo halo chini
China's vaulting economic ambition has set a new record with the construction of the world's longest bridge over water.

At 26.4 miles long, the Qingdao Haiwan Bridge would easily cross the English Channel and is almost three miles longer than the previous record-holder, the Lake Pontchartrain Causeway in the American state of Louisiana.

The vast structure links the centre of the booming port city of Qingdao in eastern China's Shandong Province with the suburb of Huangdao, spanning the wide blue waters of Jiaozhou Bay.

Built in just four years at a cost of £5.5 billion, the sheer scale of the bridge reveals the advances made by Chinese engineers in recent years.

No longer dependent on western expertise for such sophisticated projects, the six-lane road bridge is supported by more than 5,200 columns and was designed by the Shandong Gausu Group. When it opens to traffic later this year, the bridge is expected to carry over 30,000 cars a day and will cut the commute between the city of Qingdao and the sprawling suburb of Huangdao by between 20 and 30 minutes.
 
MOD HEBU TUONDOLEE HUU UHARO HAPA, NI KUKOPI NA KUPEST VITU AMBAVYO HAVINA MASHIKO , CAG ASHAKANUSHA HABARI ZOTE HIZI ZA KIZUSHI NA UWONGO.
DARAJA LA MWALIMU NYERERE NI LA KWANZA UKANDA HUU KWA UBORA NA DR DAU NA NSSF NDIO MASTAA WA SHOO , UKIWA HUKUBALIANI NA UKWELI NA UHALISIA WA MAMBO USIPITE HILO DARAJA PERIOD
 
* uhalisia

pia hii ni copy & paste mada muflis alieleta yericko nyerere mwaka jana kama sikosei...

ilajadiliwa na majibu yapo kule....

lete mada mpya!
Wewe ujielewi hili daraja limemalizika mwaka jana?
 
MOD HEBU TUONDOLEE HUU UHARO HAPA, NI KUKOPI NA KUPEST VITU AMBAVYO HAVINA MASHIKO , CAG ASHAKANUSHA HABARI ZOTE HIZI ZA KIZUSHI NA UWONGO.
DARAJA LA MWALIMU NYERERE NI LA KWANZA UKANDA HUU KWA UBORA NA DR DAU NA NSSF NDIO MASTAA WA SHOO , UKIWA HUKUBALIANI NA UKWELI NA UHALISIA WA MAMBO USIPITE HILO DARAJA PERIOD
Mbona mnakinzana na mnayosema si serekali ya uwazi? Jibuni hoja
 
Back
Top Bottom